Jipya katika hotuba ya rais Samia!

Jipya katika hotuba ya rais Samia!

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Katika hotuba yote ya rais Samia mbele ya bunge, jambo nililoliona jipya na muhimu sana, ni pale alipoahidi kuzidisha ari ya kuchimba mabwawa ya kuzuia maji Tanzania. Yaelekea serikali kadhaa zilizopita hazikujua umuhimu wa jambo hili. Kwa wale walioinukia katika miaka ya 50, 60 na 70 bila shaka watakuwa wamekuta mabwawa mengi yalioachwa na Wajerumani na Waingereza kote Tanzania. Ila kutofanyiwa ukarabati na upuuzaji kumepelekea mengi katika yao kubomoka na sehemu zilizokuwa na maji kurudi kuwa jangwa.

Katika mji wa Muheza, Mkoa wa Tanga kulikuwa na bwawa liitwalo 'Mabatani'. Hili lilichimbwa na Wakoloni na lilikuwa ndiyo chanzo kikuu cha maji, samaki, uhai wa majini na mandhari muruwa kando kand ya mji wa Muheza. Wakati tunainukia kulikuwa hakuna shida ya protein. Familia ikikosa kitoweo unatumwa kuvua samaki bwawani, na baada ya dakika chache, unarudi na kitoweo! Kuzuiwa kwa maji katika sehemu hii, kulipelekea kupatikana kwa maziwa na chemchemi chungu nzima katika mkondo (upstream) mzima unaopita maji hadi kilometa 25 hivi, hadi kwenye chimbuko (Source) la bwawa, chini ya mlimani. Hii ni kusema watu wote waliokuwa wakiishi katika mkondo huo walikuwa pia wanafaidika na samaki, ndege, na mandhari mazuri.

Kama nilivyosema, kukosekana kwa utamaduni wa ukarabati kulifanya ziwa hili libomoke mwaka 1984. Na tangu siku hiyo, mji wa Muheza umekabiliwa na shida ya maji, vumbi na ghasia nyingine. Lakini hakuna kiongozi yeyote aliyetaja jambo hili, kana kwamba halihusu na wala si muhimu.
Hii ni mara ya pili kuandika hapa juu ya 'Mabatani'. Natumai mwakilishi wetu mpya, Mwana FA, ataanza kulichimbua suala hili (pengine alikuwa hajzaliwa katika hiyo Golden Age). Lakini anaweza kuwauliza waliokuwepo na kujaribu kulirudisha ziwa hili. Akifanya hivyo, jina lake halitasahaulika!
 
MwanaFA anajiandaa kuachilia ngoma wewe unakuja na mabwawa.
 
Back
Top Bottom