Jirani yangu ana moyo wa kipekee sana, huwa anasomesha wafanyakazi wa ndani (house boy & girl) hadi Chuo Kikuu

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Hakika hapa duniani kuna binadamu wanatabia njema sana!

Jirani yangu pamoja na mkewe! Wana maisha ya kawaida kabisa kama yangu ya kipato cha kati!

Wakiishiwa hela wananiazima, vivyo nami nawaazima vyao nikiishiwa. Tuna maisha ya kawaida sana!

Lakini Jirani Siku zote hapo kwake haishi kupokea vijana wa kazi za ndani wa kike na kiume kwa siku zote tulizofahamiana!

Vijana hao alikuwa akinitambulisha kuwa ni watoto wa kaka na Dada zake (ndugu) wamekuja kumtembelea!

Sikuwahi kuhisi hata siku kuwa wale ni wafanyakazi!

Style yake ya maisha anavyoishi nao! anawahudumia kila kitu kama watoto wake wa kuzaa! Mke wake pia anapika nao chakula kwa zamu!

Kiufupi huwezi kabisa kujua yupi ni mtoto na yupi ni mfanyakazi!

Cha ajabu zaidi mfanyakazi akitimiza mwaka anamwandikisha chuo, (private sponsored) anasomesha kuanzia ngazi ya chini hadi degree, na ada anawalipia vizuri!

Na likizo wanarudi kama watoto wa pale!! Mmoja anaoingia chuo ndipo huagiza mfanyakazi mwingine mpya! Hivyo hivyo!

Wakati jirani yangu akifanya hivi! Mimi na Mke wangu tuko kwenye ugomvi mkubwa kwasababu kafumania meseji za house girl wangu navyomtafuna! Ndoa iko mashakani hadi majirani wameingia kusuruhuhishwa!

Ndipo huyu jamaa jirani kaamua kunisihi kuniambia kuwa hawa watoto tunatakiwa kuwahudumia na kuwasaidia kama watoto wetu! Siyo vizuri kuwarubuni kabisa!

Kaniambia hadi hivi leo, kashasomesha house girl watatu na boy mmoja (jumla wanne) na sasa kuna mwingine wa tano juzi katoka kuchukua form pale magogoni!

Ananisihi sana, badala ya kuwageuza wake, niwaone kama watoto wangu! Niwasaidie wafikie malengo!

Hakika nimesikia maumivu makubwa sana kwa tabia na moyo wa kipekee alionao jilani yangu!

Hakika nimemuelewa jirani yangu ni mtu wa kipekee sana!

Natamka wazi sitamtaka wala kumtamani house girl teeena! Hata akiwa na matako makubwa kama behewa! Sithubutu!

Nitafanya kama jirani yangu alivyo kuanzia sasa, hata kama iwe elimu ndogo ya ufundi chelehani nitasomesha ili nipande mbegu njema!
 
.
24577890.jpg
 
Tenda wema uende zako!
Na mungu analipa kwa kila jema utendalo, if not to you directly then to your blood
 
Watu wenye mioyo mizuri bado wapo...
Hapa mtaani Kuna familia moja hivi iliishi na Dada wa kazi muda mrefu..akapelekwa kusomea cherehani..akapata na mchumba..kuanzia kitchen party sendoff vyote viligharamiwa na ile familia..Tena ilikuwa sendoff ya maana.. watoto wa yule dada kila likizo wanakuja kwenye hiyo familia.. mwenyewe anawaita wajukuu wa Kwanza..tuwapende na tuwahurumie wadada Jamani.
 
Hata mimi kuna Binamu yangu (Mungu amrehemu ashafariki) yeye na mume wake walimsomesha dada yao wa kazi, akamaliza akapata bwana mwenye kazi nzuri na huenda hata huyo bwana hakuwahi kujua kama yule dada alikuwa dada wa kazi. Wakamfanyie send off maana wazazi wake walikuwa hawana uwezo wa huko Iringa vijijini, wakawaleta harusi ilifanyikia hapa DSM mdada akaolewa akaanza maisha yake sasa hivi ni mtu mwingine kabisa.

Kuna mkaka flani alikuwa anaishi familiamoja hapo mbezi alikuwa houseboy, anapika anadeki nyumba, anafua nguo. Lakini nje ya nyumba usingeweza kujua kama ni houseboy maana alikuwa akitoka ni anasukuma mkoko wa maana. Hadi alikuwa ana demu mkali anasoma ardhi. Sema nahisi yule demu alikuwa yupo kimaslahi maana jamaa alikuwa anamleta pale kwao maboss wakiwepo anakuwa anapika kazi wakati demu yuko sebuleni. Sema jamaa alikuwa anaaminiwa sana na mama mwenye nyumba hivyo alikuwa ana vijisent sana. hadi fununu wakawa wanasema anamtafuna mama mwenye nyumba maana si kwa urafiki na kijana wake yule.
 
