Jipe Moyo, Songa Mbele 2013

Jipe Moyo, Songa Mbele 2013

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,383
Reaction score
1,357
Haijalishi unapitia wakati au kipindi gani katika mwaka uliopita wa 2012, haijalishi huko nyuma umelia mara ngapi na bado unaendelea kulia, na haijalishi uhalisia wa maisha yako unaonyesha nini. Jambo la msingi ni kuwa Mungu yu mwaminifu daima, yeye siku zote hutuwazia yaliyo mema, anaujua mwisho wetu tangu mwanzo.

Inawezekana mapito yako ndio yamefika ukingoni, labda huu ndio mwanzo tu, hatujui hilo ila tunajua neno moja kwamba Mtetezi wako yu hai na hakika atasimama juu ya nchi. Muombe Mungu miguu ya kutembelea kwenye njia yenye miiba na utelezi ili uweze kutembea kwa ujasiri ukijua ya kuwa mbele yako kuna nchi yenye neema.

Usikatishwe tamaa na mafanikio ya wasio na haki, wewe endelea kusimama kwa uaminifu na Mungu wako na hakika utapata mahitaji ya moyo wako. Biblia inasema nawe utajifurahisha kwa Bwana naye atakupa haja ya moyo wako. Furaha yako isiwe katika vile ulivyonavyo bali katika uhusiano wako na Mungu.
Ubarikiwe ukiiweka mistari hii ndani ya moyo wako na kumwamini Mungu katika kila hatua ya maisha yako. Mungu akubariki sana


Zaburi 46:1-2 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima mioyoni mwa bahari.


2Korintho 4:16-18 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa; siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


Isaya 58:11 Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchem ambayo maji yake hayapungui.


Wafilipi 4:12-13 Najua kudhiliwa tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.


Zaburi 25:2-3-7 2-Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. 3-Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu. 7-Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.
 
Neno zuri sana, sema wasomaji wa biblia sasa humu JF wapo wachache maana sijaona hata mtu aliesema chochote kwa ajili ya neno la baraka kama hili. Asante sana mimi nazingoja baraka zangu mwaka huu wa 2013
 
Back
Top Bottom