Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Hodi JF!

Naomba kutanguliza Salaam kwa wana JF wote. Mimi ni mwanachama mpya wa jukwaa hili maarufu. Naomba kuuliza swali, hivi katika kitabu hiki cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alimtaja mwanasiasa fulani aliyejiuzulu baadae kwa kashfa kuwa hafai kuwa kiongozi? Kama ni kweli, ni mwanasiasa gani huyu na Nyerere alimtaja wapi kwenye kitabu chake? Naomba kuwasilisha.

Fareed
 
subiri toleo linalokuja la kijitabu hiki..
 
Jamani mimi natafuta ''copy'' ya Azimio la Arusha. Mwalimu alisema kwamba haoni pabovu kwenye Azimia, nami nina msukumo wa ndani kabisa wa nafsi yangu unaoniambia hivyo hivyo. Ningeopenda kusoma mwanzo hadi mwisho, ni nini kiliandikwa kwenye Azimio la Arusha.
 
Wasiliana na Mwanakijiji, atakutumia kopi.
 
Nashukuru sana na ninampongeza mwanakijiji kwa kutuwezesha kupata nakala ya kitabu hiki. Nimekuwa nikikitafuta kwa muda mrefu sana. UDUMU MWANAKIJIJI
 
Ni mambo ya kukatisha tamaa haya!!! lakini kuna siku yatawatokea puani!
 
Masaki,

Unaweza pia kusoma Azimio la Arusha hapa Jamii Forums. Nimeliona hivi karibuni ukurasa 81 wa "Nyerere: The Man, The Myth and The Legend."
 
Asante saana Mlenge kwani hicho kitabu nimekuwa nikikitafuta saana. Itabidi sasa nikisome kwa utulivu ili niweze kujua hatima ya nchi yetu kama ilivyotaabiliwa na mwasisi wetu Kambarage. Asante saana!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nimekion kitabu chenye ukombozi wa fikra juu ya kiongozi bora. Thank u kwa kukiweka humu ........
 
Daah...sikuwahi visoma wala kuviona..nimeshawishika...

MwanaKijiji niweke kwenye loop....

Natanguliza shukrani ...
 
Hivi Watanzania mnalalamikia nini kuhusu elimu? Mnapopata elimu, mnaendelea kusoma manifesto ya ki-komunisti kama Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere . Mnafikiri vijarida kama hivi vitawafikisha wapi?
 
Zakumi,
Hata manifesto za kikomunisti ni elimu. Karl Max hakuwa mbumbumbu. Soma aliyoyasema Nyerere na ainisha na yanayotokea Tanzania halafu useme ni kupoteza muda bure. Where is Companero when you need him?:-
 
Jasusi:

Yanayotokea sasa ni mapungufu ya siasa za Nyerere. Kawasomesha wakina Kikwete, Lowassa na akawajaza siasa. Matokeo yake dunia imebadilika, nchi imebakia na watu ambao hawana exposure yoyote au experience ya kazi. Na matokeo yake wanang'aninia siasa kuwa profession.

Kuhusu Karl Marx huwezi kufananisha na hivi vijarida uchwara.
 
Ningekubaliana na wewe kama akina Kikwete na Lowasa wangekuwa wanajaribu angalau kufuata sera za Nyerere. Hawa walikuwepo kuwepo tu wakati wa Mwalimu wakisubiri aondoke wapate nafasi ya kufanya vitu vyao. Ingekuwa kweli wanafuata sera za Nyerere wangegawa migodi yetu kwa wazungu at nothing? No way. Hawa ni opportunists ambao walikuwa wanasubiri muda muafaka waonyeshe makucha yao na tumeyaona. Mimi pia nimesomeshwa na Nyerere, mbona siko bogus hivyo? Think about that.
 
Mkuu Jasusi:

Kwikwikwi wewe na wenzio mliosomeshwa na Nyerere lakini sio bogus hamna political repertoire. Enzi za mwalimu ulikuwa unazunguka naye kuandika matukio mbalimbali duniani wakati mwenzako JK anakimbiza mwenge.

Sasa wakimbiza mwenge wameshika nchi unaanza kulalamika.
 
Back
Top Bottom