Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Na Paul R.K Mashauri
Kama wewe ni mfuatiliaji wa takwimu mbalimbali, utagundua kwamba, utafiti ndani na nje ya Tanzania unaonesha kwamba idadi ya ndoa zinazovunjika kila siku inazidi kuongezeka na sehemu kubwa ya wanaodai talaka ni wanawake.
Utafiti pia unaonyesha, sababu inayoongoza kwa kuvunjika kwa ndoa katika zama hizi sio masuala ya mapenzi au udanganyifu bali ni masuala ya pesa. Na utafiti unaonyesha wanawake wengi hufanya maamuzi ya talaka na kujipanga muda mrefu kabla hawajaondoka.
Hapohapo utafiti mdogo uliowahi kufanyika kupitia DNA ulionyesha kuwa idadi ya watoto ambao sio wa baba aliye katika ndoa ni ya kiwango cha kustaajabisha! Hii ina maanisha kuwa kuna ongezeko kubwa sana la udanganyifu unaofanywa na wanawake dhidi ya wanaume katika ndoa!
Lakini hii haihitaji maneno mengi ikiwa utarejea tukio la mwanaume mmoja nchini Guinea aitwae Bartazari ambaye alivuma katika mitandao ya kijamii kwa kutembea na wanawake 400 wengi wakiwa ni wake wa watu wenye uwezo wa kiuchumi na mamlaka pasipo waume zao kujua.
Utafiti pia unaonyesha kwamba wanaoathirika zaidi kwa matatizo yatokanayo na talaka na kuvunjika kwa ndoa kisaikolojia, kiuchumi na hata kijamii ni wanaume. Wengi hupoteza "castody" ya watoto, mali na afya ya akili. Zaidi ya hapo hugeuka nyenzo ya kutoa fedha tu kwa watoto huku wakinyimwa nafasi ya kuwa karibu na hao watoto!
Utafiti pia unaonyesha katika jamii nyingi, wanaume ndio wanawekeza zaidi kiuchumi katika ndoa kutokana na mila na desturi. Mfano michakato ya urafiki, uchumba, mahari, harusi, ndoa zinazoambatana na kuhudumia familia, mke na watoto kwa sehemu kubwa ni wanaume. Lakini maamuzi mengi ya kusitisha ndoa hizohizo zenye uwekezaji mkubwa hutoka kwa wanawake.
Zaidi ya hapo utafiti unaonyesha kwamba sheria kanuni na taratibu nyingi hazimlindi mwanaume katika urafiki, uchumba na ndoa na hii ni kwa sababu wanawake ni moja ya makundi maalum kulindwa kisheria kwa sababu za kihistoria. Hivyo idadi kubwa ya wanaume wanapopitia changamoto, hawana mifumo ya kuwatetea wala kuwainua. Wengi huishia katika "substance abuse" yaani ulevi wa madawa ya kulevya, pombe, mihadarati nk.
Utafiti pia unaonyesha kadri siku zinavyozidi kwenda, ndipo mifumo ya kijamii na kiuchumi inazidi kumtoa mwanaume nje ya wigo wa elimu "formal and informal", uchumi na ndoa kwa mizani dhaifu ya uwezeshaji iliyoegemea kwa mtoto wa kike. Maana yake ni kwamba kama hali itaendelea hivi, tutakuwa na baba wengi wasio na uwezo wa kutimiza majukumu yao, ya kifamilia na kijamii.
Mbaya zaidi tafiti zinaonyesha kwamba mwelekeo wa tamaduni hasa za nchi za magharibi zinajikita katika kuwapa uwezo wanawake kuishi pasipo ulazima wa mwanamke kwa mpango wa kuotesha mimba na ndoa za jinsia moja "artificial insemination and same sex marriage". Hii imepunguza umuhimu wa mwanaume na familia, na mbali zaidi haki ya mtoto kuzaliwa katika mfumo asilia unaompa fursa ya kuwa na kumjua baba.
Mbaya kuliko yote tamaduni hizi kupitia sheria na kazi za Sanaa zinachochea hamasa kwa watoto wa kiume kubadilishwa au kujibadilisha kuwa jinsia ya kike "transgender", kucheza michezo ya kike na hata kuwa wake wa wanaume katika ndoa za jinsia moja "gay marriage". Pamoja na jitihada za Rais mpya wa Marekani Donald Trump kumaliza hili tatizo, bado kuna msukumo mkali wa jambo hili kutoka kwa viongozi wa dini mbalimbali na wanaharakati wa haki za binadamu.
