Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Mkuu usimamie vipi?
- Mfano unamagari ya Biashara mabasi uwe unayaendesha mwenyewe? au uwe kondact wa mabasi yote? utasimamia biashara yako lakini huwezi simamia katika operation zote,
- Hakuna biashara ambayo utakua nayo wasikuibie wakiamua,
- Labuda uwe na TAX NA WEWE NDO DREVA NA WEWE NDO KONDACTA NA WEWE NDO UNAJAZA MAFUTA NA WEWE NDO UNAPELEKA GARI GEREJI
- Wahindi huwa wanasimamia maduka yao asubuhi hadi jioni lakini wanaibiwa wakiwa hapo hapo, sasa wewe unaongelea usimamizi wa aina gani?
- Wafanyakazi wako hata sekunde 50 zinatosha kukuibia na wala hawahitaji saa nzima, kitendo hata cha kwenda chooni kinatosha wao kukuibia,
- NA WIZI UKO KATIKA VITU VINGI SANA MKUU NA SI KWENYE PESA TU
- wanaweza kukuibia pesa sawa
- Watakuibia bidhaa zako
- Watakuibia katika manunuzi
- Watakuibia katika matengenezo
- Watakuibia muda
NILAZIMA UWAJENGEE UWEZO WAFANYAKAZI WAKO NA UWAPE ELIMU YA KUTOSHA NA UWALIPE VIZURI NA KUWAPA STAHIKI ZINGINE,
Komando,
Sio lazima usimamie mwenyewe. Unapofanya biashara yoyote kipimo ni pesa unayopata. Kama unazo taxi, waambie madereva wako kuwa ikifika jioni unataka kiasi fulani. Na akishindwa kutimiza masharti haya kwa kipindi fulani mfukuze kazi.
Vilevile kama wewe unaogopa kufanya biashara kwa sababu kuna aina nyingi za wizi, tafuta kazi ya kuajiliwa. Kwani biashara ina risks zake.