Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Uzi umevamiwa na vibwengo.

Kwenye fictional literature kuna minor (secondary) character ambaye yeye yupo kusaidia main character na kusaidia kusukuma plot events forward.
For that case mke wa jamaa ni minor character ambavyo kimsingi minor character si lazima kuhusishwa/kutajwatajwa kwenye matukio ni endapo tu inabidi kumhusisha.
Ndicho anachokifanya bwana SteveMollel.
Umeshajua ana familia, period. Utaona mke wake na mtoto baadaye maana hawa ni supporting characters hawana kipaumbele kwenye matukio, kama kuhusika (kutajwa) watahusika (watatajwa) kwenye plots za muhimu tu.


Pamoja na story kuvutia kumsahau mkewe katika story hiyo ilikuwa ni moja ya mapungufu makubwa katika hiyo story, unakumbuka kipindi wapangaji walipoweka kikao na baba mwenye nyumba??-- Wakati huo mke wa Bigi saa zote alikuwa kamkazia macho Mollel, watu tulihoji akilini mke wa Mollel wakati huo alikuwa wapi??, kwa utoaji wa macho wa mke wa Big kwa mollel je mke wa Big alikuwa anatupa agenda ya mapenzi kwa Molel akijua kwamba Mollel alikuwa single ??-- Maswali mengi yalikuwa yanaibuka kutokuwepo mke wake toka mwanzo wa story.

Tukubali kwamba mke wa molel kukosekana mwanzoni mwa story kwa mazingira ya story yalivyo ni mapungufu, nadhani kwa umahiri wake Molel anaweza kulifanyia kazi jambo hilo next time in case the story is to be published.
 
Jamani ee kwenye fasihi Kuna wahusika wakuu na wahusika napa mhusika bapa anaweza akaonekana maramoja tu kwenye stori, mhusika wetu mkuu hapa ni Big na ndugu msimuliaji basii tukomae na Jao nyiemnaotaka amtaje mkewe mnataka nini Kwa huyo mke?


Shemeji yetu akose kutajwa kwenye hadithi Kwanini??, au alikuwa anaishi na mchepuko?? au alikuwa anamlia rada mke wa Bigi??, si unakumbuka mke wa Bigi kwenye kikao na baba mwenye nyumba alikuwa akimtolea mimacho Molel bila kupepesa!!🤣🤣--- Utani tu huo.

Ila huyo Mollel yupo mahiri kweliii kwa simulizi. Kudos Mollel.
 
Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 08



Baada ya mtoto yule kupata huduma ya kadiri ilivyowezekana, kila mtu aliendelea na shughuli yake. Kasheshe ilikuja baadae kwenye majira ya saa nne hivi, nikiwa natazama marudio ya habari kwenye runinga, nilisikia kelele na zogo, kelele ambazo zilikuwa zinaita huko nje ya nyumba kubwa. Kelele hizo hazikudumu kwa muda mrefu huko nje mara zikajongea ndani hivyo nikazidi kuzisikia kwa ukaribu, nikatambua kulikuwa na ugomvi, ugomvi ulosababishwa na kipigo cha mtoto yule kwani aliyekuwa anaongea hapo kwa ukali alikuwa ni mama wa yule mtoto tuliyemkuta analia akivuja damu.

Mama huyo, sisi tulizoea kumuita Bembela, sijui kama lilikuwa jina lake halisi au lah, alikuwa ni mwanamke anayejihusisha na shughuli za mama n’tilie pale Goba kontena, nyuma ya kituo cha mwelekeo wa kwenda Goba centre, kabla hapajabomolewa na ile kampeni ya serikali ya kusafisha vituo hivi vya madaladala kwa kuwaondoa watu wanaohusika na uchuuzi wa bidhaa ndogondogo katika mfumo usokuwa rasmi.

Hapo, akiwa pamoja na wamama wengine kama wawili hivi achilia mbali mabanda mawili ya chips, walikuwa wanauza chakula mpaka majira ya usiku wa saa tatu hivi au saa nne, nahisi inategemea na mauzo ya siku hiyo kama chakula kitaisha mapema au lah. Mimi mara kwa mara nilikuwa nikipata chakula kwake haswa nikiwa mwenyewe nyumbani, so nikitoka kazini napitia kwake nakula kisha nashuka zangu nyumbani. Kwasababu alikuwa ananifahamu, alikuwa ananizingatia sana kwenye huduma na chakula.

