Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Upo sahihi sana. Tatizo kubwa ni mfumo wetu wa elimu upo influenced zaidi na mabwana zetu waliotutawala yale yaliyo nje na mabwana zetu kama hayo ya wachina wengi hawafahamu.Kama ni mfuatiliaji mzuri wa historia hakuna asiyemjua Napoleon Bonaparte, kazaliwa 1769 akafariki 1821. Huyu jamaa alikuwa mwanasiasa na commander wa jeshi la Ufaransa, amepigana vita vikubwa na akashinda.
Huyu ndiye alileta mapinduzi makubwa katika organizations za kijeshi na mafunzo kwa ujumla, Falsafa zake hadi leo vyuo mbali mbali vya kijeshi wanajifunza.
Huyu jamaa alisema namnukuu "China is a sleeping giant, when she wakes she will shake the world" .
Kafa 1821, China inapata uhuru 1949, alichosema ndio hiki dunia inakiona sasa hivi, kweli kabisa.
Ndio maana nilimuambia huyu jamaa kuna watu wenye akili ambao wanaifahamu dunia, na wanajua ya mbeleni, kama huyo Napoleon, aliiona China mbali sana lakini walikuwa wamelala.
Imepita zaidi ya miaka 100 ndipo China inapata uhuru.
Bila juhudi binafsi za kufahamu historia ya dunia na mengi yalio nje ya mabwana zetu huwezi fahamu.
Mfano mfumo wetu wa elimu mpaka leo kwenye somo la historia haitambui kama wachina ndio jamii za mwanzo mwanzo kufika East Afrika na kufanya biashara na kuondoka lakini haya hayapo.
Ni mengi sana ya kuelimisha yapo nje ya mfumo wetu wa elimu kuliko yaliyopo ndani wanafunzi wanalishwa mengi makapi