Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Hivi unajua kwenye simu yako unaweza kumpigia mtu simu kupitia wifi sio lazima hutumie line iliyopo kwenye simu yako ??
Najua wengi walikua hawajui hii ๐ Leo nakujuza kupitia @bongotech255 usisahau ku share kwa wengine tujifunze sote.
Wifi calling, ni Teknolojia inayokuwezesha kupiga simu na kutuma ujumbe (message) kupitia mtandao wa wifi ikiwa line yako haifanyi kazi au eneo ulilopo mtandao huko chini.
Mfumo huu unafanya kazi ikiwa simu yako imeunganishwa na wifi, unafanyaje kuunganisha mfumo huu kwenye simu yako.
Fungua simu yako Kisha ingia setting kwenye simu yako
Kisha >> calls >> wifi calling >> kama simu yako Haina mfumo huu pia unaweza tumia mfumo wa voice over IP calling utaiona kwenye simu yako.
Watumiaji wa iphone ingia setting Kisha phone halafu chagua wifi calling weka on โ.
Baada ya kuunganisha Sasa utaweza kutumia wifi kuweza kupiga simu kama unavyopiga ukiwa na line ya simu yako.
Kwani ukiwa imeunganishwa utaona neno "internet call" au "Wifi calling" kupitia notification iliyopo kwenye simu yako.
#wificalling #bongotech255