Jioni Moja na Bibi Titi miaka ya 1980

Jioni Moja na Bibi Titi miaka ya 1980

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JIONI MOJA NA BI. TITI NYUMBANI KWAKE UPANGA MIAKA YA 1980

Nimewakuta watoto hawa leo asubuhi hapa Ikwiriri, Rufijib wanaitazama picha ya Bi. Titi nikawaomba tupige picha mimi na wao na Bi. Titi.

Watoto hawa wamenikumbusha siku moja jioni moja kiasancha miaka 30 iliyopita nilipokwenda nyumbani kwa Bi. Titi Upanga.

Miadi hii alikuwa kanipangia Bwana Ally Sykes na nilimuimba anipangie ili nimhoji Bi. Titi kuhusu historia yake na mchango wake katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hapa Upanga nilipomkuta Bi. Titi alivyokuwa alikuwa tofauti sana na Bi. Titi niliyemuona Temeke nyumbani kwake kabla miaka michache iliyopita.

Tulikwenda mimi na wenzangu Temeke kwa Bi. Titi kwenye harusi.

Siku ile pale Temeke Bi. Titi hakuwa kachangamka kama nilivyomuona pale nyumbani kwake Upanga.

Hii ilikuwa mara yangu ya pili kufika pale nyumbani kwa Bi. Titi Upanga.

Mara ya kwanza nilifika pale Upanga nyumbani kwake ni siku alipofanya Maulid kushukuru kurudishiwa nyumba yake hiyo iliyotaifishwa na serikali katika miaka ya 1970.

Nyumba yake hii alirudishiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Maulid yale yalihudhuriwa na watu.wengi wa kimjini na Tewa Said Tewa alikuwapo na mkewe Bi. Zainab bint Maulid.

Hawa watoto niliowakuta katikati ya mji wa Ikwirir kwenye bango la Bi. Titi lilinikumbusha Bi. Titi nilipokwenda nyumbani kwake mara kwa nia ya kufanya mazungumzo kuhusu maisha yake nikamkuta kakaa na wajukuu zake wakiwa na furaha kubwa.

Bi. Titi huku akicheka aliniambia, "Bwana Mohamed huna jipya wewe utakaloandika kuhusu mimi ambalo bado halijaandikwa na waandishi."

Lakini akaniambia kitu ambacho kwa hakika kwangu kilikuwa kipya sikupata kukisikia popote.

"Sikiliza Bwana Mohamed nenda Arusha kwa Ismail Bayumi kamuulize nini tulifanya Mombasa."

Huu ukawa ndiyo mwisho wa mazungunzo yetu nikawa nimebaki pale kumaliza soda yangu na yeye akawa amekaa chini na wajukuu zake wanaangalia senema ya "Cinderella."

Wajukuu zake wakawa wanacheka wanasema, "Cinderella," yeye anawaambia, "Huyo ni "Kisonoko."

Nilikwenda Arusha kwa Ismail Bayumi na yeye ndiye akanieleza nini Bi. Titi alifanya alipokwenda Mombasa kama mgeni wa TANU Club kwa minajili ya kufanya kampeni Waingereza wamtoe Jomo Kenyatta kifungoni.

Historia hii nikaiandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Picha ya kwanza ni bango likitangaza Tamasha la Bi. Titi, Ismail Bayumi na picha ya mwisho mwandishi akamkabidhi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Mohamed Omar Mchengerwa kitabu cha Abdul Sykes.

320604312_1221251951935152_6219411077128010799_n.jpg

319550096_515439843982439_597358520530514178_n.jpg

319830693_861899521727141_6757531299281705679_n.jpg
 
Kwahiyo nani tapeli kati ya wewe unayetumia id fake na yeye ambaye yuko real? Idiot
Tapeli wa historia ya nchi..anataka kupotosha na historia kwa mlengo wake wa kidini..hafai hata kidogo.

Analazimisha hadi wauzakahawa waingie kwenye historia ya tanganyika kisa ni wadini yake.

Siku zote historia huandikwa na washindi na historia ya tanganyika imekwisha andikwa..aache utapeli.

#MaendeleoHayanaChama
 
kwenye mitandao ya kijamii nchi hii ukizungumza ukwel au uzuri wa waislam au uislam katika kuijenga nchi yao hii basi utaambiwa mdini na utatukandwa.kwani waislam wao hawastahili au sio raia wa nchi hii jamani.tuwe wenye kuvumiliana katika jamii zetu...
 
kwenye mitandao ya kijamii nchi hii ukizungumza ukwel au uzuri wa waislam au uislam katika kuijenga nchi yao hii basi utaambiwa mdini na utatukandwa.kwani waislam wao hawastahili au sio raia wa nchi hii jamani.tuwe wenye kuvumiliana katika jamii zetu...
Kabisa
 
Back
Top Bottom