Jinsi ya kuwadhibiti wafanyakazi waizi kwenye biashara yako

Jinsi ya kuwadhibiti wafanyakazi waizi kwenye biashara yako

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
Ili kujilinda Dhidi ya Wafanyakazi Wasioaminika fanya yafuatayo:

1. Fanya Uajiri wa Kiuchunguzi (Due Diligence)

Usikurupuke kumpa mtu kazi kwa sababu kaonekana mpole au amesema ana shida. Fanya yafuatayo kabla hujamkabidhi chochote:

Pata taarifa zake kamili – jina halisi, namba ya simu, kitambulisho, mahali anapoishi (na uthibitisho).

Wasiliana na referees alioweka. Uliza kama walishawahi kumwajiri au kumjua kimaadili.

Angalia historia yake ya kazi – je, alishawahi kufukuzwa? Kwa nini?

Ikiwezekana, andika mkataba wa dhamana na mtu mwingine (mfano mzazi, ndugu au rafiki wa karibu) atakayewajibika naye endapo atafanya uharibifu.

2. Tumia Mikataba ya Ajira ya Maandishi

Mkataishe kila mfanyakazi kwa maandishi. Hii ni kinga yako ya kwanza.

Andika majukumu, muda wa kazi, mshahara, na adhabu endapo kutakuwa na uvunjifu wa maadili.

Jumuisha kipengele cha "fidia ya uharibifu" endapo mfanyakazi ataiba au kusababisha hasara.

Hakikisha mkataba unasainiwa mbele ya shahidi na unapewa nakala yake na yeye.


4. Tengeneza Mfumo wa Ufuatiliaji Kazini

Usiache kazi au biashara mikononi mwa mtu bila mfumo wa kudhibiti. Fanya hivi:

Weka daftari la kila bidhaa au mapato – kila anachouza au kukusanya kiandikwe na kusainiwa.

Tumia receipts au POS (kama unaweza) – ili kuwe na kumbukumbu ya kila malipo.

Fanya ukaguzi wa ghafla – hata usiku au siku ambazo hafahamu.

Kama ni usafirishaji au pikipiki, wekwa GPS tracker.

Kama biashara yako ina uwezo, weka CCTV, hata kama ni kamera moja tu kwa duka au kaunta.

Watu ni wa kuaminiwa pale tu ambapo kuna mfumo wa kuwawajibisha.

Uaminifu bila ufuatiliaji ni mwaliko wa wizi.
Lazima biashara iwe na kinga, sio hisia tu.
 
Kupigwa kupo tu hasa ukishajaa kwenye mfumo !!

Mimi nina slogan moja tu sijui ni ya kizee/kizamani/kiuoga ama kwa namna yoyote ile nitaipokea !!!

Simpi mtu back kaz ama connection!!! Lazima nikufahamu vyema background yako kuanzia ww mwenyewe, kwenu ndugu zako n.k,,,, ! Likitokea lolote niwe na pakuanzia !!!

Watu wamekuwa wanyama, hakuna uaminifu kabisa!
 
Ajiri unayemfahamu ili akitokomea ujue pa kuanzia
 
Si wanafanya mpaka Vetingi huko serikalini.....vipi kuhusu wizi, umekomeshwa

Wizi na Ukahaba ni shughuli kongwe duniani,
 
Back
Top Bottom