Jinsi ya kuwafanya wateja wako wajione wanatumia bidhaa au huduma yako kabla hawajanunua

Jinsi ya kuwafanya wateja wako wajione wanatumia bidhaa au huduma yako kabla hawajanunua

Adama H

Member
Joined
Jan 9, 2026
Posts
28
Reaction score
66
Rafiki

Sasa ivi ni saa 9.30 asubuhi.

Ndio muda ambao nimeamua kukuandika makala hii fupi na kwanini nimekuandika makala hii muda huu. Nimekuandika makala hii wewe mjasirimali, Mfanyabiashara unayehangaika kupandisha mauzo ya Biashara yako upate kujifunza na kufahamu moja ya mbinu ya siri itakayokusaidia kupandisha mauzo ya Biashara yako ndani ya usiku mmoja.

Nisikuchoshe, twende pamoja

Mbinu za jinsi ya kufanya Mauzo ya Biashara/ Huduma;

Kuna hizi mbinu za kawaida ambazo unafundishwa na kuhubiriwa usiku na mchana na watalamu feki kama vile kutumia watu wenye ushawishi, kujiweka kama mtaalamu nk.

Sasa leo sahau kuhusu hizo mbinu za kawaida unazohubiriwa na watalamu feki kila siku uzitumie ila leo ndani ya second 60 zijazo nataka nikukabidhi moja ya mbinu ya hatari sana inayotumiwa na Guru wa Mauzo.

Kupandisha mauzo ya makampuni na Biashara tofauti tofauti na mbinu Hiyo inaitwa feature pricing.

Je, feature pricing ni Nini?
Feature pricing ni pale ambapo unamfanya mteja wako aanze kujiona anatumia faida zilizopo kwenye bidhaa yako kabla hata hajanunua hiyo bidhaa. Kwa lugha rahisi unamuonesha maisha ya kesho kupitia bidhaa Yako. Kwa mfano, kama unauza Fridge Ya Hisense Rd 27 litre 205 wakati unaelezea vipengele na faida za hivyo vipengele vilivyopo ndani ya Fridge kwa mteja wako.

Badala ya Kusema Fridge Hii ina milango miwili sehemu ya juu na Chini, sehemu ya juu ya Fridge itakusaidia kufanya Vinjwaji na Vyakula vigande na sehemu ya chini itakusaidia kufanya Vinjwaji vyako vipate baridi ya wastani bila kuganda.

Wewe sema Hivi kwa mteja wako "Hebu jaribu Kufikiri siku ya ijumaa jioni umerudi kazini umefika nyumbani (Sebleni kwako ) Moja Kwa Moja unaelekea sehemu lilipo fridge lako la Hisense la Milango miwili. Kisha Unafungua mlango wa juu wa Fridge Yako ya Hisense alafu unatoa Juice Yako ya Matunda iliyoganda vizuri kisha unamimina kwenye Glasi ya Udongo baada ya Hapo unaelekea kwenye kochi unakaa na Kuanza kuinywa taratibu huku uchovu wa kazi ukiondoka taratibu mwili mwako."

Je kwanini Mbinu Hii inafanya kazi kama wazimu kwenye ulimwengu wa Mauzo ni kwasababu inamjengea mteja wako picha kichwani mwake ajione anatumia Bidhaa Yako wakati kiuhalisi hiyo Bidhaa hana mkononi mwake.

Kwenye ulimwengu wa Mauzo Kuna msemo unasema ukiweza kumfanya Mteja wako Ajione Tayari kaanza kutumia Bidhaa auHuduma Yako. Kabla Hajanunua Basi Fahamu kabisa asilimia 99.9 anunua Bidhaa Hiyo Na Mbinu Hii inafanya kazi kwenye Bidhaa/ Huduma yoyote Ile unayouza.

Mbinu Hii unaweza kuitumia wakati wa Kufanya Matangazo ya Bidhaa/ Huduma Yako au wakati unaelezea faida za Bidhaa/ Huduma Yako Kwa wateja wako.

Gracia

Mtwa Mkwawa Kiboko ya wajerumani​
 
Kwa mfano unafanya biashara ya ng'ombe je utamwambiaje mteja ili umshawishi kujiona amenunua hata kabla hajanunua... Adam H
 
Kwa kufuga
Unawaonaga wamasai wanavyouza ngombe minadani mara nyingi

wanavyokushawishi kwa kukwambia maneno ambayo yatakufanya ujione tayari unamiliki ngombe wengi mfano mara nyingi utasikia wanasema

ukinunua huyu ngombe lazima zizi lako lijae atakazulia watoto wengi Hadi utaongeza zizi jingine

Unaona uyu Ngombe ukinunua Kila siku asubuhi utakuwa unakamua maziwa ndoo tatu

Mara nyingi kwenye mifugo Hasa hii ya kufuga watu wengi kabla Hawajanunua Huwa wana angalia uwezo wa huyo myama Kuzaa na uwezo wake wa kutoa maziwa


Kwa ufupi wewe unahitajika kujenga ujuzi wa closing skills ( jinsi ya Kufungua Mauzo sababu Mauzo ya ngombe Huwa

yanafanyika ana kwa ana hasa minadani kwahiyo unahitajika ujenge Huu ujuzi kwa Kiwango kikubwa ili kwa Kila mteja atakaye kuwa anakuja kwako kununua ngombe uwe na uwezo wa kumuuzia kwa asilimia 99.9

Na unahitajika ujenge ujuzi wa Kuuza Bidhaa za Bei kubwa high tictek

Kama upo serious nitaftie kwenye Hizi Namba siku ya jumatatu majira ya Saa mbili usiku 0618474341
 
Back
Top Bottom