matthew2000
Member
- Apr 6, 2021
- 7
- 14
Sanduku la posta ni mali ya mtu, na mhusika anakaa na funguo.Lakini mi navyofahamu sanduku la posta ni kama kituo cha mzigo wako kufikia, sio lazima umiliki sanduku.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua posta unayotaka kupokelea hiyo barua. Mfano kama hiyo posta ipo Ubungo basi unachagua namba ya sanduku tu kwa mfano 100 na anwani yako itasomeka kama ifuatavyo:
SELMAX,
P.O BOX 100,
UBUNGO - DAR ES SALAAM
Barua itafika posta ya Ubungo kwenye sanduku 100 kwa jina la SELMAX. Na posta wanakupigia poa simu kama barua itakuwa na namba ya simu au ukienda kuiliza watakuuliza ulituma sanduku namba ngapi na jina ulilotumia mfano hapo, sanduku namba ni 100 na jina ni SELMAX.
Mimi hufanya hivyo ninavyonunua vitu AliExpress na huwa nabadili anwani kama nataka kupokelea mzigo sehemu tofauti.
Google hawana tatizo kabisa kwenye payments.Sasa mzee kwa hiyo views 50k unatakiwa uwe na hela kabisa. Binafsi sina blog ila kwa ninaosoma shuhuda za waandishi wa nje kwa views 50k unaweza ingiza mpaka $500 ukizingatia na niche yako ni nini. Umechelewa sana kuanza monetization. Tatizo kubwa sisi hatuna PayPal ambayo ni rahisi zaidi
Bongo sio wasomaji ukiandika Kiswahili unajichosha labda uwe famous kama kina Bongo5 na uandike umbea. Ningependa kujua zaidi kutoka kwako
Sanduku la posta ni mali ya mtu, na mhusika anakaa na funguo.
Ukitumia sanduku la posta la mtu au ofisi fulani hakikisha unamjua anayekaa na funguo za hilo sanduku.
Vinginevyo utapoteza barua yako.
Mkuu kwenye Wire transfer ya Bank Swift code kila tawi la bank linayo tofauti ?Tumia s.l.p ya shule ilio jiran yako
Hongera mkuuHatimae nimeweza kuthibitisha pin. Asanteni kwa mchango wenu
SWIFT CODE huwa ni moja tu kwa benki husika, mfano kama unatumia crdb bank swift yao ni CORUTZTZMkuu kwenye Wire transfer ya Bank Swift code kila tawi la bank linayo tofauti ?