Hakika hapa duniani kuna binadamu wanatabia njema sana!

Jirani yangu pamoja na mkewe! Wana maisha ya kawaida kabisa kama yangu ya kipato cha kati!

Wakiishiwa hela wananiazima, vivyo nami nawaazima vyao nikiishiwa. Tuna maisha ya kawaida sana!

Lakini Jirani Siku zote hapo kwake haishi kupokea vijana wa kazi za ndani wa kike na kiume kwa siku zote tulizofahamiana!

Vijana hao alikuwa akinitambulisha kuwa ni watoto wa kaka na Dada zake (ndugu) wamekuja kumtembelea!

Sikuwahi kuhisi hata siku kuwa wale ni wafanyakazi!

Style yake ya maisha anavyoishi nao! anawahudumia kila kitu kama watoto wake wa kuzaa! Mke wake pia anapika nao chakula kwa zamu!

Kiufupi huwezi kabisa kujua yupi ni mtoto na yupi ni mfanyakazi!

Cha ajabu zaidi mfanyakazi akitimiza mwaka anamwandikisha chuo, (private sponsored) anasomesha kuanzia ngazi ya chini hadi degree, na ada anawalipia vizuri!

Na likizo wanarudi kama watoto wa pale!! Mmoja anaoingia chuo ndipo huagiza mfanyakazi mwingine mpya! Hivyo hivyo!

Wakati jirani yangu akifanya hivi! Mimi na Mke wangu tuko kwenye ugomvi mkubwa kwasababu kafumania meseji za house girl wangu navyomtafuna! Ndoa iko mashakani hadi majirani wameingia kusuruhuhishwa!

Ndipo huyu jamaa jirani kaamua kunisihi kuniambia kuwa hawa watoto tunatakiwa kuwahudumia na kuwasaidia kama watoto wetu! Siyo vizuri kuwarubuni kabisa!

Kaniambia hadi hivi leo, kashasomesha house girl watatu na boy mmoja (jumla wanne) na sasa kuna mwingine wa tano juzi katoka kuchukua form pale magogoni!

Ananisihi sana, badala ya kuwageuza wake, niwaone kama watoto wangu! Niwasaidie wafikie malengo!

Hakika nimesikia maumivu makubwa sana kwa tabia na moyo wa kipekee alionao jilani yangu!

Hakika nimemuelewa jirani yangu ni mtu wa kipekee sana!

Natamka wazi sitamtaka wala kumtamani house girl teeena! Hata akiwa na matako makubwa kama behewa! Sithubutu!

Nitafanya kama jirani yangu alivyo kuanzia sasa, hata kama iwe elimu ndogo ya ufundi chelehani nitasomesha ili nipande mbegu njema!
umeandikanpoints nzuri lakini zimeyeyushwa na maneno ya hovyo uliyoingiza humo
 
Mkuu sema nawe ulizingua house yupo ndani mwako kwann mchat kwenye msg?..yaan kuku wako manati ya nini?,huyo ulipaswa uharibu tu kitasa cha mlango basi!
 
Big mistake !

Kama ni Mfanyakazi mpe stahiki yake, mlipie NSSF kila mwezi pamoja na Bima ya Afya basi hayo mengine siyo kazi yako, kama unataka mtoto nenda kaasili Vituo wapo watoto wengi wenye mahitaji, ...
 
Guys binadamu wenye roho mbaya wanahesabika duniani

wengi wenye roho mbaya si wao ila ni umaskini uliowazidi

kusomesha binti chuo private ulipie ada na makorokoro yakubidi

uwe nazo wasiowasomesha wengi shida ni uwezo,watoto wake wenyewe

wameishia la SABA yeye mwenyewe ana zero form 4 leo aje asomeshe dada wa kazi

Pesa ikiwepo huwa naamini hata nia mbaya/tabia mbaya/roho mbaya za binadamu zitapungua sana.
 
Watu wenye mioyo mizuri bado wapo...
Hapa mtaani Kuna familia moja hivi iliishi na Dada wa kazi muda mrefu..akapelekwa kusomea cherehani..akapata na mchumba..kuanzia kitchen party sendoff vyote viligharamiwa na ile familia..Tena ilikuwa sendoff ya maana.. watoto wa yule dada kila likizo wanakuja kwenye hiyo familia.. mwenyewe anawaita wajukuu wa Kwanza..tuwapende na tuwahurumie wadada Jamani.
Kabisa
 
Mkuu kumbe house girl wako ana matako makubwa

Punguza kuchagua makalio angalia kichwa mkuu kama ana ubongo
 
Umeanza vizuri sana ila ulipofika hapo katikati tu sijui unawala mahausigeli nikaacha na kusoma kabisa nikaona haya matangazo inatakiwa ulipie huna tofauti na wale wanagawa vi peperushi vya waganga wa kienyeji mabarabarani
 
Back
Top Bottom