Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Pamoja na story kuvutia kumsahau mkewe katika story hiyo ilikuwa ni moja ya mapungufu makubwa katika hiyo story, unakumbuka kipindi wapangaji walipoweka kikao na baba mwenye nyumba??-- Wakati huo mke wa Bigi saa zote alikuwa kamkazia macho Mollel, watu tulihoji akilini mke wa Mollel wakati huo alikuwa wapi??, kwa utoaji wa macho wa mke wa Big kwa mollel je mke wa Big alikuwa anatupa agenda ya mapenzi kwa Molel akijua kwamba Mollel alikuwa single ??-- Maswali mengi yalikuwa yanaibuka kutokuwepo mke wake toka mwanzo wa story.

Tukubali kwamba mke wa molel kukosekana mwanzoni mwa story kwa mazingira ya story yalivyo ni mapungufu, nadhani kwa umahiri wake Molel anaweza kulifanyia kazi jambo hilo next time in case the story is to be published.
Muandishi kaweka wazi kuna muda huwa anakula kwa Mama Bembela ikiwa mkewe hayupo,pia mkewe kwenye hii hadithi yetu ya kusisimua sio Mhusika mkuu.
 
Pamoja na story kuvutia kumsahau mkewe katika story hiyo ilikuwa ni moja ya mapungufu makubwa katika hiyo story, unakumbuka kipindi wapangaji walipoweka kikao na baba mwenye nyumba??-- Wakati huo mke wa Bigi saa zote alikuwa kamkazia macho Mollel, watu tulihoji akilini mke wa Mollel wakati huo alikuwa wapi??, kwa utoaji wa macho wa mke wa Big kwa mollel je mke wa Big alikuwa anatupa agenda ya mapenzi kwa Molel akijua kwamba Mollel alikuwa single ??-- Maswali mengi yalikuwa yanaibuka kutokuwepo mke wake toka mwanzo wa story.

Tukubali kwamba mke wa molel kukosekana mwanzoni mwa story kwa mazingira ya story yalivyo ni mapungufu, nadhani kwa umahiri wake Molel anaweza kulifanyia kazi jambo hilo next time in case the story is to be published.
Mjuaji kazini!!??
ww kula story pita vile
 
Inachosha unaandika vitu havina hata maana , mpaka mtu unaburuza Aya nyingine

Mfano kulikuwa Kuna haja gani ya kufafanua umama ntilie wa bembela? Kuwa anauzia sehemu Fulani sijui anauza mpaka saa sita za usiku mara kubomolewa vibanda duuh!

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Nafikiri hizo information utaona umuhimu wake baadae
 
Utake ama usitake sisi kusema ni lazima tu mkuu na ukiona unakasirika basi ujue wewe si muungwana. Cheki haya:-
A.Mke kwenye intro unae lakini Stori ilivyoanza hukuwa nae (na ikapendeza uwe huna mke). Kuna waliotetea kwamba mke alitajwa kwenye geti limefungwa na Bonge huku ukiwa bafuni. Labda wenzetu hawawezi kusoma maana ulisema ulisogelea madirisha ya waliokuwa ndani (majirani) na mpaka jirani mwenyewe akakuona kabla hujagonga Wala kumwita sasa hapo mke yukwapi?

B.Umesema mke hakukuwA na sababu ya kumtaja maana hakukuwA na sehemu ya mojakwamoja ya yeye kuingia mapema ikaendana na stori. Wakati huohuo umesahau Kuna Stori kibao umezirefusha ambazo basins muunganiko wa mojakwamoja na stori. Mfano story za agenda za mkutano mpaka zilivyowasilishwa, Stori ya mama Bembela, na mifano mingine

C.Unalala kesho yake lakini hakuna hata mke kukuamsha kwenye usingizi mzito. Unatulia dirishani si chini ya nusu saa lakini hakuna hata mke kushtuka siku moja na kushangaa hata akakuuliza kulikoni. Hospital sijui zahanati mkitaka kwenda mke hakushiriki hata kunyanyua gauni la jirani yake lisiingie kwenye tairi ya pikipiki.