Kwa makutano hayo machachemachache, story za hapa na pale haswa tukikutana zaidi katika mazingira yake ya kazi, nilipata kumjua Bembela kama mwanamke mmoja mpambanaji sana. Mungu ambariki huko aliko. Kwa kupitia shughuli za mikono yake alikuwa analipia kodi ya pango na anamsomemsha mwanaye. Bembela alikuwa ni ‘single mother’. Lakini mbali na hapo alikuwa ni mwanamke mmoja mwongeaji mno, kuongea kwake si kazi, na kama ungepata kula kwake basi ungelichukua sekunde chache sana kujua haiba yake hiyo. Sauti yake ni kali na anapenda kusema hili na lile hapa na pale.

Basi kitambo kidogo tu, mimi nikiwa hapo sebuleni nilisikia mlango fulani unabamizwa bum-bum-bum, kwa ukali, kisha sauti ya Bembela ikanguruma, “haya nyie mabondia, tokeni nje tupigane!” Nikajua swala hili sio la mchezo., wakati huo nikawa nasikia na majirani wengine kwa mbali wakiwa wanaongeaongea huko nje.

Kidogo tena Bembela akaubamiza mlango kwa fasheni ileile, bum-bum-bum-bum, alafu akaropoka; “nasema tokeni, nyie si mnajifanya mtoto wenu ni bondia, haya nimemleta huyu aendelee kumpiga.”

Nikatambua Bembela amekuja hapo kwa shari kamili na si nusu shari. Amekuja hapo kuwasha moto, si kuuzima. Aliendelea kuubamiza mlango na kuongea kwa nguvu akisema namna gani anavyomlelea na kumpambania mwanaye kwa tabu alafu mtu anakuja na kumjeruhi kiurahisi. Akaenda mbele zaidi akiuliza kama jirani huyo anaujua uchungu aloupata akijifungua mtoto huyo, lakini maneno yote hayo hayakusaidia kitu kwani mlango aliokuwa anaufokea na kuubamiza hakufunguliwa kamwe. Zaidi sisi majirani, ambao kwa namna moja ama nyingine ndo’ tulikuwa tunaathirika na makelele yake majira yale ya usiku ndo’ tulitoka kumtuliza jazba na kumsihi atumie njia nyingine ya stara.

Bembela aling’aka, “hapana, hawa hawana ustaarabu na ndo’ maana hawastahili ustaarabu vilevile! Wanajua kabisa mtoto wao alichokifanya, wanashindwa kuja kuomba radhi au kuongea na mimi? Maana yake nini kama sio wamedhamiria? Ndo maana nimemleta huyu mtoto hapa waendelee kumpiga!”

Mwanamke huyo alikuwa anaongea kwa mikono mingi mno na vidole vya majigambo. Dera lake amelibana na mtandio kiunoni. Uso wake umefura kweli, anaongea huku mdomo ukienda pembeni, lakini kama ungemsikiliza vema Bembela ungebaini kulikuwa na presha fulani ambayo alipewa na mwanamke mwenzake wa jirani, mmoja wa wanawake tuliowakuta wakiwa na mtoto yule wakati sisi tunatokea kwenye mkutano, maana Bembela alisema muda wote huo wazazi wa yule mtoto hawakufanya jambo lolote pamoja na kwamba waligongewa na kuambiwa, sasa muda wote upi ingali yeye alikuwa amerejea kazini muda si mrefu? Hivyo bila shaka alikuwa amepewa maneno juu ya yale yaliyotokea na nilimjua vema mtu huyo aliyemwambia kwani naye alikuwa akiongezea nyama katika maneno hapa na pale.

Mwanamke huyo katika moja ya kuthibitisha hoja yake, alimuuliza mke wangu ambaye alikuwa amesimama kwenye kingo ya mlango, eti mama fulani hukuwagongea mlango saa ile kuwaita? Walitoka?

Basi zogo lile lilidumu kwa muda kidogo hapo pasipo kuzaa matunda yoyote kwani mhusika hakupata kuonekana mpaka mwisho wake, matokeo yake kwenye majira ya kama saa sita hivi, kila mtu alirudi kwenye makazi yake usiku ukazidi kusonga mbele, lakini kisa kile cha mtoto wa BIGI na mapigano yake ndo’ ulikuwa mwanzo mzuri kabisa kwa watu wasiokuwa na maisha ya usiku mkubwa kuanza kuinyooshea kidole familia ile lakini kwa ambao walikuwa na desturi ya kulala kesho yake kama mimi na ambao walikuwa wanapata kuwa macho mara kadhaa kwenye usiku mkubwa kama Tarimo, ile haikuwa ‘breaking news’ bali tu mwendelezo wake.

Ni tokea hapo, ndipo niligundua hisia za udadisi zilizopo ndani ya mke wangu zikaanza kumea kwa kasi, kitu ambacho mimi binafsi nilikihofia sana kutokana na hali aliyokuwa nayo muda huo, ujauzito wa takribani miezi mitano au sita hivi kama niko sahihi. Usiku huo, baada ya lile zogo na kabla ya yeye kwenda kulala, alinieleza vizuri vyote vilivyojiri mpaka kupelekea tukio lile la mapigano na watoto kuumizana.

