jinsi ya kuwadhibiti watu tuliowajiri ktk biashara zetu wasituibie.


Komando,

Sio lazima usimamie mwenyewe. Unapofanya biashara yoyote kipimo ni pesa unayopata. Kama unazo taxi, waambie madereva wako kuwa ikifika jioni unataka kiasi fulani. Na akishindwa kutimiza masharti haya kwa kipindi fulani mfukuze kazi.

Vilevile kama wewe unaogopa kufanya biashara kwa sababu kuna aina nyingi za wizi, tafuta kazi ya kuajiliwa. Kwani biashara ina risks zake.
 
Kipapai ni dawa tosha,
Kama ni mwanaume basi akigusa tu anageuka Mlupo
 
hebu twende na mfano wa guest house ya vyumba 21
una chaji kila chumba sh 10000......

na umeajili watu wa tatu wasimamizi na wasafishaji

na imetokea umesafiri wiki mbili

utawezaje kuzuia wasikuibie?

mkuu hapa nadhan ndio teknolojia inaweza kusaidia kudhibiti.
cctv camera na mashine za cash register zinaweza kusaidia.
 

asante kwa ushauri mkuu.
Ila mkuu kwanza hii inabidi iwe ni biashara kubwa yenye kuingiza pesa ya maana,si kila mfanyabiashara anaweza kuyafanya haya kwa wafanyakazi wake.
Na pia,hata ukifanya hivi,siku zote wafanyakazi wakipata mwanya wa kupata cha ziada wataiba tu.
Katika hali halisi mim naona hii sio dawa ya kudhibiti wizi.
 

mkuu ushauri wako ni mzuri asante,ila hapo pakuwa mkatili patanishinda ni bora nimuondoe mtu kuliko aendelee kunisaidia huku nikimfanyia ukatili kama njia ya kumdhibiti,naona hiyo ndo itafanya waniibie bila hata huruma.
 

asante dearest.
Kipengele cha kutokuanao rafiki sana inabidi nikifanyia kazi,mim nimezidisha sana matani na urafiki na wafanyakazi wangu.Kumbe ni tatizo nitalishughulikia na kufuata pia yote uliyoshauri.
 
mkuu umeongea sawa,elimu na mshahara mzuri kulingana na kipato cha biashara ni muhimu,lakini huwezi tu kutegemea kufanya hivyo ukaamin kwamba hawatakuibia.Kama kuna nafasi za kuiba wataiba tu.Bado elimu na mshagara mzuri sio mbinu yakuwadhibiti.
 
Bibie ume raise very important point kwenye biashara kwani biashara ina element mbili

Mapato (faida) na Matumizi, plus hasara ikiwemo uwizi wa aina mbalimbali

Kuhus kudhibiti wafanyakazi naomba nikupe mfano wangu sijui unafanya biashara gani

a. Fahamu kwa uhakika margin ya mapato ya siku (average) hii inatokana na wewe kukaa kwenye sehemu ya biashara hiyo kwa muda wa kutosha..then hiyo inakuwa benchmark ya ku-detect uwizi ikiwa faida (mapato yamepungua sana kwa siku kadhaa...STUKA

b.Hakikisha wafanyakazi wako wanalipwa on time (hata kama kuna nini? very impotant) hata kama uko kwenye difficulties wafanya kazi stahili zao zipatikana haraka iwezekanavyo na waone kuwa kweli owner anajali stahili zao in case manager wao wanawazengua

c. Internal infomer na external field visit, internal atakusaidia kupata uwizi na mawazo ya wafanyakazi kuhusu biashara yako na kazi, external visit ni kama auditing ya mara kwa mara bila taarifa..

d. Angalia sana usifukuze wafanyakazi wako (ni hatari) wafanyakazi wakishajua kuwa hapa turnover ni kubwa wanajua owner ni mnoko kwa hiyo wanakula haraka..(hapa na concur na yule jamaa aliyeshauri elimu na uhakika kuwa hii kazi ni kudumu kwake na kwako..

nitaendelee...
 
mkuu hapa nadhan ndio teknolojia inaweza kusaidia kudhibiti.
cctv camera na mashine za cash register zinaweza kusaidia.
CCTV guest? utakimbiwa na wateja woote. Any way control measures inategemea aina ya biashara na u need more than one offcourse. Na measures zinaanza tangu unapo hire, treatment ya wafanyakazi wakiwa kazini na separation wanapoacha kazi.

Waajiri wengi wa bongo huwafanya wafanyakai wao kuwa watumwa, hali inayofanya wakate tamaa na wasiheshimu kazi kwani waweza kuwa fired bila notice. Wafanye wafanyakazi wako wapende biashara na kuona kama ni yao. Incentive kama kuwapeleka short courses na zawadi ya sikukuu yaweza kusaidia.

Matumizi ya tekinolojia kama computer na cctv yaweza kusaidia lakini inategemea aina ya biashara na jinsi ulivyodesign mfumo wa utendaji kazi .

Separation of responsibilities pia ni muhimu. kwa mfano kwenye guest waweza kuwa na cashier na house keeper.Keshia anapokea fedha tu na house keeper anatunza funguo na ku update room status. kila mmoja ana keep daily recods zake. wewe utakua una verify kwa kumatch the two records.

Wabongo wooote ni wezi, hata mimi ni mwizi.
 

Kutumia teknolojia hapa ndio kikomo cha wizi. Kama una guest weka milango inayofunguka kwa kadi, chumba hakifunguki bila login details na mambo mengine muhimu kwenye software kukamilika. Hata kama haupo hawawezi kuuza vyumba bila funguo, actuially hata umeme chumbani hautowaka kama hujaanza kuingiza details kwenye computer...
Kudhibiti wizi inahitaji clever approach. Na hizi zinavary kwa kila aina ya biashara.
 

mkuu nashukuru kwa ushauri.
cctv guest inaweza kutumika mapokezi bila ya wateja kufahamu kuwa ipo pale.Kumbuka hata ktk mahoteli makubwa ambayo watu pia huyatumia kwa mambo yanayofanyika guest kuna cctv cameras,cha msingi ni kuhakikisha matukio yanayorekodiwa yanaheshimiwa kwa aidha mim mmiliki tu ndiye ninayeweza kuona kilichorekodiwa na sio kila mtu.
 

wazo zuri sana mkuu lakini hii inahitaji mtu uwe na uwezo wa kuweka hiyo teknolojia maana sidhani kama ni ya bei rahisi.Kwa hizi guest za kawaida kawaida sidhani kama wataweza kumudu hizi gharama.
asante kwa wazo lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…