D.Bembela ni jirani yako lakini tena Bembela ni mtoto wa huyohuyo jirani yako. Halafu walikuwa wanazozana lakini kumbe kutoka ni Bembela kamleta mtoto apigwe na kwa Big hayupo aliyetoka sasa sijui alikuwa anazozana na nani. Mtoto wa big ulisema ni chizi like lakini hapo mwisho umetaja watoto kukaongezeka tena kama chizi wa pili ambapo umesema mkeo hakuwa akimjua vizuri kwakuwa alikuwa akifungiwa (au ni Mimi nimeshindwa kusoma na kuelewa labda).

E.Kwa macho ya wanawake lakini mkeo hakuweza kuona mke wa Big anavyokukata jicho. Hakuandalii maji, chakula, hakupokei, Wala hamuagani ukitoka. Tufanye hakuwepo kikaoni basi au alisafiri Kipindi chote Cha mauzauza. Una Kazi Fulani unamalizia kwa Laptop lakini... au basi!

Kuna mtu alisema kadiri unavyoirefusha Stori ndo unavyozidi kuiharibu, nimeamini nilipofika sehemu ya 8. Labda tu niseme wazi Mimi sinaga tabia ya kufuatilia maseason au mastori yenye episodes lakini hii ilinivutia kuifuatilia nikaisoma yote. Kusema ukweli ilipofika kwenye unaenda kilabuni kutafuta mbege nikaanza kukosa mvuto ila nikajikaza nikijua mbele itarudi itakuwa nzuri lakini kwa mpaka kufikia sehemu ya 8 niseme tu safari imenishinda nakung'uta matako naaga mashindano rasmi.
Mtanipa summury mtakaomaliza yote
 
Mleta story endelea kukaza hivi hivi...wale wanaotaka mkeo awepo Kila episode waiendeleze wao iwe wanavyotaka....msalimie BIGI, Tarimo nae anaendeleaje?
😅😅😅😅
 
Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 07




Nilitazama ndani ya kiroba kile pasipo kujali harufu yake kali iliyonifanya nizibe pua, ndani yake nikakuta nywele nyingi, sikujua ni nywele za nini na za wapi ila zilikuwa nywele ndefundefu za usinga, nguo zilizojifinyangafinyanga na nyama zilizokuwa zinatoa harufu … nyama ya nini hii? Nilijiuliza nikipekua, kidogo nikakutana na kichwa cha mbuzi, kichwa hicho kilikuwa na pembe fupi ambazo zimengushiwa uzi mwekundu, kukibinua kichwa hicho kukikagua na kukitazama vema mara nikasikia kitu kimedondoka mguuni pangu, nikapatwa na hofu kubwa, niliangaza upesi kwa tochi ya simu nikaona sarafu ya hamsini iko chini, sarafu hiyo ni mpya kama imetoka benki muda huu.

Niliichukua sarafu hiyo nikaiweka mfukoni kisha nikaendelea kupekuapekua kiroba kile kwa kijiti, nywele nyingi nisizozeielewa pamoja na manyoyamanyoya ambayo niliamini ni ya mbuzi yule yalijaa humo, kabla sijamaliza zoezi hilo nikasikia sauti za wanaume wakiwa wanateta, wanaume hao walikuwa wanakuja kutokea upande ule wa bar nilikotokea.

Nilitazama upande huo nikaona mwanga wa tochi ukimulikamulika, na pia nikasikia vishindo vya miguu vikisogea kwa upesi, basi haraka nikaona ni vema nikajificha kwani nikionekana hapo hakuna mtu atakayenielewa kuwa mimi ni mshuhudiaji tu, niliona hilo ni wazo bora kwasababu kama ningejaribu kukimbia ama kurejea katika njia yangu basi wangenikuta kabla sijafanikisha hilo na basi wangehisi kuna kitu kinaendelea na mimi humo korongoni.

