Jirani yangu kaenda Sumbawanga kisa kuku wake kapotea

Jirani yangu kaenda Sumbawanga kisa kuku wake kapotea

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
Kama kichwa kinavyojieleza wakuu,

Kuku wa jirani Yangu amepotea sasa jirani yangu huyu yeye badala ya kuniuliza kasafiri Kimya Kimya kwenda Sumbawanga sasa Matatizo huwayanatatuliwa hivyo Jamani.

Jana jioni ndio napata taarifa yake kuwa amekwenda Sumbawanga kwa ajili ya swala la kuku wake.
 
Atakuwa kaenda kununua kuku wengine huko kijijini kwao
 
Wengine wanajua kutisha watu, kuku Bei gani alafu nauli kwenda na kurudi si Bora anunue kuku mwingine tu.
 
Yaan usithubutu kugusa kitu cha mtu uswahili ayo tushayapitia sn tu
 
Wengine wanajua kutisha watu, kuku Bei gani alafu nauli kwenda na kurudi si Bora anunue kuku mwingine tu.
Ukinunua kuku mwingine jambo hili litajirudia bora ugharamike halafu wawe na uoga kurudia kugusa vya watu.
 
Jana nimechinja mbuzi usiku, asubuhi nimeamka nimemkuta zizini, lakini mbwa wa jirani hajulikani alipo tangu jana usiku. Fb
 
Toka VVD aumie Liverpool imekuwa inasema sababu ya kufungwa eti ni pengo lake la kukosekana uwanjani.
 
Hata kwenye level ya nchi Kuku akipotea wanaenda Sumbawanga pia.Imagine zimetumika billion nne kusaka kimtu kinachoitwa Kigogo!
6789076.jpg
 
Back
Top Bottom