Aliniambia katika majira yale ya jioni, yeye alikuwa nje anaanua nguo za mtoto alizopata kuzifua asubuhi yake. Akiwa katika zoezi hilo, kama ilivyo kawaida ya weekend, watoto wengi walikuwa wanazungukazunguka wakicheza huku na kule ikiwemo mtoto yule wa Bembela lakini kwasababu ya majira kuanza kuwatupa mkono, yaani jua kuanza kuzama, jirani mmoja mwanamke, yule ambaye mimi nilihisi ndo’ alimpa maneno Bembela, alianza kuwasihi watoto wale kuacha michezo warejee majumbani mwao kwani giza lishaingia, ni hatari kucheza muda huo kwasababu wanaweza kusababisha ajali na majeraha.

Basi watoto wakapungua, wengi wao wakirejea ndani mwao na wale wa mbali wakaanza safari, hapo wakabakia mtoto wa Bembela na mtoto wa huyo mama jirani. Bembela yeye tofauti na wengine hakuwa na mzazi wa kumwita muda huo wala wa kwenda kukaa naye ndani, mama yake yuko shughulini mpaka majira ya usiku wa saa tatu au nne, kwasababu hiyo basi mtoto huyo alifurahia kupata angalau ‘kampani’ ya mtoto mmoja aliyebaki naye, watoto hao wakawa wapo kibarazani wanachezea ile midoli ya kike.

‘Wife’ aliendelea kuanua nguo zake na alipomaliza alibaini nguo zile hazikuwa timilifu, kwa mujibu wake kuna nguo mbili za mtoto hakuziona, kwasababu hiyo alienda kwenye moja ya mlango wa mtu ambaye naye alifua siku ile na kuanika kumuuliza kama amekosea kwenye kuanua akabeba na nguo zake. Alipotoka huko, japokuwa hizo nguo hakupata kuziona, alirejea akakuta pale kibarazani kuna watoto watatu, mmoja wa kiume ameongezeka, mtoto huyo alikuwa amemwona kwa mara ya pili sasa tangu wamehamia pale na siku hiyo ndo’ alipata kumwona kwa ukaribu alipokatiza kupeleka nguo ndani, mtoto huyo alikuwa anachekacheka mdomo wake ukichuruza udenda, hapo ndo’ akajua hakuwa mzima wa akili na huenda hiyo ndo’ sababu wazazi wake wanamfungia sana ndani, ni ngumu sana kumwona nje.

Alipeleka nguo zake ndani, lakini kitambo kidogo akiwa anazikunja nguo hizo akasikia sauti kali ya mtoto analia pale nje, alitoka upesi kwenda kutazama, alipofungua mlango akamkuta mtoto yule mwenye matatizo ya akili akiwa amesimama mlangoni kwao anatazama nje kwa kuchungulia. Alimwendea mtoto anayelia nje akamkuta mtoto yule wa Bembela ameshikilia kichwa chake anavuja damu, hapo ndipo yakaendelea na mengine mpaka sisi kuwakuta pale wakati tunatoka kwenye kile kikao.

Aliponieleza yote hayo, mimi nikatokea kuamini labda mtoto yule alikuwapo mwenyewe nyumbani na ndio maana aliufunga mlango hivyo hakukuwa na mtu mwingine wa kutoka nje kuja kumwona majeruhi, swala hilo mke wangu akakataa, yeye aliamini kulikuwa na mtu mule ndani kwani kuna muda fulani wakati anatazama maharage jikoni alisikia sauti ya mwanaume ikifoka kidogo mule ndani kwahiyo aliamini kabisa baba yumo.

Pale mimi nilipokuwa naishi, ‘wife’ na hata wanawake wengine wa ile nyumba kubwa walikuwa na utaratibu wa kupikia kwenye majiko mawili ya mkaa yaliyokuwa yanakaa koridoni, majiko hayo yalikuwa yanasaidia kwenye kutunza gesi kwa kutumika kama mbadala wa kupikia vitu vya muda mrefu mathalani maharage na njugu mawe. Majiko hayo yalikuwa hapo muda wote, hamna aliyethubutu kupikia jiko la mkaa ndani mwake.

Basi baada ya maongezi hayo mimi nilibaki sebuleni peke yangu. Nilikaa hapo mpaka majira yangu ya kawaida nilipoanza kuhisi kichwa change kizito ndipo nikaenda kujilaza.

Niliamini kabisa usiku huo na makeke yake ulikuwa umeshapita, lakini muda kidogo mbele kama baada ya lisaa limoja hivi mimi kuwapo kitandani, nikagundua kumbe usiku ule bado ulikuwa na mimi. Usiku ule ulikuwa haujamaliza mambo yake.