Nikajibana nyuma ya mti nikatulia tuli niwezavyo, nikawasikia watu wale wakijongea na kujongea karibu huku wanaongeaongea, tochi yao kali inamulika hapa na pale, mwendo wao wa upesi sana.

Majamaa wale walipofika mahali fulani katikati ya korongo lile, katika kumulikamulika kwao huku na kule, wakamulika kile kiroba nilichokuwa nakipekua, nikamsikia mmoja akisema;

“Oya, nini kile?”

Nilitazama nikiwa hapo nyuma ya mti, nikaona kile kichwa cha mbuzi. Sijui akili yangu ilikuwa wapi, kumbe kile kichwa nilikitupia chini nikakiacha papo hapo, sasa kichwa hicho kilikuwa kimesimama chini kikitazamia kule njiani! Nikahamaki na moyo wangu. Niliogopa watu wale wasije kwa karibu kukitazama kwani wakifanya hivyo tu basi ningekuwa nimekwisha. Japo sikuwa kwa ukaribu mkubwa lakini uwezekano wa kuniona nilipojibana ulikuwa ni mkubwa pia.

Mwingine akamjibu mwenziwe: “Mbona kama kichwa cha mbuzi?” Walimulikamulika maeneo hayo ya karibu huku wakiwa wanaongeaongea kuhusu korongo lile, mimi akili yangu ikiwa inaomba tu wasije wakasogea upande wangu, muda si mrefu wakakata shauri wakaondoka kuendelea na safari yao, hiyo ndo’ ikawa ahueni yangu.

Mabwana wale wakawa wameenda wakiwa wemeniachia funzo kubwa kwani nilihisi nimevuka sana mipaka na sikutakiwa kabisa kufanya yale niliyoyafanya. Vipi kama ningeonekana hapo na watu wakanishuku na kunidhuru kwa ulozi?

Nilitoka nikaenda nyumbani moja kwa moja, hakukuwa na kingine siku hiyo, nilijilaza na kwa msaada wa pombe nilizokunywa siku hiyo nikapitiwa na usingizi mapema ya saa saba, hiyo kwangu ilikuwa ni mapema maana si kawaida yangu. Kesho yake nikaendelea na mambo yangu mengine huku nikiwa najaribu kuona ratiba yangu itakuaje hapo karibuni ili nikapate kumtembelea bwana Tarimo kule Muhimbili.

Ikapita siku na masiku, bado sikwenda kumtazama mgonjwa, kila nilipojifaragua na ratiba ya kazi sikufanikiwa kabisa kupata upenyo hata weekend nilihisi uchovu, kiasi kwamba yule jirani niliyeagana naye kwenda pamoja hospitali akajiendea mwenyewe. Bwana huyo aliendea siku tatu tu baada ya siku ile ya Mwananyamala, mimi nikaapa mwisho wa wiki ijayo, yaani weekend nyingine inayofuata, haswa Jumapili, lazima nitaenda kumwona bwana yule kumjulia hali, kwahiyo kwa wakati wote huo nilikuwa naulizia tu na kupewa habari za mgonjwa toka kwenye vinywa vya watu wengine.

Nakumbuka vema, ilipofika siku ya Jumamosi, yani bado siku moja kwenda kumtembelea mgonjwa kama nilivyopanga, nikiwa nipo nyumbani pamoja na familia majira ya asubuhi, tulisikia tangazo la kipaza sauti likikatiza katika mitaa yetu, kwa mara ya kwanza nikadhani ni watu wa kuuza sumu za panya, mende, kunguni na viroboto maana nao siku hizi wamerahisisha kazi zao kwa vipaza sauti lakini kitambo kidogo tangazo hilo lilifika karibu nikalisikia vema, lilikuwa ni tangazo la kukumbusha kikao cha mtaa wa Mashuka, wito ukitolewa na mwenyekiti.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kikao kilikuwa kinafanyika kuanzia saa kumi jioni kwenye kiuwanja fulani kidogo ambacho kilikuwepo upande wa kushoto mita chache tu tangu ukiacha njia pana iliyosakafiwa kama unatokea kituo cha Kontena kushuka zaidi kule Mashuka. Kiwanja hiko hakikuwa rasmi, kilikuwa kipo tu katika ‘saiti’ ambayo haikumaliziwa, nyumba fulani hivi ambayo ni kama ilitelekezwa kwa muda kidogo.

Agenda kuu ya kikao hiko ilikuwa ni kujadili kuhusu kumaliziwa kwa barabara ile ya sakafu tokea pale ilipokuwa imeishia, mbele kidogo ya geti la lile ghorofa la bweni la Saint Joseph, iende mpaka mwisho kabisa wa Mashuka, yani njia zima kusiwe na vumbi.

Tangazo hilo kwangu likawa ndo’ mara ya kwanza kulisikia lakini nilipouliza, ‘wife’ akaniambia ni siku ya tatu sasa linapita lakini kwasababu majira yake yalikuwa ni mchana, muda ambao mimi sipo home, ndo’ maana sikupata kulisikia.

Basi baada ya hilo tangazo, nilikaa hapo nyumbani mpaka majira ya mchana nikatoka kwenda Goba centre kwenye mnada. Siku ya Jumamosi kulikuwa na mnada hapo na mimi nilikuwa napendelea kwenda kwasababu ya kuchukua vitu vingi vya ndani kwa bei nzuri kuliko kuchuuza kidogokidogo.

Nilienda huko nikafanya kila kilichonipeleka, wakati wa kurudi, kama kawaida, nilipofika kituo cha Kontena nilishuka na barabara ile iliyosakafiwa kuelekea nyumbani kule Mashuka. Nilipomaliza barabara hiyo nikashika njia ya vumbi, kidogo mbele, pale kwenye kile kiwanja nikakuta tayari watu wameanza kusogeasogea, hapo pamewekwa viti kadhaa vya plastiki tayari kwaajili ya kikao.

Mimi nikanyookea nyumbani kwanza kutua mizigo na kuoga kabisa, kisha nikarejea kujumuika na wale watu wa kwenye kikao. Nilikuta tayari wameshaanza.

Kuhusu ile barabara, nilichosikia kwa maneno ya mwenyekiti, ilikuwa ipo katika mpango wa kuendelea kujengwa kumaliziwa lakini changamoto iliyoibuka ni kwamba kuna baadhi ya makazi ya watu na hata pia magenge yamebana hifadhi hiyo ya barabara, haswa huko Mashuka kwa chini, na watu hao si kwamba wamevamia ama wametenda kosa, la hasha, yale ni maeneo yao kabisa kwa haki hivyo kikao kiliitwa ili pajadiliwe na ikiwezekana watu hao waombwe kutoa sehemu ndogo za maeneo yao kwaajili ya kukamilisha mradi wa barabara ile ilosakafiwa.

Kitendo cha serikali ya mtaa kukaa kimya muda mrefu bila kuiendeleza ile barabara, kuliibua minong’ono kwamba pesa iliyotengwa huenda ilishapigwa, kwasababu hiyo kikao cha kuweka mambo wazi kilikuwa ni muhimu.

Watu wakajadiliana na wakakubaliana, wengine waliokuwa wamiliki wa maeneo husika wakiwa pale, mwisho wa siku ikaadhimiwa mwenyekiti atatengeneza pendekezo rasmi na litafikishwa kwa walengwa, lakini wachache waliokuwepo pale wao waliridhia kabisa kugawa maeneo yao alimradi maendeleo yapite.

Baada ya swala hilo kumalizika mwenyekiti alitoa fursa kwa watu kuuliza ajenda zingine muhimu mbali na ile iliyojadiliwa, katika uwanja huo ndipo mjumbe akaibuka na yale ya kule korongoni juu ya namna gani watu wameligeuza kuwa dampo lisilokuwa rasmi. Mjumbe huyo alieleza kuwa korongo hilo limegeuka kuwa kero kubwa ya harufu kwenye baadhi ya maeneo kitendo ambacho ni hatarishi kwa milipuko ya magonjwa haswa kipindi cha mvua.

