Jinsi ya kuwa muuzaji mzuri watu wengi wanunue kile unachouza

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ili ufanikiwe katika maisha lazima uwe muuzaji(sales person) mzuri

Hizi ni mbinu unazoweza kutumia katika kuuza bidhaa, huduma au siasa.

1. Taja namba/sifa kubwa kubwa zinazovutia watu kusikiliza lakini ambazo itakuwa vigumu wao kuzifuatilia.

2. Rudia mara kwa mara ubora wa bidhaa,huduma, sera. Binadamu anapolisikia jambo mara nyingi zaidi ni rahisi kuliamini hata kama ni la uongo, duni au haliwezekani.

3. Zungumza kile watu wanachopenda kusikia hata kama hakitekelezeki au hakina uhalisia na bidhaa yako.

4. Jifanye unajua vitu ambayo huvijui ila unadhani watu wanaamini unavijua.

5. Onyesha kwamba umetokea mazingira ya shida sana na umepambana sana kufika hapo ulipo, kuteka hisia ni jambo muhimu katika biashara na siasa sio mapenzi tu.

6. Jaribu kufanya utani, usiwe serious sana.

Zingatia: Uzuri au ubovu wa stori yako ni jambo la pili, jambo la kwanza watu wengi kukuamini ni jinsi unavyoisema stori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…