***
Inachosha unaandika vitu havina hata maana , mpaka mtu unaburuza Aya nyingine

Mfano kulikuwa Kuna haja gani ya kufafanua umama ntilie wa bembela? Kuwa anauzia sehemu Fulani sijui anauza mpaka saa sita za usiku mara kubomolewa vibanda duuh!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Inachosha unaandika vitu havina hata maana , mpaka mtu unaburuza Aya nyingine

Mfano kulikuwa Kuna haja gani ya kufafanua umama ntilie wa bembela? Kuwa anauzia sehemu Fulani sijui anauza mpaka saa sita za usiku mara kubomolewa vibanda duuh!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Hivi umesoma mpaka mwisho ukaona hayo mambo hayana maana? Unajuaje kama nitakuja kuongelea hiyo setting hapo baadae ikiwa related na matukio ya Jirani?


Kila ninachoandika, every detail, ni muhimu sana kwenye mtiririko wangu. Unaweza usione kwa sasa ila baadae uka-appreciate.


Nyie mnaoburuza aya ndo baadae mnaanza kuongea vitu ambavyo kumbe vilishainishwa huko nyuma in details alafu useme hadithi ina ukakasi.
 
Hivi umesoma mpaka mwisho ukaona hayo mambo hayana maana? Unajuaje kama nitakuja kuongelea hiyo setting hapo baadae ikiwa related na matukio ya Jirani?


Kila ninachoandika, every detail, ni muhimu sana kwenye mtiririko wangu. Unaweza usione kwa sasa ila baadae uka-appreciate.


Nyie mnaoburuza aya ndo baadae mnaanza kuongea vitu ambavyo kumbe vilishainishwa huko nyuma in details alafu useme hadithi ina ukakasi.
Acha kujibu kila swali, kwa mwenye akili akisoma ataelewa kwanini ulielezea profile yake. Tupe muendelezo mkuu
 
Inachosha unaandika vitu havina hata maana , mpaka mtu unaburuza Aya nyingine

Mfano kulikuwa Kuna haja gani ya kufafanua umama ntilie wa bembela? Kuwa anauzia sehemu Fulani sijui anauza mpaka saa sita za usiku mara kubomolewa vibanda duuh!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app


Hapa anataka kudhihirisha kwamba hiyo ni true story.
 
Hivi umesoma mpaka mwisho ukaona hayo mambo hayana maana? Unajuaje kama nitakuja kuongelea hiyo setting hapo baadae ikiwa related na matukio ya Jirani?


Kila ninachoandika, every detail, ni muhimu sana kwenye mtiririko wangu. Unaweza usione kwa sasa ila baadae uka-appreciate.


Nyie mnaoburuza aya ndo baadae mnaanza kuongea vitu ambavyo kumbe vilishainishwa huko nyuma in details alafu useme hadithi ina ukakasi.
Achana nae
 
Hapa ndani kuna watu hawana shukrani jamani hadi aibu.
Oooh mara hivi mara vile, Yani kama mtu anaona anajua sana kuandika atoe na yeye story yake tuone kama kweli ako na ubavu majitu mengine sijui yakoje aiseh.
Tulia wewe "fom foo felia". Ulishindwa kuuliza mwaswali darasani ukafeli hata hapa unashindwa kuuliza?
 
Ndugu Steve una maneno mazuri ya kiswahili na mpangilio mzuri wa kuandika story ila kuna mambo unachanganya mfano
1. Jana nilisoma kuwa mtoto wa BIG ndio kaumia leo nasoma mtoto wa jirani. Umechangajya wewe au ni mimi sijaelew


3. Jina Bembela umelitumia kwa mama n mtoto pia umemwita hivyo. .

Huyo mama anaitwa Mama Bembela,hivyo basi Bembela ni mtoto,pia mtoto alie jeruhiwa toka episode iliyopita ni mtoto wa Mama Bembela,rejea point ya kuwa wewe ndio umejichanganya
 
Mkuu ungekausha tu kujibu..wewe shusha tu episodes! Hawa wadwanzi tuachie sisi..
Jinga jingine hili. Unasoma kama kasuku, huwezi kupambanua mambo, unapelekwa tu. Itabidi mfumo wa elimu Tanzania ubadilishwe ili tusiwe na watu wa hovyo kama hawa.
 
Hii Episode ya 8 kusema ukweli hamna kitu... bora isingeandikwa kabisa. Vitu vinarukwa rukwa na kuchomekwa vingine kabla vya episode iliyopita havijatengemaa. Hapa issue ni BIG na yanayomhusu,hayo mengine ni kujaza server tu!
 
Back
Top Bottom