Swala hilo likaibua mengine, kuna wajumbe wakasimama na kuituhumu pia shule ya St. Joseph wakisema shule hiyo imekuwa ikielekezea uchafu wake wa machemba kule kwenye lile korongo. Punde chemba zao zinapojaa basi wanazifungulia kumwagia korongoni na ndo’ maana halijawahi kuonekana gari lolote la kunyonya maji machafu hapo shuleni tangu kuanza kwake kwa shughuli.

Basi swala hilo mwenyekiti akaahidi kulifanyia kazi lakini pia akapiga marufuku kwa mtu yeyote kutupa taka kule korongoni na endapo yeyote akikamatwa basi atawajibishwa. Katika kutimiza hilo, tena likijumuishwa na swala la wezi majira ya usiku wa manane ambalo kumbe lilishawahi kuongelewa kwenye vikao vya nyuma, mwenyekiti pamoja na wajumbe wakaazimia kuwe na ulinzi shirikishi katika maeneo yale japokuwa mimi mpaka naondoka kikaoni haikuelezwa wazi oparesheni hiyo itaanza rasmi lini.

Nilishika njia ya kurejea nyumbani, nikajikuta napatana na majirani wenzangu wawili wa kuongozana nao, majirani hao nao walikuwa katika kile kikao hivyo tuliongozana kwa pamoja tukiyajadili yale yaliyozungumzwa kikaoni, mwelekeo wetu ukiwa mmoja, hapo majira sasa yakiwa yanaelekea kuwa giza la saa moja.

Kufika getini tulipokelewa na sauti ya kilio cha mtoto, mtoto ambaye mimi sikumfahamu ni nani kwa sauti yake hiyo. Tuliingia ndani tukakuta wanawake wawili wakiwa wanahangaika na mtoto mmoja wa kike anayeishi humu ndani, mtoto wa kama miaka kumi hivi kwa makadirio, ambaye alikuwa analia kwa machozi mengi huku amejishika kichwa.

Mtoto huyo nilipomtazama vema, kwa upande wake ule wa pili, alikuwa anavuja damu kichwani, juu kidogo ya sikio lake la kushoto. Mkono wake ulioshika hilo jeraha ulikuwa umelowa damu vidoleni.

Kabla sijafanya jambo, nikamwona ‘wife’ anakuja kwa kasi akitokea nyumba kubwa, amevalia khanga kiunoni na kifuani, akasema: “Hamna mtu ndani, yupo yule mtoto peke yake. Nimegonga na kuita lakini kimya, mlango ameufunga kwa ndani.”

Katika maongezi yalojiri hapo nikabaini kuwa yule mtoto wa BIGI ndiye aliyemjeruhi mtoto huyo kisha akakimbilia ndani na kujifungia, lakini zaidi katika maongezi hayo nikabaini kuwa mtoto yule wa BIGI kumbe hakuwa mtoto mzima kama wengine bali ana matatizo makubwa ya akili. Hata muda huo tukiwa tunazungumza na kumpatia huduma mtoto yule aliyejeruhiwa, yeye alikuwa dirishani akitutazama. Mimi nilimwona.

Lakini zaidi ya yote, nilijikuta napoteza yale yote niliyokuwa nayajenga kwaajili ya usalama wa familia yangu … si jingine bali jambo la kutokutaka kuwahusisha kwenye lolote lile kuhusu mwenendo wa yule jirani.