Haya yote yanatokea kwa kasi kubwa katika nyanza za kiserikali, taasisi za dini, mifumo ya kiuchimi, harakati za kifeminia, Sanaa za muziki na filamu hasa "Hollywood" asasi za kiraia na ufadhili wa NGOs. Kwa tafsiri nyepesi jinsia ya kiume iko katika hatari kubwa katika dunia ambayo imeendelea sana kiteknolojia kiasi cha kutafuta mbadala wa jinsia ya kiume katika eneo la familia.
Hapa ni pamoja na baba zetu, kaka zetu na kubwa zaidi watoto wa kiume. Na ukifikiria kwa kina utagundua dhana nzima ni kuiaminisha dunia kwamba familia ni kama haitakiwi na umuhimu wake ni wa kinadharia zaidi na kutengenezwa tu na imani za dini ingawa imepitwa na wakati na sio "relevant" katika zama za karne ya 21. Kwa elimu yangu ya sayansi ya jamii "sociology" na uchumi "economics", bado naamini kwamba taasisi ya kwanza ya kijamii yaani familia ni muhimu sana ingawa iko mbioni kusambaratika.
Kwa mfano, asilimia kubwa ya biashara zote duniani ni biashara za kifamilia ambazo ni 80% ya biashara zote duniani. Asilimia kubwa ya tabia, mienendo, changamoto na mafanikio ya watu wote duniani yanategemea sana malezi na mchango wa familia. Idadi kubwa ya watoto wa mitaani inatokana na changamoto za familia. Mtumiaji mkubwa wa bidhaa za kila siku kuanzia chakula mpaka afya, elimu nk ni familia. Na tafiti zinaonyesha kwamba wengi walio nje ya familia wanapitia changamoto za kiuchumi, afya, upatikanaji wa elimu "formal and informal" nk.
Baadhi ya nchi kama Kenya na Marekani zimeanza kubadili misimamo yao juu ya hatma ya jinsia ya kiume na familia katika nchi zao kwa kufanya mabadiliko ya sera na sheria katika maeneo ya jinsia zinazotambulika kisheria, masuala ya mali na talaka nk. Mfano masuala ya mgawanyo wa mali baada ya ndoa kuvunjika yalifanyiwa marekebisho nchini Kenya ili kila mwnandoa kupata stahiki anayostahili baada ya ndoa kuvunjika.
Zipo tetesi pia kwamba Rais Donald Trump anao mpango wa kuangalia upya eneo hilo. Lakini bado changamoto ni kubwa zinazohitaji mjadala wa kijamii, kitaifa na kidunia. Hii haimaanishi kwamba jinsia ya kike haina changamoto. Inazo nyingi sana na tafiti zinaonyesha kwamba bado ukatili wa kijinsia ni mkubwa kwa wanawake hasa katika jamii za nchi kusini mwa jangwa la Sahara "Sub Saharan Africa".
Zaidi ya hapo utafiti unaonyesha mila na desturi nyingi hasa Afrika bado haziwapi wanawake umiliki wa rasilimali hasa ardhi. Nilishuhudia hilo nilipoenda kikazi mkoani Mtwara ambako kuna mradi wa UN Women kwa kushirikana na halmashauri mbalimbali katika masuala ya rasilimali katika familia. Wapo wanawake wanaolima korosho lakini wakati wa mavuno, waume zao huchukua pesa zote kwenda kunywa pombe na kuoa wanawale wapya.
Na pia katika baadhi ya tamaduni mfano maeneo ya maziwa makuu hasa katika mkoa wa Mara na mikoa mingine, zipo mila kandamizi kama ukeketaji wanawake! kwa kiingereza "female genital mutilation" au "FGM". Naandika hayo kuonyesha bado changamoto za wanawake zipo lakini ipo mifumo inayozishugjulikia. Lakini kwa upande wa jinsia ya kiume, zipo changamoto nyingi sana lakini hakuna mifumo thabiti ya kuzishughulikia zaidi ya mifumo ya kuhoji uwajibikaji wao kiuchumi na katika ndoa angali wigo wao wa kufanikiwa kiuchumi unaondolewa katika mifumo kadhaa ikiwemo mifumo ya uwezeshaji "economic empowerment initiatives".
Hoja yangu ya msingi ni kwamba wanawake na wanaume ndio jamii na ndio familia ingawa mizani ya kushughulikia matatizo yao imeegemea zaidi upande mmoja wa jinsia ya kike na kufumbia macho jinsia ya kiume na madhara yake yako wazi.
