Jinsi ya kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio

Jinsi ya kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Ujasirimali ni uzinduzi, ubunifu na uendeshaji wa biashara then kuwa na uwezo pamoja na nia ya uendelezaji wa hiyo biashara.

Unapokuwa mjasiriamali inamaanisha unatakiwa kupitia mchakato wa kuandaa na kusimamia mradi wa biashara pamoja na risk yoyote itakayojitokeza ili kutengeneza faida.

-Kuwa mjasiriamali bora inakuhitaji msukumo na kujitoa.

-Kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio inakuhitaji uwe mjasiriamali bora mwenye usimamizi mzuri na nguvu ya kujiinua.

>>>>Zifuatazo ni njia za kufanya uwe Mjasiriamali bora na mwenye mafanikio.


1. SIKU ZOTE INAANZA NA SHAUKU (PASSION),..

-shauku ndio itakufanya upate wazo bora.

-shauku ndio itakufanya usiogope kufeli.

-shauku ndio itakupa ujasiri wa kuingia na kuendelea.

2. CHUKUA NAFASI YA KUJIPA CHANGAMOTO (CHALLENGE YOUR SELF)

-Usiogope kuchukua risk.

-Fanya maamuzi ambayo haujawahi kufanya maishani mwako juu ya kutafuta fursa.

-Fikiria kuwa hauwezi kuishi bila ujasiriamali.

3. USIFIKIRIE JINSI INAVYOFIKIRIKA, FIKIRIA JINSI YA KUFANYA WAKIFIKIRIE TOFAUTI INAVYOFIKIRIKA.

-Gundua kile watu wanachokosa, ifanye kama furasa kwako na tafuta njia ya kuwafanikishia.

-Tambua kile watu wanachopenda na wanachokihitaji, ila tafuta njia mbadala ya kuwafikishia tofauti na zile zilizoeleweka.

-Ingia katika mfumo uliozeleweka , tafuta njia ya kuboresha miundombinu ya kulahisishia mfumo huo tofauti na wengine.

4. JIFUNZE KUWA GENERALIST (MWANA-UJUMLA) ILA PALE UTAKAPOKUWA HAUNA MAARIFA KWA AJILI YA USIMAMIZI WA MOJA YA SEKTA YA BIASHARA YAKO THEN UNAWEZA KUAJIRI MTU ALIYE NA MAARIFA HAYO.

-Usimamizi wa hatari za kifedha na za uendeshaji (financial and operation risk)

-Usimamizi wa fedha na uhasibu (Financial management and accounting)

-Utengenezaji wa mpango mkakati wa mauzo, masoko na promtion ya bidhaa au huduma.

5. BORESHA UFAHAMU NA UJUZI WAKO (KNOWLEDGE AND SKILLS)

-Jifunze kutoka kwa biashara zilizofanikiwa na zile zilizo feli

-Kuongeza kiwango chako cha elimu

-Kuhudhuria na kuwa sehemu ya semina na vikundi vya ujasiriamali.

-kupata mentor.



Sent using Jamii Forums mobile app
Y
 
Pia mjasiriamali aelewe kitu anachofanya ili aweze kukifanya kitu hicho kwa ubora ili kimletee faida,.hapa elimu juu ya ujasiriamali inahusika,.
 
Pia mjasiriamali aelewe kitu anachofanya ili aweze kukifanya kitu hicho kwa ubora ili kimletee faida,.hapa elimu juu ya ujasiriamali inahusika,.
Ya ni kweli Mother Confessor ..unatakiwa kufanya lile unalo weza kufanya kwa ubora na usiloliweza itakuhitaji kupata elimu yake zaidi na mafunzo ya uendeshaji wake... Lakini pia baada ya elimu, itarudi tena kwako kama utahitaji kufanikiwa zaidi inatakiwa usifanye kama inavyozoeleka itakubidi ufanye ubunifu na kutafuta style mpya yenye mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya ni kweli Mother Confessor ..unatakiwa kufanya lile unalo weza kufanya kwa ubora na usiloliweza itakuhitaji kupata elimu yake zaidi na mafunzo ya uendeshaji wake... Lakini pia baada ya elimu, itarudi tena kwako kama utahitaji kufanikiwa zaidi inatakiwa usifanye kama inavyozoeleka itakubidi ufanye ubunifu na kutafuta style mpya yenye mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam,.Ubunifu ni sifa kuu ya mjasiriamali,lazima awe nayo ili kuleta ushindani wa soko,mvuto wa kazi yake na faida katika kile akifanyacho.
 
easier said than done..mara nyingi mtu kama mtoa mada utakuta hajawahi kufanya hata biashara ya chips...ni theory tu za kufa mtu.....
 
easier said than done..mara nyingi mtu kama mtoa mada utakuta hajawahi kufanya hata biashara ya chips...ni theory tu za kufa mtu.....
Ndio kawaida ya wabongo kama nyie...

Roho mbaya inakuwa juu juu na mchanganyiko wa fitna na wivu.

On wht evidence do u have that i am not an entrepreneur ....natoa hapa mada kwa ajili ya kusaidia na kuhamasisha watu, sio kwa ajili ya wenye negative thinking kama wewe.

Grow up...or u will remain stupid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mfanyabiashara na mjasiliamali wana utofauti gani
Nitajaribu kukuelezea kwa mifano...

-Tuseme kuna john na jane.

-john ameanzisha biashara ya chipsy na mishikaki.

-jane amegundua jiko lenye kurahisisha uaandaji wa chipsy na ameliweka sokoni kwa ajili ya kuliuza.

So..john ni mfanyabiashara wa chipsy na mishikaki ila jane ni mjasiriamali.

Tuseme kuna frank na florah

-frank analangua matikiti maji kutoka shambani na kuyaleta mjini na kuyauza katika vipande.

-florah ametengeneza website inayowakutanisha walanguaaji wa matikitiki maji, wenye shamba la matikiti maji na wanunuzi wa reja reja wa matikiti maji .

So john ni mwana biashara na jane mjasiriamali


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom