Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Hahaaa endelea sasaAsante sana. Maana pages ni nyingi sana [emoji28]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaaa endelea sasaAsante sana. Maana pages ni nyingi sana [emoji28]
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8]
Uliomba msaada ukatukanwa?Uzii huu watu wengi wanaufatilia.lkn ingekuwa jamaa kaandika Uzi wa jambo LA maana au kuomba msaada wowote hakuna MTU angesapot zaidi ya kutukanwa na kukatiswa tamaa.wana jf tubadlike tuache kufatilia mambo ambayo pindi flni havitusaidii
Hawa wazenguaji tuachie sisi tu-deal nao. We concentrate na storyKaka, ebu naomba unionyeshe hata sehemu moja ambayo nilisema natuma story muda fulani alafu sikufanya hivyo zaidi ya jana tu? Mbona mnakuwa wasahaulifu mno? Hivi kuna mtumaji wa story humu anayejitahidi kutunza ahadi yake kama mimi?
Mnyonge mnyongeni ...
Sana tu na kukatiswa tamaaUliomba msaada ukatukanwa?
Mkuu,Ulivyoanza hii story ulituma episode 5 ndani ya sku moja ila ss hv hyo moja yenyewe had malalamiko ndio utume....sijui kwanini mnakua hvyo waleta story....maybe ndio njia ya kupata attention.....nway all the best
Tayari nishamaliza 😅Hahaaa endelea sasa
Kuwa na kazi binafsi,kulipwa au kutokulipwa haisuiani na nilichoandika unless hujanielewa nilichoandikaMkuu,
Hamjui watu wana kazi zao binafsi? Au mnawalipa kuleta story?
Nasubiri namba 8Jioni nikitoka kazi, tunaendelea.
Lucha Antonnia sophy27Yule Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 10
LILE ZOGO la BIGI na msiba lilipita kwa majuma kadhaa lakini Bembela bado hakupata kuonekana nyumbani wala mazingira yake ya kazini. Hamna aliyekuwa anajua haswa yuko wapi au anaendeleaje bali kuamini tu maneno ya yule shoga yake aliyokuwa akisema ya kwamba mwanamke huyo anamtafuta mtaalamu, lakini kufikia hapo baadae hata shoga yake mwenyewe akawa anasema hampati tena kwenye simu, amejaribu mara kadhaa pasipo mafanikio, ‘location’ yake ya mwisho alimwambia yupo huko Tanga. Basi sisi tukawa hatuna lingine la kufanya bali tu kumwombea salama.
Haikupita siku nyingi, mjumbe alikatiza katika makazi yetu akatutambulisha juu ya oparesheni ya ulinzi shirikishi ambayo inataka kuanza kama vile tulivyoazimia katika kile kikao cha siku ile. Bwana huyo alitueleza majira ya kazi ya watu hao kuwa ni kuanzia saa nne usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri, mabwana hao watakuwa wanafanya kazi kwa ‘zone’, kila mmoja atakuwa akitembea na ‘reflector’ itakayomtambulisha yeye pia na eneo lake la kazi, na zaidi akatueleza juu ya utaratibu wa kuwalipa hao mabwana ya kwamba ni shilingi alfu tatu kwa kila mlango kwa kila mwezi.
Baada ya hapo, siku na mara kadhaa, katika majira ya usiku mkubwa, nikawa nawasikia watu wakiwa wanakatizakatiza huko nje ya uzio. Watu hao wangepita wakizungumzazungumza na kuteta, kwa mtu ambaye angalikuwa macho muda huo na hivi ni majira tulivu ya usiku basi angepata kuwasikia tu, moja kwa moja nikabaini watu hao ni ulinzi shirikishi.
Basi siku moja, siku chache tu tangu ulinzi shirikishi waanze kazi, katika majira ya usiku mkubwa, nilitoka kwenda maliwato kujipatia huduma binafsi. Kama ilivyo ada nje kulikuwa kumetulia sana kiasi hata ukiburuza ndala chini sauti inaitika kweli. Niliporejea kutoka maliwato, nikiwa barazani nataka kuingia ndani, nikasikia sauti ya miguu ya mtu ikiburuza, sauti hiyo inatokea ndani koridoni, nikangoja kutazama, kidogo nikamwona mwanaume mnene ambaye kwa umbo lake tu nilimfahamu kuwa ni BIGI, mara nikasikia baridi la ajabu likikatiza mwilini mwangu kuanzia juu mpaka miguuni! Nilijikuta nasimama nisijue cha kufanya kwa sekunde kadhaa, bwana yule akakatiza kunipita, lakini kidogo nikamwona tena mke wake akiwa anafuatia kwa nyuma, mwendo wake kama mtoto anayejifunza kusogeza mguu tee-tee. Mwanamke huyo alikuwa amevalia kitu kifuani ambacho nilikitambua ni kaniki nyeusi pale aliponisogelea, kichwa chake kipo wazi, cheupe hakina hata nywele, anatembea akiwa anatazama chini.
Walinipita wakashuka ngazi kisha wakashika njia kuelekea maliwato. Mimi sikungoja nikaingia zangu ndani nikiwa najiuliza mambo mengi kuhusu wale watu, kiu yangu ya kutaka kujua kinachoendelea ikanifanya niende dirishani kutazama. Kama baada ya dakika tatu watu wale wakatoka maliwato bwana BIGI akiwa anaongoza njia, waliingia ndani pasipo kufunga geti kubwa kisha kukawa kimya.
Sikusikia tena kitu kingine mpaka napotelea usingizini, kesho yake ndipo nilikuja kupata taarifa kuwa pale koridoni na pia kibarazani palikutwa na matone matone ya damu, aliyebaini jambo hilo alikuwa ni mke wa Tarimo ambaye alidamka asubuhi ya mapema kwaajili ya kwenda hospitali kupeleka chakula cha mgonjwa wake. Mwanamke huyo alisema kwanza aliona mabaki ya damu maliwatoni, alipotoka kurejea ndani ndipo aliangaza akabaini pia damu ile ilichuruza pia mpaka kibarazani na koridoni, binafsi sikushangazwa na hilo maana kule bafuni kuna taa kali yenye mwanga wa kutosha , ni rahisi mtu kuona kitu, lakini pale kibarazani na koridoni mwanga wake ni hafifu, yawezekana damu ile ilichuruza ule usiku wake lakini mimi sikupata kuiona kwa urahisi.
Na sikuwa na shaka na hili, damu ile ilikuwa inamchuruza yule mwanamke wake BIGI. Ule mwendo wake haikuwa bure.
Baada ya tukio hilo, siku chache zilizokuja, majira ya jioni walikuja wanaume wawili wa ulinzi shirikishi, mimi sikuwapo siku hiyo lakini habari nilikuja kuipata niliporejea nyumbani. Mabwana hao walisema wamepewa taarifa na mmoja wa majirani wanaokaa kwenye zile nyumba za kule chini karibia na korongo ya kwamba kuna bwana anayekaa pale nyumbani kwetu huwa anashusha taka kule korongoni majira ya usiku. Mabwana hao walisema wanatoa onyo, kwa muda huo hawana ushahidi lakini punde watakapomkamata basi atalipa ‘fine’ na watambembesha taka hizo mgongoni mpaka hapo anapokaa, yani pale kwetu, waje kuzimwagia kiwanjani. Mabwana wale kwa akili zao walikuwa wanadhani mtu yule anayeenda kutupa taka huko huwa anazikusanya pale nyumbani kumbe wala, hamna mtu anayehusika naye.
Basi kesho yake, kama ilivyo kawaida nilienda kazini majira ya asubuhi lakini niliporejea kutoka kazini nikakuta hali si nzuri kiasi nyumbani, mke wangu alikuwa analalamika anasikia maumivu ya tumbo, haswa maeneo ya chini ya kitovu. Maumivu hayo yalimwaza majira ya jioni.
Nilimtaka twende hospitali lakini alikuwa mbishi, huwa ni kawaida yake kuwa mbishi kwenda hospitali, alichoniambia ni kawaida kwa mjamzito kuhisi maumivu ya tumbo hivyo baada ya muda atapoa tu, nikaingia mkenge kuamini, kweli kuna muda tumbo lile likapoa akasema anahisi unafuu ila shughuli kamili ikanijia usiku mkubwa. Mwanamkea yule hakulala kabisa, ni anagugumia tu kama paka anayekata roho, anageukia huku na kule, tumbo tumbo na huku anavuja damu, nikaona hapa mambo yashakuwa makubwa, upesi nikamwendea jirani yangu, Mama Tarimo, kumwomba akae na mtoto wangu ili mimi nipate kuwahi hospitali, mama huyo kwa huruma akampokea mtoto lakini akanishauri tuelekee wote hospitali maana mgonjwa hatoweza kukaa mwenyewe kwenye pikipiki, nikaona ni vema.
Alimwacha mtoto wangu kwa mtoto wake mkubwa alokuwapo ndani kisha akajiandaa upesi tupate kuondoka. Mimi niliingia ndani nikanyakua suruali na kiasi fulani cha pesa, kama alfu sitini, kisha nikaungana naye, nikawapakia wanawake hao moja kwa moja mpaka hospitali ya Massana. Huko tulipokelewa na wahusika, na wa hali aliyokuwa nayo mgonjwa alipelekwa moja kwa moja kupata huduma ya dharura, akiwa hapo anahudumiwa mimi nikatakiwa niende kufuata mchakato wa malipo pale mapokezi na kisha kwa ‘cashier’.
Nilifika mapokezi nikaulizwa kama mgonjwa ndo’ mara ya kwanza kuhudumiwa hapo, nilipojibu ndio akanitaka nifungue kwanza faili jipya, gharama yake ni alfu kumi, nikamwambia sawa fungua maana kusema nimkimbize mwanamke yule mpaka Lugalo ilikuwa uongo, hali ile ya dharura haikuniruhusu. Lakini ajabu nilipozama mfukoni kuchukua pesa sikuona kitu! Nilipapasa kila mfuko lakini sikuambulia kitu, kila mfuko ulikuwa mweupe, nilichoambulia katika mfuko mmoja ni shilingi hamsini tu! Kweli nikachanganyikiwa.
Ile pesa yote niloweka mfukoni kule nyumbani ipo wapi? Nilibaki nikitoa macho, natazama huku na kule kama fala. Kwenye simu pesa ni ya vocha tu, hamna cha maana. Kidogo nikampigia jamaa yangu wa kazini apate kunisaidia kwa dharura lakini naye simu haikuwa inapatikana, nikicheki muda umeenda kwelikweli, nikahisi kichwa kinawaka moto. Siku hiyo ndo’ nilijifunza maana ya bima ni nini? Bima niliyokuwa nayo ilikuwa ni ya mtoto tu.
Nilichoamua kufanya nilitoka pale hospitali pamoja na Mama Tarimo kuelekea nyumbani. Nilimrejesha mama yule kisha mimi nikaenda kusaka pesa nyingine chumbani, nilikuwa naweka akiba katika droo ya kitanda, hapo nikapata alfu kumi na tano, hiyohiyo nikaikwapua lakini nikasita kuiweka mfukoni, niliogopa kunitokea kama yale ya mwanzoni, nilichofanya nilivua ile suruali ambayo sikuiamini tena nikavaa nyingine kisha nikatoka nje. Pesa yangu sikuiweka mfukoni, niliamua kuishikilia tu mkononi. Pesa hiyo ilikuwa ni mahususi kwaajili ya kufungulia faili la mgonjwa alafu pakikucha nitajua cha kufanya, niliamini sitashindwa kupata pesa ya ‘bill’.
Nilifungua geti nikatoka nje ya uzio, nikapaki pikipiki na kulirejea geti lile ili nipate kulirudishia lakini kabla sijalifunga geti hilo nikasikia watu wanaongea wakiwa wanatokea kule korongoni, nikatulia kidogo kutazama, punde nikawaona wanaume wawili kwa mbali kidogo wakiwa wanaburuza kitu, wanakuja mwelekeo wangu. Wanaume hao walikuwa wanang’aa kwa ‘reflector’ zao nikawatambua ni ulinzi shirikishi. Kidogo nikasikia mtu anafungua mlango wa grill, kutazama alikuwa ni mtoto wa Mama Tarimo, yule mtoto ambaye tulimwachia mtoto wangu mara ya kwanza wakati tunaenda hospitali. Mtoto huyo alikuwa amebebelea kopo bila shaka anaenda chooni.
Kugeuka hivi nikakutana na tochi kali mno ya wale ulinzi shirikishi. Mabwana wale wakiwa huko huko walipaza sauti yao, “Wewe unafanya nini hapoo?” sikuwajibu. Nikawasikia wanasema sio huyu anayepeleka taka korongoni? Anafanya nini pale? Ngoja atatueleza.
Waliposogea kidogo nikaona kumbe walichokuwa wanaburuza mabwana wale kilikuwa ni kiroba. Sikujua kile kiroba walikitoa wapi lakini nilihisi kabisa ni kule korongoni walipotokea, sikujua kiroba kile kina nini ndani lakini zaidi nilichokuwa najiuliza ni kwanini walikuwa wanakileta huu upande wetu?
Walinifikia wakaniuliza maswali nami nikawajibu, uzuri yule mtoto wa Mama Tarimo alikuwamo kwa ndani anasikia kila kitu, akapaza kusema huyo ni baba fulani amekuja na mama muda si mrefu.
Bwana mmoja akasema, “tumemwona mtu anatupa hizi taka kule korongoni. Sasa tumewaletea uchafu wenu hapa tuwamwagie tuone kama mtapenda kuishi nao! La sivyo mtulipe faini.”
Mimi nikawauliza, “huyo bwana mliyemwona ni nani? Na mna uhakika gani anakaa hapa?”
Wakanambia walishapewa taarifa na watu kumhusu bwana huyo, hata hivyo siku hiyo almanusura wangemkamata lakini aliwapotea machoni, nikaona watu hawa wataniweka na mimi nina mambo yangu muhimu ya kufanya, nikawaaga nikaondoka zangu kwenda hospitali kuhangaika na mambo yangu binafsi.
Nilikuwa huko hospitali mpaka majira ya asubuhi ya saa mbili niliporejea tena nyumbani. Siku hiyo sikwenda kazini kwani nilikuwa nimechoka mno. Nilipohakikisha nimepata pesa na hali ya ‘wife’ haikuwa mbaya sana niliona ni kheri niende nyumbani mara moja kupumzika, hospitali nikamwacha mama yangu mzazi ambaye alikuja na chakula asubuhi ya mapema.
Nilipofika nyumbani getini nikastaajabu kukuta kifusi cha taka pembezoni mwa geti. Kifusi hicho kilikuwa na nguo kadhaa zenye damu, nywele na matakataka mengine ambayo sikuyaelewa, yanayotoa harufu ambayo sijawahi kuisikia.
Cha ajabu katika takataka hizo nilipata kuona nguo za mwanangu! Nikakumbuka kipindi kile ‘wife’ alivyoniambia kuna nguo zilipotea kambani, ina maana ndo’ zile? … Kilichonichanganya zaidi na kunitia wazimu ni pale nilipokuja kuambiwa katika taka hizo kulikuwapo pia na nguo za mtoto wa Bembela, yule mtoto marehemu, maneno hayo aliyasema yule shoga yake Bembela kwa kinywa chake, nikaona hii sasa balaa.
“Nakwambia baba fulani, yule mbaba ni mchawi!” aliniambia akinong’ona. Macho ameyatoa.
Kweli nikashindwa kuvumilia, upesi nikauendea mlango wa BIGI na kugonga.
Asante sana mamy!!😘
Hahhaha tukutane episode inayofuataTayari nishamaliza [emoji28]
Sawa mkuu!Kuwa na kazi binafsi,kulipwa au kutokulipwa haisuiani na nilichoandika unless hujanielewa nilichoandika
Wamemletea mazaga yake ghetto toka korongoni ila mkuu SteveMollel hivi hayo maviroba huwa hayatoi harufu yakiwa chumbani kwa BIGBIG kayakanyaga