BRELA
Govt Institution
- Dec 14, 2023
- 119
- 89
Habari! na Karibu, Leo kupitia video hii utajifunza Jinsi ya kutumia huduma ya usajili wa kampuni kwenye mfumo wa BOS unapotaka kufungua kampuni yako.
Baada ya kuingia kwenye mfumo utabofya sehemu ya Company Services, ukurasa ukifunguka utapata ordha ya huduma mbalimbali katika moduli ya kampuni.
Baada ya kuingia kwenye mfumo utabofya sehemu ya Company Services, ukurasa ukifunguka utapata ordha ya huduma mbalimbali katika moduli ya kampuni.
- Katika sehemu ya My Registry, hapa utapata taarifa za kampuni yako ambayo tayari imeshasajiliwa BRELA
- ‘Name Clearance:’ katika sehemu hii utaweza kuangalia kama jina la kampuni limetumika au bado halijatumika, hapa utaweza pia kuwasilisha maombi mapya, kufuatilia maombi yaliyowasilishwa na maombi yaliyokamilika.
- New Company: Kwa kubofya sehemu hii, utaweza kuwasilisha maombi ya kusajili kampuni kwa kuchagua aina ya kampuni unayotaka kusajili. Private Company, kwa kampuni ya watu wawili na kuendelea, Public Company kwa kampuni ya Umma pamoja na Foreign Company kwa kampuni ya Kigeni
- Change Details: Katika huduma hii, mmiliki wa kampuni utaweza kufanya mabadiliko mbalimbali ya taarifa za kampuni, kuanzisha maombi mapya ya mabadiliko, kufuatilia maombi yaliyokamilika, maombi yaliyorudishwa na maombi yasiyokamilika.
- Data Updates: Kwa kubofya sehemu hii, utaweza kuhuisha taarifa za kampuni yako, kufuatilia maombi yaliyokamilika, maombi yaliyorudishwa kwako na maombi yasiyokamilika.
- Filling Servicess: Katika huduma hii utaweza kuwasilisha taarifa za mizania ya mwaka, taarifa za fedha kwa mwaka ikiwa kampuni ya kigeni, kufuatilia maombi yaliyokamilika, maombi yaliyorudishwa kwako na maombi yasiyokamilika.
- Charges Services: Huduma hii itakuwezesha kuwasilisha maombi ya usajili wa haki ya dhamana ya mali inayowekwa juu ya kampuni (Registration of Charges) pamoja na Utilimishaji wa dhamana juu ya mali iliyowekwa na kampuni (Satisfaction of Charges).
- Winding Up, Kwa kubofya sehemu hii utapata huduma ya kufunga kampuni yako endapo utahitaji kufanya hivyo.
- Striking Off: Katika huduma hii itakusaidia kufuta kampuni yako kwa idhini ya msajili kwa kampuni zote zilizoshindwa kuwasilisha taarifa kwa muda mrefu.