Jiraji Jirani Jirani kwanini jirani?

Dola Iddy Wa Chelsea

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,526
Jiraji Jirani Jirani kwanini jirani?

Hapo awali jirani ulikuwa na tabia njema jirani!

Lakini leo wewe sio tena yule wakale jirani !

Wa leo ni mpya jirani!

Kabla umeme wa Tanesco haujafika ushirombo jirani!

Kumbuka mimi ndio nilikuwa Tanesco kwako jirani!

Kwa bei ya kutupa ya elfu 10,000/= jirani!

Wakati kwa wateja wengine wanalipa elfu 30,000/= mpaka 40 kwa mwezi jirani!

Leo hii Umevuta umeme wa Tanesco jirani!

Ndio naona tabia yako halisi jirani!

Hakuna tena salamu jirani!

Upo bize kivyako vyako jirani!

Hauna time na mimi wako mwema jirani!

Mke wangu mara ya mwisho kumfunga mtoto pampas ilikuwa takribani miezi 6 iliyopita jirani!
Lakini juzi umekuta pampas zilizotumika zimetupwa katika eneo lako ukammwagia matusi mke wangu jirani!

Sina mengi jirani kwa kuwa ule msemo wa MASIKINI AKIPATA MAT**O HULIA MBWATA upo na umeshadhihirika kwako jirani!

Baki na maisha yako jirani Fadhila zangu kwako hazikuwa kitu jirani!

NATAMATISHA JIRANIII!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…