Idadi ya wanaume wanaopitia changamoto za afya ya akili na kujinyonga au kuingia katika vitendo vya uhalifu ni kubwa kuliko idadi ya wanawake. Idadi ya wanawake wajane au "single mothers" ni kubwa kuliko miaka michache iliyopita.
Na idadi ya vijana wa kiume wasio na mifumo ya kuwawezesha kiuchumi na kuwapa stadi za maisha ni kubwa kuliko idadi ya mabinti wa kike. Na cha kutia hofu ni kwamba idadi ya watoto wa kiume wasiotaka kusikia suala la kuoa inashika kasi kuliko idadi ya mabinti wanaotaka kuolewa ambao ni wengi. Mimi kama baba wa watoto 2 wa kiume na watoto 2 wa kike, nahisi wazazi wenzangu wanaoguswa na hali hii duniani ni wengi hivyo suala la familia na mkanganyiko uliopo linahitaji kupewa kipaumbele. Na kwa kufanya hivyo sikukaa kimya na kulalamika. Nilichukua hatua. Mwaka jana nchini Marekani pale Seattle, Washington, mimi na wenzangu tulianzisha kampuni ya Family Plus International (www.fpiglobalinc.com) kufanya kazi hiyo. Kampuni ambayo iko mbioni kusajiliwa Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.
Tayari tuna programu nyingi za kusaidia "single mothers" na "single fathers" iitwayo "Bridges", watoto walioathirika na ndoa zilizovunjika "talaka" nk. Kupitia "digital platforms" zetu wanasheria na wataalam wa masuala ya kisaikolojia na fedha wanasaidia familia na watoto zinazopitia changamoto kupata msaada stahiki pamoja na "Scholarships". Pia wafanyakazi wa maofisini wanaopitia changamoto za kifamilia na hawawezi kutunza watoto wakati wakiwa kazini na hata watoto, wanawake na wanaume wenye ndoto ambao wanaanza upya maisha baada ya kila kitu kuanguka. Hapa tuna programu ya (Employee Assistance Program au EAP) wanayolipiwa na waajiri wao.
Kwa kutafuta masuluhisho ya hizi changamoto, tunayo programu ya mazungumzo kuhusu masuala ya familia iitwayo "FAM Talk". Hii tunafanya katika taasisi za umma na serikali, jumuiya mabalimbali kama wahamiaji "immigrants", mashuleni na vyuoni katika taasisi za dini nk. Pia FAM Talk kupitia mitandao ya kijamii. Kingine ni "CareConnect" ambapo ni mfumo wa kidigitali kuwaunganisha wazazi na huduma za matunzo kwa watoto na wazee yaani "child and aged care" Tunafanya yote haya kwa kushirikiana na wadau wa FPI Global kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na Mameya wa Majiji.
Lai yangu ni ushirikiano wako katika kurekebisha hii mizani na kuirudisha familia katika kusudi lake. Hakuna mshindi familia inaposambaratika. Zaidi ni kuua misingi ya jamii zetu na kupata Taifa la ajabu.
Ni kutengeneza shida na taabu kwa vizazi vijavyo. Wanawake ni mama na dada zetu na wakati huohuo wanaume ni baba na kaka zetu. Popote ulipo okoa vijana wa kiume, rekebisha mizani, wanaume na wanawake tunategemeana. Pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, bado asili ya mwanadamu haiwezi kubadilika. Na asili ya mwanadamu sio chaguo letu sisi, tulizaliwa tukajikuta tulishachaguliwa. Uwe unaamini Mungu au hauamini huu ni ukweli usiohitaji ushahidi.
Picha hii ni ya Pep Guardiola, Meneja mkongwe wa klabu ya Manchester City ambaye hivi karibuni amepoteza sehemu kubwa ya kiasi cha utajiri wake wa dolla za Kimarekani milioni 126 kutokana na mke wake kudai talaka kwa sababu mume wake anatumia muda mwingi katika kazi yake ya kufundisha soka kuliko kuwa na yeye mke wake. Wengine walioripotiwa kupitia changamoto hizo ni wengi sana akiwemo mchezaji wa zamani wa Brazil Kaka aliyeachwa kwa sababu mke wake hajapenda alivyo karibu na familia, alivyo karibu na yeye mke wake ma watoto wake na kwa jinsi asivyo na kashfa za udanganyifu katika ndoa. Pia yupo Roberto Carlos, mchezaji gwiji wa zamani wa Real Madril na timu ya Taifa ya Brazil, ambaye alijikuta akilala katika eneo la uwanja wa soka wa Real Madrid baada ya mke wake kuomba talaka.