LGE2024 Jionee tofauti kati ya Mikutano ya CCM na ya CHADEMA iliyofanyika eneo moja la Kariakoo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Mungu fundi sana!

Polisi wakiendelea kutumiwa vibaya na CCM ambao wanawanyonya na kuwafanya waishi maisha magumu leo wamezuia Mkutano wa Chadema uliopaswa kufanyika pale Kariakoo

Angalia picha hapa chini👇


Cha kufurahisha zaidi Polisi hawahawa wamekuwa wanawaruhusu CCM kufanya Mikutano eneo hilo hilo la Kariakoo bila kuwazuia, kuwakamata wala kuwabughudhi.

Picha za Mikutano ya CCM inayofanyika hapo Kariakoo bila kubughuziwa na Polisi hizi hapa👇


Kweli hatuna budi kuwaelewa Chadema wanavyosema No Reform No Election

Lord denning
Arusha
 
Ccm ndio yenye dola, wangojee chadema na wao washike dola
 
Huo wa CCM ulikuwa barabarani kama wa Heche? Huoni hadi watu wamekaa kwenye viti ? Hapo ni barabarani? Jukwaa liko barabarani hilo?
 
Heri kuhudhuria matanga kuliko misiba ya ccm
 
Na sababu ya cdm kupigwa na vyombo vya dola ni huo ukweli unaowaumiza ccm.
 
Kumbe ulikuwa wapi? Hata unaijua Kariakoo wewe??
Nionyeshe jukwaa la CHADEMA na viti watu waliwa wamekaa kwenye viti

Heche yuko kwenye gari na kipaza sauti barabarani hilo ndilo eneo la mkutano kwenye barabara?
 
Nyie wafuasi wa Lissu ni wapumbavu sana, hivi huo ujinga wenu ndio mlitaka muupeleke kariakoo kwenye eneo la kibiashara!!?
 
Wanatufikisha vizuri sana wanapotaka tufike Watanzania
Du! Sikujua kuwa wanawafikisha vizuri. Sijui wanawafikishaje. Je kweli mmefikishwa au kufikirishwa mmefikishwa huko mlikofikishwa hadi mnageuzwa machawa, kunguni, funza, na viroboto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…