***
Big kisanga anacho aisee (mke kiziwi na mtoto tahira) duh...
 
Ndugu Steve una maneno mazuri ya kiswahili na mpangilio mzuri wa kuandika story ila kuna mambo unachanganya mfano
1. Jana nilisoma kuwa mtoto wa BIG ndio kaumia leo nasoma mtoto wa jirani. Umechangajya wewe au ni mimi sijaelew


3. Jina Bembela umelitumia kwa mama n mtoto pia umemwita hivyo. .
We ndio hujaelewa rudia kusoma, hakuna mahali ameandika mtoto wa Big ndiye alieumia
 
Uzi umevamiwa na vibwengo.

Kwenye fictional literature kuna minor (secondary) character ambaye yeye yupo kusaidia main character na kusaidia kusukuma plot events forward.
For that case mke wa jamaa ni minor character ambavyo kimsingi minor character si lazima kuhusishwa/kutajwatajwa kwenye matukio ni endapo tu inabidi kumhusisha.
Ndicho anachokifanya bwana SteveMollel.
Umeshajua ana familia, period. Utaona mke wake na mtoto baadaye maana hawa ni supporting characters hawana kipaumbele kwenye matukio, kama kuhusika (kutajwa) watahusika (watatajwa) kwenye plots za muhimu tu.
Umemaliza mkuu
 
Mkuu wangu soma vizuri. Mtoto aliyeumia si wa BIGI bali mtoto wa BIGI nilimtaja kuwa alikuwa dirishani akitazama wakati tunamhudumia huyu aloumia, na mtoto huyo aloumia sijamtaja jina lake zaidi ya kumrejea kwa kutumia jina la mama yake, yaani mtoto wa Bembela.
"...Bembela yeye tofauti na wengine hakuwa na mzazi wa kumwita..."
 
Muandishi kaweka wazi kuna muda huwa anakula kwa Mama Bembela ikiwa mkewe hayupo,pia mkewe kwenye hii hadithi yetu ya kusisimua sio Mhusika mkuu.


Kwa mazingira ya hadithi yenyewe (mazingira ya nyumbani) ilivyo haiwezekani aslani kuikwepa nafasi ya mke licha ya mara kwa mara kula kwa mama Bembela, kwa maneno mengine angalisema mkewe wakati huo alikuwa na udhuru gani kiasi kwamba ashindwe kumtaja lakini wakati huo huo amtaje mke wa Bigi, sasa huoni hivi sasa kashtukia mchezo/mapungufu na kaanza kumuhusisha mkewe!!, je huko nyuma huyo mkewe alikuwa wapi??
 
Mjuaji kazini!!??
ww kula story pita vile


Wewe ni mpuuzi bali mjinga, tunapoona mapungufu lengo ni kuifanya hii hadithi ipendeze zaidi, sisi ndio wasomaji au walaji sasa tunapoona chumvi au kiungo fulani hakitoshi basi yatupasa tuemueleze mtunzi ili ajue hayo mapungufu na wakati mwingine anapoandika story ya aina hiyo akumbukee hayo mapungufu ili asiyarudia na hadithi iwe the best.

Isitoshe hadithi hajaimaliza hivyo huo unakuwa ni wakati wa kuangalia hayo mapungufu na ayafanyie kazi ili sehemu ya mwisho ya hadithi iwe nzuri.

Kwa hakika SteveMollel ni mtunzi mzuri na sidhani kama anatosheka na huo umahiri wake kiasi kwamba asihitaji kushauriwa au hata kukosolewa.
 
Kwa mazingira ya hadithi yenyewe (mazingira ya nyumbani) ilivyo haiwezekani aslani kuikwepa nafasi ya mke licha ya mara kwa mara kula kwa mama Bembela, kwa maneno mengine angalisema mkewe wakati huo alikuwa na udhuru gani kiasi kwamba ashindwe kumtaja lakini wakati huo huo amtaje mke wa Bigi, sasa huoni hivi sasa kashtukia mchezo/mapungufu na kaanza kumuhusisha mkewe!!, je huko nyuma huyo mkewe alikuwa wapi??
Wanaomtetea wanahisi wako salama, kumbe wanaharibu ladha ya simulizi.
 
Back
Top Bottom