Chaula_J
New Member
- Jul 23, 2022
- 3
- 3
Kila mtu katika maisha ana malengo yake ya kimafanikio, yanaweza kuwa mafanikio ya kiuchumi, kisiasa, kielimu au katika nyanja nyingine zozote za kijamii. Lakini watu wengi hushindwa kutimiza malengo yao kama vile walivotarajia kutokana na sababu tofautitifauti, ikiwemo matimizi mabaya ya muda wao. Makala hii ina lengo la kumpasomaji mbinubalimbali za namna ya muutunza muda na kuutumia muda vizuri na hatimaye kutimiza malengo yao. Bila kupoteza muda basi nipende kua!za mijakwa moja kwa kueleza mbinu hizo za kutunza muda.
1.Kuwana lengo madhubiti.
Jambo la kwanza kabisa ili mtu uweze kufanikiwa ni lazima uwe na lengo. Lengo linaweza kuwa lolote kulingana na wewe unataka kuwa nani ama unataka kufanya nini. litakuwa kama dira ya kukuongoza katika kila unachokifanya, Hivyo hautapoteza muda kufanya mambo mengi ambayo hujui unaelekea wapi ama unataka ufike wapi.
2. Zingatia kitu ama kazi unayofanya kwa wakati thabiti.
Unapoamua kufanya jambo basi hakikisha hauna jambo lingine unalolifanya yaani kufanya jambo moja huku unafikiria lingine kwa wakati mmoja, ukifanya hivyo utashindwa kulimaliza lile ulilokuwa ukilifanya ama kutolifanya kwa usahihi hivyo ukajikuta umepoteza muda.
3. Tenga au gawanya muda wako katika makundi kulingana na kazi.
Hapa utatakiwa kulipa kila jambo unalolifanya muda wake maalumu. Kwa mfano una vitu 10 vya kufanya kwa siku, basi hakikisha muda wako wa siku moja umeugawanya katika hayo mambo yako unayotaka kuyafanya na kuyatimiliza katika siku hiyo. Hii itakusaidia kujenga fikra kuwa usipomaliza jambo hilo kwa wakati utakuwa umeharibu ratiba zingine, hivyo utawaka juhudi na maarifa zaidi ili hatimaye uweze kumaliza mambo yote kwa wakati wake.
4. Tumia muda wako wa ziada.
Hapa namaanisha unapopata muda wa ziada (muda baada ya kumaliza majukumu yako makuu ya siku, au muda mwingine ambao haufanyi majukumu yako makuu, kwa mfano wakati wa likizo, muda ukiwa safarini nk.) unaweza kutumia muda huu kufanya yale mambo ambayo hukuweza kufanya wakati wa siku za kawaida kwa sababu ulibanwa na majukumu mengine. Hii itakusaidia kupunguza mrundikano wa mambo ya kuyafanya pindi unaporejea katika majukumu yako makuu.
5. Kusanya mambo yanayofanana na uyafanye kwa wakati mmoja (Batching).
Hapa tunamaanisha kufanya mambo ambayo yanaendana na ambayo yanaweza kufanywa kwa wakati mmoja. Yanaweza kuwa yanaendana moja kwa moja kwa maana ya kuwa na sifa zinazofanana lakini pia yanaweza kuwa yanaendana kwa maana ya mahali pa kuyafanyia. kwa mfano ukienda kununua bidhaa nje ya mkoa kwa ajili ya biashara yako, unaweza pia kufanya manunuzi ya mahitaji yako mengine ya msingi. Hii itakusaidia kupunguza usumbufu wa safari za mara kwa mara, na hatimaye ukawa umeutunza na kuutumia muda wako vizuri na kwa usahii.
6. Jifunze kusema "hapana" kama kuna upazima ama umihimu wa kufanya hivyo.
Hapa tunamaanisha si kila ombi ama kitu unachoambiwa kukifanya basi ukubali kwa kuwa unaweza kukifanya kitu hicho. Unaweza kuwa unaweza kufanya jambo vizuri sana lakini ukakosa muda wa kulifanya jambo hilo, kukataa kulipokea na kulikubali jbo hilo kutakufanya upunguze mrundikano wa mambo mengi ya kufanya hivyo kuwekeza zaidi katika vile vitu unavyoweza kuvimudu na hatimaye ukawa umefanikiwa kutumia muda wako vizuri
7. Jifunze kugawanya majukumu(delegation of tasks).
Hapa ninamaanisha, pale unapoona una mambo mengi na yanakuzidia basi jifunze kuwapa watu wengine pia wakusaidie kuyatimiliza majukumu hayo. Kwa mfano kama unatakiwa kuwepo sehemu fulani kwa ajili ya kutoa huduma fulani, na muda huohuo unahitajika sehemu nyingine kwa ajili ya huduma hiyohiyo, basi unapaswa kumwachia mtu mwingine mwenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ili akusaidie. Hii itakusaidia kufanya mambo yako kwa ufasaha, vilevile utafaidika kwa maana ya kupata muda wa kutosha na wa kutulia kufanya huduma yako kwa utulivu zaidi.
Hizo ni baadhi ya njia za muhimu ambazo unaweza kuzitumia kuutunza muda wako na hatimaye ukaweza kufanikiwa katika malengo mbalimbali. Mwisho kabisa nikutakie kila la kheri mdomaji wa makala hii.

Upvote
1