Jinsi ya kuthibitisha PIN Google Adsense

Jinsi ya kuthibitisha PIN Google Adsense

karibu kwenye team ya adsense

kuhusu p.obox tafuta mtu,ofisi utumie box lao pIN zikifika utazipata kwa urahisi ila ukihitaji huduma ya box inapatikana kwa 5000.
kuhusu identify verification tumia ID ya mpiga kura.

karibu PM kwa maelezo zaidi
 
Lakini mi navyofahamu sanduku la posta ni kama kituo cha mzigo wako kufikia, sio lazima umiliki sanduku.

Unachotakiwa kufanya ni kuchagua posta unayotaka kupokelea hiyo barua. Mfano kama hiyo posta ipo Ubungo basi unachagua namba ya sanduku tu kwa mfano 100 na anwani yako itasomeka kama ifuatavyo:

SELMAX,
P.O BOX 100,
UBUNGO - DAR ES SALAAM

Barua itafika posta ya Ubungo kwenye sanduku 100 kwa jina la SELMAX. Na posta wanakupigia poa simu kama barua itakuwa na namba ya simu au ukienda kuiliza watakuuliza ulituma sanduku namba ngapi na jina ulilotumia mfano hapo, sanduku namba ni 100 na jina ni SELMAX.

Mimi hufanya hivyo ninavyonunua vitu AliExpress na huwa nabadili anwani kama nataka kupokelea mzigo sehemu tofauti.
Sanduku la posta ni mali ya mtu, na mhusika anakaa na funguo.

Ukitumia sanduku la posta la mtu au ofisi fulani hakikisha unamjua anayekaa na funguo za hilo sanduku.

Vinginevyo utapoteza barua yako.
 
Sasa mzee kwa hiyo views 50k unatakiwa uwe na hela kabisa. Binafsi sina blog ila kwa ninaosoma shuhuda za waandishi wa nje kwa views 50k unaweza ingiza mpaka $500 ukizingatia na niche yako ni nini. Umechelewa sana kuanza monetization. Tatizo kubwa sisi hatuna PayPal ambayo ni rahisi zaidi

Bongo sio wasomaji ukiandika Kiswahili unajichosha labda uwe famous kama kina Bongo5 na uandike umbea. Ningependa kujua zaidi kutoka kwako
Google hawana tatizo kabisa kwenye payments.

Watu wanachukulia pesa Western Union, Check, Bank ( Wire transfer ) n.k

Hakuna PayPal kwenye malipo ya Google.
 
Sanduku la posta ni mali ya mtu, na mhusika anakaa na funguo.

Ukitumia sanduku la posta la mtu au ofisi fulani hakikisha unamjua anayekaa na funguo za hilo sanduku.

Vinginevyo utapoteza barua yako.

Mzigo haupotei unaenda ofisini kwao wanauchukua wanakupatia na sio mizigo yote inaweza kaa kwenye vile vibox, ni mizigo midogo midogo kama bahasha na box moja haliwezi milikiwa na mtu mmoja au taasisi moja linawekuwa na watu wengi, kinachotofautisha ni majina tu ya hiyo anwani.
 
Kwa uhitaji wa Google AdSense account ipo.. imetoa pesa Mara moja fully verified ..
 
Nimekuwa nikisoma comments za watu humu wengi nimegundua hawana uzoefu na adsense au admob.
Binafsi nimekuwa nikijipatia kipato toka admob tangu mwaka 2015.
Ngoja nije kwenye mada.. nimeona wengi mkisema jinsi ya kupokea malipo ni shida sijui paypal haitumiki tanzania. Nani kasema google wanalipa kwa paypal?? Anyway walikuwa wanalipa zaman sio siku hizi. Sasa hiv google wanalipa kwa njia ya wire transfer (unatumiwa pesa kwenye account yako ya bank) hapa kuwa makini. Ukichahua njia hii hakikisha hiyo bank ina swift code na inakubali malipo ya dola. Kwa uzoefu wangu bank zote kubwa Tanzania zinapokea pesa kwa malipo ya dola. Mfano NMb, CRDB EQUITY bank n.k hizo bank nisha zitumia
 
Back
Top Bottom