Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
Hii sawa, lakini nafikiri, zaidi kwa Mzee wa watu Mtei, ama?Kweli mkuu. Ni jazba tu maana kila kona nakutana na hizi hisia. Sasa huwa inaniuma napokutana nazo kwa wazee wetu ambao wanapaswa kutuonesha njia vijana tunaopumbazwa na vyombo vya habari. Nahisi hii iliniuma zaidi maana ndio kwanza nimetoka kukisoma kitabu cha Mzee wetu. Samahani kwa kuumiza hisia zenu.
FMES,
..unless kuna kitu ambacho sikifahamu, lakini kwa uelewa wangu Wabunge wale walikuwa wanatumia haki yao ya kikatiba ndani ya Bunge la Jamhuri.
..kuhusu Njelu Kasaka kupewa Unaibu Waziri labda ilikuwa ni njia ya kumnyamazisha. wengine kama Sebastian Rukiza Kinyondo[r.i.p] alipewa wadhifa wa ukuu wa mkoa.
..nimeelekeza kwamba hawa G-55 walikuwa wamekerwa zaidi ya rushwa iliyokuwa inafanywa na Mwinyi na kundi lake. kwenye hoja yao walikuwa mpaka na malalamiko kwamba wa-Zenj wanateuliwa kushika nafasi zisizo za muungano. kuwapa G-55 madaraka ilikuwa ni njia ya kuwaingiza ktk kundi la wenye ulaji.
NB:
..binafsi ningependa sana kusoma hoja ya Tanganyika kama ilivyowasilishwa na Njelu Kasaka, na zaidi kupata hansard na kumbukumbu za mjadala huo bungeni.
Jamani, PM Malecela alikuwa nacheza strategy nzuri sana ya "" no blood in my hands"" na kwa kweli angeshinda kama sio Mwalimu kuona mchezo mzima. Huwezi kushindwa kuitetea Serikali bungeni ukabaki PM, no way. Huwezi kwenda kinyume na CCM, halafu bado ubaki kiongozi wa serikali ya CCM.
So JKN was right.
Mabavu ya kumleta Mkapa hiyo ni topic nyingine, na vile vile kutuletea Mwinyi wakati alikuwa hana uwezo hiyo nayo ni topic nyingine.
..Mwalimu,Mwinyi,na Malecela, wote kwa pamoja walijaribu kuwashawishi bila mafanikio Wabunge 55 waondoe hoja yao.
..ukisoma kitabu kwa undani utaona kwamba, baada ya kushindwa kutumia ushawishi, Mwalimu alitaka litumike rungu la nidhamu ya chama; kwamba, watu waanze kufukuzana ktk chama na baraza la mawaziri.
..tatizo lilolokuwepo wakati ule ni rushwa iliyokuwa ikiendekezwa na Raisi Mwinyi, pamoja na mtizamo kwamba alikuwa akiwatenga Watanganyika na kuwapendelea Wazanzibari ktk ardhi ya Watanganyika.
..kwa mtizamo wangu hicho hapo juu ndicho kilikuwa chanzo cha hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. kwa bahati mbaya, naona Mwalimu alikuwa anaona aibu kulishughulikia tatizo hilo na badala yake akaamua kuwatoa kafara Malecela na Kolimba[r.i.p].
NB:
..FMES, amedokeza kwamba baada ya Malecela kuondolewa ktk nafasi yake, Raisi Mwinyi alimteua Njelu Kasaka, mbunge aliyeongoza wabunge 55 kuwasilisha hoja ya Tanganyika, kuwa naibu waziri wa kilimo. vilevile wabunge wengine waliounga mkono hoja ya Tanganyika, mfano Sebastian Kinyondo, walipewa nyadhifa za ukuu wa mkoa. Mwalimu hakupinga teuzi hizo, kitu ambacho naona kinaleta contradictions.
..Philip Marmo,Mateo Quares,Jenerali Ulimwengu,...walikuwa vinara wa hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. kama hao hawaandamwi, sioni uhalali wa Cygwiyemwisi Malecela kuandamwa kwasababu tu alishindwa kuwapinga/kuwavuruga bungeni.
