..Mwalimu,Mwinyi,na Malecela, wote kwa pamoja walijaribu kuwashawishi bila mafanikio Wabunge 55 waondoe hoja yao.
..ukisoma kitabu kwa undani utaona kwamba, baada ya kushindwa kutumia ushawishi, Mwalimu alitaka litumike rungu la nidhamu ya chama; kwamba, watu waanze kufukuzana ktk chama na baraza la mawaziri.
..tatizo lilolokuwepo wakati ule ni rushwa iliyokuwa ikiendekezwa na Raisi Mwinyi, pamoja na mtizamo kwamba alikuwa akiwatenga Watanganyika na kuwapendelea Wazanzibari ktk ardhi ya Watanganyika.
..kwa mtizamo wangu hicho hapo juu ndicho kilikuwa chanzo cha hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. kwa bahati mbaya, naona Mwalimu alikuwa anaona aibu kulishughulikia tatizo hilo na badala yake akaamua kuwatoa kafara Malecela na Kolimba[r.i.p].
NB:
..FMES, amedokeza kwamba baada ya Malecela kuondolewa ktk nafasi yake, Raisi Mwinyi alimteua Njelu Kasaka, mbunge aliyeongoza wabunge 55 kuwasilisha hoja ya Tanganyika, kuwa naibu waziri wa kilimo. vilevile wabunge wengine waliounga mkono hoja ya Tanganyika, mfano Sebastian Kinyondo, walipewa nyadhifa za ukuu wa mkoa. Mwalimu hakupinga teuzi hizo, kitu ambacho naona kinaleta contradictions.
..Philip Marmo,Mateo Quares,Jenerali Ulimwengu,...walikuwa vinara wa hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. kama hao hawaandamwi, sioni uhalali wa Cygwiyemwisi Malecela kuandamwa kwasababu tu alishindwa kuwapinga/kuwavuruga bungeni.
..