- Mkuu mbona unalazimisha hoja, Mwinyi alimuondoa Warioba aliyechomekwa kwenye Umakamu wa Rais from nowhere na kumuweka Malecela, toka ile siku Mwinyi alipoteza amani yake ya uongozi maana alichokoza nyuki, na ndio kwa mara ya kwanza likazuka kundi lenye nguvu za ajabu sana yaani G55, ndugu yangu usiombe kujua yote yaliyotokea behind the scene toka ile siku maana ilikuwa balaa!
Es!
Mwinyi hakumuondoa Warioba kwenye uwaziri mkuu. Ni kweli kuwa Joseph Warioba aliupata uwaziri mkuu Novemba 1985 baada ya masaa kadhaa baada ya kumkabidhi Mwinyi katiba ya nchi.
Warioba aliendelea na uwaziri mkuu hadi mwishoni mwa 1990 na nchi nzima ikaingia kwenye uchaguzi. Hivyo Warioba alimaliza ngwe ya kwanza ya Rais Mwinyi na yeye akaenda kugombea ubunge jimbo la Bunda ambako yeye alipambana na Stephen Wasira wote kwa ticket ya CCM kwani bado ilikuwa ni kipindi cha chama kimoja.
Uchaguzi wa mwaka 1990 ulimalizika, Warioba akamshinda Wasira kwenye ubunge wa Bunda. Mwinyi akamchagua tena Warioba kuwa waziri mkuu. Hivyo kama ingeendelea vile basi Warioba angemaliza ngwe ya pili ya Mwinyi iliyoisha mwaka 1995.
Kilichotokea na wasichokikumbuka wengi ni kwamba mara baada ya uchaguzi wa mwaka 1990 na mara baada ya kuchaguliwa Warioba kwa mara ya pili kuwa waziri mkuu, Stephen Wasira akafungua kesi kulalamikia uchaguzi wa Bunda.
Sikumbuki vizuri mwenendo wa kesi lakini moja ya malalamiko yaliyokubaliwa hata na majaji ni kwamba iweje waziri mkuu aende kwenye kampeni akisindikizwa na msululu wa vimulimuli na mapikipiki. Je hii ni haki. Jaji mmoja aliuliza "hayo mapikipiki alikuwa anapelekewa nani" kwenye kampeni ya uchaguzi.
Hivyo Wasira akashinda kesi ile, matokeo a Bunda yakabatilishwa na hivyo Warioba asingeweza kukanyaga bungeni kwani hakuwa mbunge na jimbo la Bunda likawa wazi.
Kwa maana hiyo na uwaziri mkuu ukapotea. Ndipo hapo Mwinyi ikabidi azibe nafasi ya Warioba kwa kumteua John Malecela. Hivyo hilo ndilo sakata zima la Warioba kuukosa uwaziri mkuu.
Kuna wakati Stephen Wasira aliwahi kuulizwa kama wanasalimiana na Warioba lakini kwani ndiye hasa chanzo cha kuupoteza uwaziri mkuu.
Nadhani maelezo haya yanaweka sawa historia.