..
FMES,
Sema tu ndugu yangu mbona wengine tunajua? Lakini la ajabu ni kwamba watu kama Mwinyi wameshindwa hata kuandika chochote kuhusu chochote wakati wa utawala wao. Angalau hata Jumbe alijitahidi kuandika Ze Patnaship. Lakini sijaona popote pale ambapo hoja za Mwalimu zimejibiwa kwa hoja.Hoja mojawapo ya Mwalimu ni kwamba kungeundwa serikali tatu ungekuwa ndio mwisho wa muungano. Ningependa kusikia hoja mbadala inayotetea kuwepo kwa serikali tatu na kuimarishwa kwa mwungano.
-
....lakini kwa makusudi mazima akaamuwa ku-waste his energy his intellectualism na kitabu ambacho hakigusi kabisa matatizo ya wananchi wa kawaida wa Tanzania...
kitabu ukweli ni kwamba hakiwezi kusimama maana the whole book is a fraud kwa sababu kinasimama kwenye unclean ground
Mungu Aibariki Tanzania.
Respect.
FMEs!
- Mkuu Joka, Mwalimu angekua serious angemshauri Malecela kuwafanya hawa G55 kama yeye aliivyowafanya kina Seif Bakari na wenzake, yaani kuwaweka under house arrest hawa wahaini, unafikiri ni kwa nini hakufanya hivyo?
- Tizama baada ya Malecela kuhama ndani ya nyumba ya Waziri Mkuu kutokana na hiki kitabu, Kasaka walipewa uwaziri wengine u-RC, lakini waulize wanaojua ile nyumba ya Waziri Mkuu aliyotoka Malecela alihamia nani? Hapo ndipo utashangaaa sana mkuu maana ni aibu hata kusema jina la aliyehamia! Nisemeeeeee?
Respect.
FMEs!
mkuu, nimekisoma kwa haraka sana,
lakini mbona kina Typo nyingi sana? ndo chenyewe au draft?
- - I mean hivi vitabu kuna siku vitajibiwa tu, one ni ujinga wa hali ya juu sana kuvijibu sasa hivi, ni lazima kusubiri wananchi waamke kwanza, in 20 years from now wananchi watakwua wameamka sana kisiasa ndio utakwua wakati mzuri sana wa kujibu hivi vitabu hasa hiki kitabu.
FMEs!
Wote tuajua alihamia Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Lakini hatuwezi kusema alihamia kwani Waziri mkuu baada ya kuenguliwa Malecela alikuwa Cleopa Msuya.
Ni Msuya kwa mapenzi yake alimpisha Mwalimu aishi kwenye nyumba ile kwa muda maana nyumba yake ya Msasani ilikuwa matengenezoni kipindi hicho ambacho kiliisha baada ya matengenezo kuisha na Mwalimu kurudi Msasani.
Mkuu ES, mimi najadili zaidi nafasi ya PM kuliko mtu aliyekuwa PM. Sasa hapa makosa aliyofanya PM ambayo kwa ukweli sio makosa maana alikuwa anajua exactly alichokuwa anataka na kuamua kupindisha mambo ili tu apewe support ya kuwa president, ndio ambayo sikubaliani nayo.
Sasa itakuwa vizuri tusijali sana mambo aliyofanya mwalimu na makosa yake, na kujiuliza
1) Kweli PM aliyoyafanya kushindwa kuilinda serikali bungeni ni sahihi??
2) Kumshauri President mambo mawili tofauti kabisa in less than 72 hrs na kubaki na kazi ni sahihi??
3) Kumpeleka rais bungeni kukemea serikali ya Tanganyika kuanzishwa, and then wakati rais bado anamsimamo huu PM anakubali msimamo wa wabunge wachache, hii ni sawa??
Hapa issue ilikuwa kubwa mno sababu ilikuwa inaweka nafasi ya urais hatarini na vile vile constitutional crisis btn bunge na serikali.
