Hodi JF!
Naomba kutanguliza Salaam kwa wana JF wote. Mimi ni mwanachama mpya wa jukwaa hili maarufu. Naomba kuuliza swali, hivi katika kitabu hiki cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alimtaja mwanasiasa fulani aliyejiuzulu baadae kwa kashfa kuwa hafai kuwa kiongozi? Kama ni kweli, ni mwanasiasa gani huyu na Nyerere alimtaja wapi kwenye kitabu chake? Naomba kuwasilisha.
Fareed
Jamani mimi natafuta ''copy'' ya Azimio la Arusha. Mwalimu alisema kwamba haoni pabovu kwenye Azimia, nami nina msukumo wa ndani kabisa wa nafsi yangu unaoniambia hivyo hivyo. Ningeopenda kusoma mwanzo hadi mwisho, ni nini kiliandikwa kwenye Azimio la Arusha.
Jamani huyu jamaa ana kiingelesa kigumu!"res ipsa loquitor"
subiri toleo linalokuja la kijitabu hiki..
Zakumi,
Hata manifesto za kikomunisti ni elimu. Karl Max hakuwa mbumbumbu. Soma aliyoyasema Nyerere na ainisha na yanayotokea Tanzania halafu useme ni kupoteza muda bure. Where is Companero when you need him?:-
Ningekubaliana na wewe kama akina Kikwete na Lowasa wangekuwa wanajaribu angalau kufuata sera za Nyerere. Hawa walikuwepo kuwepo tu wakati wa Mwalimu wakisubiri aondoke wapate nafasi ya kufanya vitu vyao. Ingekuwa kweli wanafuata sera za Nyerere wangegawa migodi yetu kwa wazungu at nothing? No way. Hawa ni opportunists ambao walikuwa wanasubiri muda muafaka waonyeshe makucha yao na tumeyaona. Mimi pia nimesomeshwa na Nyerere, mbona siko bogus hivyo? Think about that.Jasusi:
Yanayotokea sasa ni mapungufu ya siasa za Nyerere. Kawasomesha wakina Kikwete, Lowassa na akawajaza siasa. Matokeo yake dunia imebadilika, nchi imebakia na watu ambao hawana exposure yoyote au experience ya kazi. Na matokeo yake wanang'aninia siasa kuwa profession.
Kuhusu Karl Marx huwezi kufananisha na hivi vijarida uchwara.
Ningekubaliana na wewe kama akina Kikwete na Lowasa wangekuwa wanajaribu angalau kufuata sera za Nyerere. Hawa walikuwepo kuwepo tu wakati wa Mwalimu wakisubiri aondoke wapate nafasi ya kufanya vitu vyao. Ingekuwa kweli wanafuata sera za Nyerere wangegawa migodi yetu kwa wazungu at nothing? No way. Hawa ni opportunists ambao walikuwa wanasubiri muda muafaka waonyeshe makucha yao na tumeyaona. Mimi pia nimesomeshwa na Nyerere, mbona siko bogus hivyo? Think about that.