Jinsi ya kuwa na aina ya Mahusiano unayoyataka na Mwanamke

Jinsi ya kuwa na aina ya Mahusiano unayoyataka na Mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Unaweza kuwa kwenye mahusiano lakini si vile unavyotaka. Unaweza ukawa unanyimwa unyumba. Au mwanamke anakuendesha. Au unasalitiwa mara kwa mara. Au mwanamke king’ang’anizi wa vitu. Au mwanamke anataka kukubadili misimamo yako kila muda.

Na hali hiyo ikawa inajirudia kwa kila mwanamke unayekua naye. Tatizo sio mwanamke. Tatizo ni kwako mwenyewe. Ndio maana ni muhimu ujijue kwanza kabla ya kulaumu mwanamke hafai. Ni muhimu ujiangalie kwanza wewe na ujihakikishie kuwa we ni mtu sahihi kwa mahusiano unayohitaji.

Kwanini uanze kujiangalia wewe? Sababu ndege wafananao huruka pamoja. Watu tunakua pamoja na kuelewana sababu ya tabia. Huwezi kuwa na mtu umtakaye kama we mwenyewe hauna tabia za kufanana naye. Huwezi kutaka uaminifu wakati huna tabia hiyo.

Huwezi kuwa na mwanamke mwenye shukrani wakati we mwenyewe huna shukrani.

Huwezi kuwa na mwanamke mwenye changamoto nzuri wakati we mwenyewe huna changamoto nzuri. Huwezi kuwa na mwanamke anayetumia hela vizuri kama huna matumizi mazuri ya pesa we mwenyewe. Tabia zako ndio zitakupatia mwanamke unayemuhitaji au mwanamke atakaye kuumiza. Unaweza pata mwanamke anayejielewa kabisa, lakini moyoni mwako unaona hustahili kuwa naye.

Sababu tabia zake ni mpya kwako, hujazoea hali hiyo. Lazima utampoteza. Unaweza jikuta unabaki na uchungu na majuto. Kujiangalia tabia na kutaka kurekebisha tabia ni jambo gumu. Ndio mana wengi huishia kwenye mahusiano wasiyoyataka, hukata tamaa. Lakini sio lazima iwe hivyo.

Cha kufanya.
Badilisha mitazamo na misimamo.
Ni muhimu mwanaume kusimamia mtazamo na msimamo wako. Lakini pale unapoona haufanyi kazi, usiwe mbishi kubadilika. Unaweza kuwa na mtizamo kuwa wanawake wote malaya, utaishia kuvutia wanawake ambao hawajui thamani ya uaminifu. Na ukipata mwaminifu, bado utakua humuamini na atajiona humthamini atakuacha. Angalia mitazamo yako ndio inayokuongoza maishani.

Utaijuaje mitazamo yako?
Utaijua kwa kujijua au kujua vitu;
Unavyopenda kusikiliza.
Unavyopenda kuangalia.
Unavyopenda kuongea au
Unavyopenda kuwa karibu navyo.

Kama mtazamo wako ni ‘wanawake ni maua mazuri kwenye jamii’ utajikuta unapenda stori zinazoonesha kuwa wanawake ni wazuri na wanawake unaokutana nao wanakua wasafi wa moyo pia.

Kama mtazamo wako ni ‘wanawake wote malaya’ stori utakazosikiliza au maneno unayoongea yatakua yanaonesha wanawake sio watu wa kuwaamini, au uwachezee tu uwaache. Na wanawake utakao kutana nao ni wale ambao hawana mpango kukaa maishani mwako. Na ukimpata anayefaa hutoweza kumtunza.

Hata nyimbo unazosikiliza zinachangia, kama unasikiliza nyimbo za kuvunjwa moyo sana, tegemea utavunjwa moyo. Kama una mtizamo pesa ndo kila kitu hata mwanamke utakayemvutia ni yule atakayekua anategemea pesa yako kwenye kila kitu hadi vitu vidogo vidogo.

Jilazimishe kuishi kwenye mtazamo mpya/ hali mpya.
Ukishatambua mitazamo yako.
Na umeamua kuibadili ili upate unachokitaka. Ni muda wa kukubali hali mpya utakayokutana nayo. Sababu unapitia mabadiliko. Mwanzoni itakua ngumu, sababu hujui usichokijua. Utajikuta unafanya makosa mengi.
Lakini sio tatizo. Utajilazimishaje kuwa na mtazamo mpya? Kwa kubadili unachokiingiza kichwani.

Ni kama vile chakula mwilini, ili uwe na afya ya muda mrefu, lazima uwe makini na kile unachokiingiza mwilini.
Angalia stori unazosikiliza, kisha badili na kuanza kusikiliza zile zinazoendana na malengo yako. Angalia maneno unayoongea na ubadili yako yawe yanaendana na malengo yako. Kisha rudia, hadi iwe tabia rasmi.

Changamoto za hapa na pale zisikufanye ukapoteza picha ya malengo yako. Hata tabia na mitazamo uliyonayo sasa ilianza taratibu.

Yote hayo ni tabia tu. Ni muhimu ukubali kuwa unatengeneza tabia mpya itakayokusaidia kuwa na mahusiano unayotaka. Japo utapata shida mwanzoni ila ukishazoea utafurahia. La sivyo utaishia kufanya kitu kile kile kwenye kila mahusiano na mwanamke unayebadili. Na kuona wanawake wote hawafai.
 
Back
Top Bottom