Mwinyi was a disaster no question, lakini PM hapa lazima akubali lawama sababu alicheza mchezo ambao kama ungefanikiwa sijui leo issue ya nchi yetu tungekuwa wapi.
disclaimer:: Muungano kwangu mimi sio issue kubwa na siku zote wala sipingi wazanzibar wakiamua kujitenga
Haviwezi kujibiwa sasa hivi kwa sababu wapo wengi tu waliokuwepo, walioshuhudia na hawatakuwa tayari kumruhusu limbukeni yeyote ajaribu kuipindisha historia. Toeni hayo majibu kama kweli yanaweza kukubalika kwani ukweli hauna tabia ya kujificha - mficha ficha maradhi, kilio humuumbua.
- Anayeumbuliwa na kilio anajulikana sana mkuu, huwezi kupanda mahindi ukavuna mihogo, sasa hivi Tanzania tunavuna mbegu za uongozi mbovu zilizopandwa na nani mkuu? Bwa! ha! ha! nyumba ni foundation mkuu sasa jiulize foundation ya uongozi mbovu iliwekwa na nani?
Nakuhakikishia kuwa hata baada ya miaka 20 watu watakuwa bado wanamkumbuka Mwalimu. Kama unadai aliendelea kutawala hata baada ya kung'atuka nafasi zake zote kwenye chama na serikali, hiyo peke yake yaonyesha alikuwa na uwezo wa kipekee. Na kama bado mzimu wake unaendelea kuwatesa hata baada ya kifo chake miaka zaidi ya kumi iliyopita, basi na uendelee kuwatafuna. Wengine tunasubiri hicho kitabu kwa hamu, bring it on.
- Miaka 20 kutoka sasa taifa litakwua na wananchi objective sio bendera bendera kama sasa, historia huandikwa wakati wowote kinachojali ni facts, Mwalimu kuendelea kutawala baada ya kuacha ni dalili za kupenda power kitu anachowalaumu wengine ndio unaitwa unafiki huo,
- Mwalimu hana mzimu unaomsumbua mtu, wewe unafikiri kina Lowassa wanasumbuliwa na mizimu wa anybody, hawa Kina Rostam wanasumbuliwa na mzimu wa anybody, Malecela ndio hivyo yupo huko US anaendelea na shuguli za ujenzi wa taifa, hakuna anayesumbuliwa tunachofanya hapa ni kuweka upande wa pili wa habari, lakini hamukuzoea kusikia upande wa pili kwa hiyo mnajaribu kama zile kawaida zenu kutumia nguvu, vitisho, na ukali pamoja na matusi, ila hatuogopi tutaendeelea kuweka tu upande wa pili wa shillingi na sio siri unawatesa maana mlikuwa likizo ya miezi sita mkakimbia sana kurudi Bwa! ha! ha!
- Nyumba ni foundation, ikiwa mbovu basi na nyumba nzima itakua mbovu, watawala wote waliowahi kututawala hili taifa hakuna mwenye nafuu wote walikuwa sawa tu ndio maana tumekwama, Mwalimu alikwua tofauti kidogo hakua na tamaa ya mali, lakini alikuwa na tamaa ya madaraka kuliko wengine wote!
FMEs!
...tatizo la Mwalimu lilikuwa Malecela asiwe Rais na ni kwa matatizo yao binafsi wala sio ya taifa, sasa kwa nini kulidanganya taifa zima kwamba tatizo letu ni Muungano?
Respect.
FMEs!
Waliwahi kuchangia mke?.
- Acha matusi, Malecela na Mwalimu wote walikuwa na wake sasa una maana mke wa nani aliyechangiwa kwa sababu si inaeleweka yupi ambaye siku zote alikua na tatizo mwenziwe, kama umeishiwa hoja tulia mkuu achia wengine walionazo.
Hivi aliyemteua Malecela kuwa waziri mkuu wa Tanzania ni nani?
- Alikuwa ni Rais Mwinyi, mwaka 1990.
Es!