Jinsi zao la alizeti linaweza kupunguza uhaba wa mafuta ya kupikia

Jinsi zao la alizeti linaweza kupunguza uhaba wa mafuta ya kupikia

Vindaniel

New Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
3
Reaction score
1
UTANGULIZI
Sekta ya kilimo inachangia zaidi ya 40% ya pato la taifa. Ili taifa loloteliweze kukua vizuri kiuchumi lazima liwe na mikakati dhabiti na endelevu juu ya kilimo bora na chenye tija kwa taifa na kwa wananchi wake

Kilimo za alizeti
Zao la alizeti ni zao la kibiashara linalolimwa kwa wingi baadhi ya mikao hapa Tanzania.
Baadhi ya mikoa inayolima alizeti ni Singida,Manyara,Dodoma,Simiyu

Kipaombele
Serikali na wadau mbali mbali wa kilimo wanapaswa kuona ya kwamba kilimo cha alizeti kiwa ajenda kwa Taifa kwa mikao inayozalisha kwa wingi zao hilo ili kuja kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa mafuta ya kupikia ndani ya nchi
Kuokoa gharama za uagizaji wa mafuta ya kupikia nje ya nchi.

Mfuko wa pembejeo za kilimo
Katika kazalisha kwa wingi alizeti wadau wa kilimo na serikali kwa kuungana na mfuko wa pembejeo za kilimo waweze kuungana kwa pamoja kuwapatia wakulima pembejeo bora za kilimo zinazoendana na wakati ili kuweza kukuza uzalishaji kwa wakulima .
Kuwakopesha wakulima au kuwauzia pembejeo kwa bei inayoendana na hali zao za kiuchumi
Kama wataamua kumkopesha mkulima pembejeo ili mkulima aweze kulima kilimo chenye tija na mwisho wa msimu mkulima aje arejeshe asilimia fulani kwenye mazao yake.
Hitimisho
Kama serikali na wadau wa kilimo wataamua zao la alizeti kuwa ajenda kwa mikao inayo zalisha hilo zao hapa nchini tutaweza kupunguza kwa kiasi fulani uhaba wa mafuta ya kupikia
Hatuna budi kuchagua mikao michache kwa ajili ya kulima alizeti kwa wingi.
 
... sio tu kupunguza uhaba wa mafuta ya kupikia bali nchi hii inatakiwa iwe exporter wa edible oil. Hela zinazopelekwa kwenye mamiradi yasiyo na tija zingeelekezwa huku tungeweza ku-export many agricultural produces endapo fedha hizo hazitaishia kununulia V8's za mabosi kama ilivyofanyika kwenye ule ujinga ulioitwa Kilimo Kwanza.
 
Back
Top Bottom