kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Awali:
Kabla ya yote napenda kuanza kwa kusema kuwa albino ni binadamu sawa na binadamu wengine waliozaliwa na hitilafu za kiafya za kurithi kutoka kwa wazazi wao kama vile hitilafu/ulemavu macho makengeza, kisukari, kansa, kifafa (epilepsy), ugonjwa wa akili (schizophrenia) fibroid, sickle cell, ukosefu wa viungo mwilini, shinikizo la damu, damu kuchelewa kuganga (hemophilia), makundi ya damu (blood groups), kuzaa mimba za mapacha, n.k. Haya ni mambo ambayo mtoto anaweza kuyarithi kutoka kwa wazazi na kizazi chake cha pande zote za baba na mama yake.
Ikumbukwe kuwa mtu anaweza kurithi tabia, umbo na hitilafu za kiafya kutoka hadi kizazi chake cha tano cha ukoo wake (yaani wazazi, mababu, mabibi............. hadi kizazi chake cha 5 nyuma kiumeni na kikeni).
Hivyo basi asilimia 99% ya ma-albino wamepata ualbino huo kutokana na kurithi tabia (traits) kutoka kwa wazazi wao na ndugu zao wa nyuma sana ambao hata wao inawezekana hawawafahamu wala kuwasikia habari zao.
Hivyo ni makosa kudhani kuwa albino ni kiumbe tofauti na walemavu wengine duniani, kama watu wengine walivyolemaa viungo vingine wao albino wamelemea ngozi yao.
Albino amekosa nini hadi awe mweupe?
Albino amekosa vinasaba (genes) vinavyobeba taarifa ya kutengeneza rangi (nyeusi) ya ngozi, macho na nywele inayojulikana kama Melanin. Vinasaba hivi vinaweza kuharibiwa kwa urahisi na vitu kama kufanyakazi au kukaa kwenye jua kali, joto kali, mionzi mingi ya X-ray, kula vyakula vyenye sumu, n.k. Wazee wetu wa zamani walikuwa wakifanyakazi ngumu na kutembea juani machanakutwa hivyo kupata uwezekano wa kuharibu miili yao kwa mionzi ya hua na joto kunakoweza kusababisha hitilafu kwenye DNA zao zinazobeba vinasaba vya urathi. Wazee wetu inawezekana pia katika harakat za maisha yao huko nyuma walikula au kukosa vyakula na madini yanayoharibu miili yao na kusababisha uharibifu/upungufu katika miili yao. Hata leo hii wapo watu "wajinga" ambao wanajichubua (kujikoboa) ngozi zao kwa kuiondoa hii rangi nyeusi kwenye miili yao kwakutumia madawa (chemicals) ili wawe weupe (albino). Hawa wanafanya kosa la kujitengenezea ualbino kwa makusudi. Hivyo albino sio shetani, malaika wala mwenye kitu tofauti na mtu mwingine zaidi ya kukosa tu rangi nyeusi kwenye ngozi, macho na nywele zake.
Rangi ya ngozi (Melanin) ina kazi gani mwilini?
Kazi kubwa ya rangi hii ya ngozi (melanin) ni kupunguza kiwango cha mionzi mibaya (radiations) kutoka kwenye jua isipenye na kuingia kwa wingi mwilini. Kama mionzi hii itaingia kwa wingi mwilini inasababisha kansa ya ngozi na madhara mengine kwenye chembehai za mwili, macho na damu. Hivyo basi, adui mkumbwa namba moja wa Albino ni jua. Mlemavu wa ngozi pia ana matatizo ya kuona vizuri (uoni hafifu).
Namna ya kuzuia kuzaa mtoto albino
Matunzo ya mtoto albino yamejaa changamoto nyingi sana na ni ghali sana. Hata hivyo huwa ni vigumu sana mtu kuzuia kuzaa mtoto albino kwa 100% kwakuwa huna taarifa za ukoo wako wote tangu huko nyuma, lakini mambo yafuatayo yanasaidia kupunguza uwezekano wa kuzaa albino:
1. Anza kwa Chunguza ukoo wako kwanza ili kufahamu kama kuna mtu (baba, mama, babu, bibi, kaka, dada) au historia ya watu wenye au waliowahi kuwa au kuzaa watoto albino.
2. Usioe: Kama wewe mwenyewe, mzazi/wazazi, babu, bibi, shangazi, mama mdogo, kaka, dada wako wako ualbino basi wewe usioe wala kuzaa na mwanaume/mwanamke albino, mwenye wazazi au ndugu wenye uaalbino (kaka, dada, babu, bibi, changazi, baba mdogo, mjomba, au mama mdogo), inaweza kusababisha uzae watoto au uwe na wajukuu maalbino. Kanuni hii inaweza kutumika pia katika kuepuka kuzaa watoto na wajukuu wenye hitilafu nyingine za kurithi kama vile pumu, kisukari, sickle cell, makengeza, kifafa, ugonjwa wa akili, mimba za mapacha n.k.
3. Usifanye kazi kwenye jua kali sana la mchana kama vile kuchunga, kulima, kutengeneza barabara, n.k bila kujikinga kwa mwamvuli, kuvaa kofia pana na overall (ovaroli)
4. Usioge wala kuogelea kwenye maji (bahari, ziwa, mto, bwawa) wakati wa jua kali la kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 mchana ili kuepuka kupata miozi mingi ya jua
5. Usipende kunyoa upara na kutembea kwenye jua kali
6. Usitembee kwenye jua kali ukiwa umevaa singileti tu au kifua wazi
7. Epuka miozi ya x-rays kila mara, hasa sehemu za siri
8. Usikae karibu na madini/vifaa yanayotoa mionzi kama vile Uranium
9. Epuka kufanyakazi sehemu zenye joto jingi kama vile kiwandani, migodini, kuyeyusha vyuma/uhunzi, kuendesha magari makubwa/malori ya safari ndefu sana kila siku.
Namna ya kumsaidia mtu mwenye albino
1. Aepuke jua kali kuchoma ngozi yake moja kwa moja
2. Vaa kofia pana
3. Vaa miwani ya jua (sunglass)
4. Vaa nguo za mikono mirefu
5. Paka mafuta maalumu ya ngozi (sun screen) yenye viwango vinavyokubalika kwa kuzuia mionzi isipenye
6. Asioge wala kuogelea juani
7. Darasani akae dawati la mbele/ubaoni
8. Darasani mweke albino karibu na mtoto wa kawaida ili apate usaidizi wa kusomewa.
Hitimisho:
1. Albino sio kiumbe cha ajabu ni binadamu kama wengine
2. Albino tayari anakabiliwa na changamoto nyingi hasa za jua, tusiwaongezee changamoto mpya
3. Albino wanazaliwa na watu wa makabila yote, nchi zote na mabara yote duniani, sio tanzania tu.