ABTWAHILAKILIMALI
Member
- Jan 10, 2015
- 78
- 27
JIONGEZE
Ni kweli mazingira uliyokuzwa nilikuwa marufuku baba au mama akishaongea kitu alafu wewe nawe utoe mchango wako kwenye hilo jambo. Ukajikuta ukiambiwa safisha sebuleni wala huwezi kujiongeza ukasafisha na chumbani. Lakini sasa umeshakua mkubwa unaweza jiongeza usikubali hali ile iendelee mpaka leo. Usiwe kama wale madada wa nyumbani kwa sababu aliambiwa apike nyama na mchicha lakini akakosa mchicha anashindwa kujiongeza na kununua sukuma wiki.
Kwa sababu wewe taaluma yako ni udaktari basi wala hujiongezi kujua mambo ya biashara. Kwa sababu wewe taaluma yako ni kilimo wala hujisogezi ukajua mambo ya siasa ya nchi yako. Kwa sababu wewe unapenda kusoma vitabu vya mahusiano basi wala hujiongezi ukasoma vya sanaa. Kwa sababu wewe ni mwanamuziki hujiongezi ukasoma hata uchumi kidogo.
Kuna sehemu nyingi tunaonewa kwa sababu tulishindwa kujiongeza huko nyuma. Tunaabishwa sababu hatujui kujiongeza. Nilikuwa nawaza na kutafakari kidogo tu kuna biashara ngapi, bank ngapi, makanisa mangapi,misikiti mingapi, hospitali ngapi ambazo zipo Kenya ama Uganda au Rwanda basi tuseme Burundi ambazo waanzilishi wake ni watanzania au ni matawi ya watanzania. Ukipata jibu ligeuze swali hilo hilo je ni ngapi zipo Tanzania na zinamilikiwa na raia kutoka nchi hizo tajwa. Nimezitaja nchi hizo sababu tumepata Uhuru kabla ya wao. Na marais wa nchi zao wengine wamesoma hapa Tanzania . Nimegundua wenzetu wanapenda kujiongeza wanafundishwa kujiongeza wanawaza kujiongeza.
Zaidi ya miaka 30 iliyopita Uganda ilitaka kujiongeza na kuchukua sehemu ya Kagera iwe kwao yaani Uganda ujiongeza ukubwa. Wala haijapita miaka 5 Malawi walitaka kujiongeza upande wa ziwa Nyasa. Wanawaza kujiongeza najua tunatambua jinsi Kenya inavyojiongeza kwenye mlima Kilimanjaro na jinsi watalii wengi wanapitia Kenya kuuona mlima Kilimanjaro . Sisi hatujui kujiongeza hatufundishwi kujiongeza hatujifundishi kujiongeza na wala hutufundishi kujiongeza.
Nawashukuru wazazi wangu wamenifundisha kujiongeza. Nakumbuka wakati najianda kusoma A level wakaniuliza unapenda kusoma nini na wapi na kwanini. Sio kwamba waliniuliza sababu hawazijui shule au hawajui napenda nini la hasha ila kwa sababu walitaka nijifunze kujiongeza katika kuwaza na kufikiri sababu siku moja nitaishi mimi. Nakumbuka siku moja Mzee wangu ananiambia soma waza kuhusu maisha yako na uliza chochote kwangu na wala usiwaze kuhusu nyumba zangu au chochote. Unajua alisema hivyo sio kwamba hanipendi laa ila alitaka nijue kujiongeza nisiwe na akili tegemezi. Je kama wewe ni mzazi au nikiongozi je unawafundisha watu kujiongeza au ndio ulichosema ndio maneno ya mwisho lazima wafanye na wasipofanya unakimbilia kulaani.
Najua watu wengi wanaogopa kujiongeza kwa kuogopa kukosea. Wanaogopa kujiongeza kwa kuogopa kuaibika. Wanaogopa kujiongeza kwa kuogopa hasara. Wanaogopa kujiongeza kwa sababu wameridhika na maisha yao ya sasa.
Jiongeze thubutu jaribu fanya tena rudia ila katika mlengo wa kupatia na kufanikiwa kihalali.