Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida - Night Shift.

NILIGONGA mlango kwa kama sekunde kumi hivi, kimya, hamna mtu aliyeongea ndani wala kuja kuufungua, nikagonga tena na tena na tena. Nilihakikisha nimetumia dakika kadhaa hapo lakini bado sikufanikiwa, hakuna aliyethubutu kufungua mlango ule, basi nikasema:

"Nataka tuongee,nina shida na wewe!"

Kwa muda huo nimeparwa na jazba. Damu inapita kwa kasi kweli mwilini,jasho linanichuruza. Yani naona kama nakawia kumwona bwana yule. Kichwani mwangu nawaza, sipati raha, kwanini nguo ya mwanangu aliichukua kuifanyia mambo yake? Anataka kumuua kama yule mtoto wa Bembela? Nikagonga nikiongea na mlango mwenyewe kama mwehu. Nilipoona nimefanya kila jitihada ya kugonga mlango na nimegonga mwamba, akili yangu ikanituma nitengue kitasa cha mlango ule.

Nikafanya hivyo ...

Kikweli sikutegemea kama mlango ule utafunguka, mimi nilichokuwa nimedhamiria ni kumshtua mtu alokuwemo ndani kama kweli yumo humo ili aitikie haja yangu ya kuja nje, ila hamaki mlango ukafunguka!

Uliachama mwanya mdogo nikapata kuona kwa kiasi chake yale yalokuwemo ndani japo si kwa ukamilifu kwasababu sebule ile ilikuwa na mwanga hafifu sana, madirisha yamefungwa,yani kama si mwanga mchache uloingia ndani sababu ya mimi kuufungua ule mlango, sidhani kama ningeshuhudia jambo lolote humo ...

Basi kwa macho yangu ya nyama, pale chini sakafuni, niliona miguu ya watu wawili ambao niliamini wamejilaza: miguu miwili ilikuwa ni ya mtu mzima na miwili ni ya mtoto! Miguu hiyo imetulia tuli wala haikutikisika pamoja na mimi kuufungua mlango kutazama.

Upesi nikaurejeshea mlango huo kama nilivyokuta, moyo wangu unanienda mbio, nikaondoka hapo kwa haraka kwenda kwa Mama Tarimo kwa madhumuni mawili: moja kumpa taarifa ya maendeleo ya mgonjwa ambaye tulimpeleka naye hospitali hapo awali na pili nimwone mwanangu ambaye nilimwacha hapo.

Dhumuni la kwanza likatimia lakini la pili halikutimia kiukamilifu kwani mtoto alikuwa amelala na mimi sikuona haya ya kumsumbua, nikaelekea kwenye makazi yangu ambapo nilifikia sebuleni kwenye kochi nikaketi hapo nikiyatafakari yale niliyoyaona kwenye ile sebule ya BIGI na pia yale mengine niliyoelezwa na Mama Tarimo.

Mama huyo, kama alivyofanya shoga yake Bembela, alinieleza yale yalosibu pale nyumbani nikiwa hospitali, akienda mbali kwa kusema Mjumbe alifika pale nyumbani kuhusu lile swala la taka korongoni, mjumbe huyo alikuwa ameshapewa taarifa na wale watu wa ulinzi shirikishi asubuhi ya mapema walipoenda kwake kukabidhi lindo hivyo alikuja kwa minajili ya kutujuza kuwa tumepigwa faini, kitu ambacho mimi kwakweli sikukubaliana nacho hata kidogo na sikuwa tayari kutoa hata sent'ano.

Nikiwa nayatafakari hayo, kwasababu ya uchovu wangu nilioulimbikiza toka usiku ule, nikajikuta nalala hapo fofofo bila kubadili chochote mwilini. Nilikuja kukurupuka baadae baada ya kusikia mtu akigonga mlango, kutazama simu ni majira ya saa nane ya mchana, niliufungua mlango nikamkuta shoga yake Bembela akiwa ameegamia ukuta mkononi ameshikilia simu.

Alinisalimu, "Habari za saa hizi, shemeji?"

Nikamwitikia salamu yake na kumkaribisha ndani, akasema hapana haina haja, amekuja hapo kwa dharura tu.

"Bembela anataka kuongea na wewe," alisema akinipatia simu yake alafu akaongezea, "atapiga muda si mrefu, nitakuja kuichukua simu yangu." Kisha akaenda zake, mimi nikaingia ndani na kweli si muda simu ile ikaita nikapokea. Kusikia tu sauti nikajua ninayeongea naye ni Bembela.

Alinisalimu tukajuliana hali kisha akanieleza kuwa kesho yake atakuwa njiani kuja Dar akitokea Tanga.

Aliniambia amepata habari zote zilizotokea nyumbani maana shoga yake ameshamweleza alivyompigia simu majira ya asubuhi, lakini pia akanieleza juu ya hofu yake kwangu kuhusu zile nguo za mwanangu kuonekana katika kile kiroba ambacho yeye aliamini kabisa kuwa ni cha bwana BIGI.

Alisema, "Baba fulani, nguo za mwananangu zilipotea hivyohivyo katika mazingira ya kutatanisha hata kabla ya kifo chake, na kufa kwake hakukuwa na mahusiano kabisa na ugomvi ulotokana na mwanaye huyo BIGI bali hiyo ndo' kanuni yake ya kuua, hammalizi mtu mpaka pale mjumbe anayemtumia atakapopata sababu ya kufanya hivyo, na atakapoipata sababu hiyo basi huitumia hiyohiyo kwenye maangamizi yake."

Hapo ndo nikakumbuka yale maneno ya Bembela kwenye mlango wa BIGI, namna mwanamke huyo alivyokuwa anapiga kelele siku ile akiwa amemshika mwanaye pale koridoni akisema familia ya BIGI itoke kuendelea kumpiga mtoto wake, na kweli ikawa hivyo mpaka kifo cha mtoto yule!

Lakini zaidi nikakumbuka ndoto alizokuwa anaota mke wangu na kukurupuka nyakati za usiku: Ndoto za mtu kugonga mlangoni, mtu ambaye ana sauti ileile kama ya kwake, hapo ndipo nikafahamu kuwa jambo lile ni kwasababu ya yeye kuugonga ule mlango wa BIGI akimwita mtoto yule au yeyote aliyemo ndani baada ya huyo mtoto chizi kusababisha kadhia ya kumpiga mtoto wa Bembela.

Kumbe kwasababu hiyo, mjumbe wa mauaji anayetumiwa na BIGI aliutumia huo mwanya kumbishia hodi za kutisha mara nenda rudi kwenye ndoto zake, majira ya usiku mkubwa, mpaka pale alipoondoka na uhai wa kiumbe kilichokuwa tumboni mwake!

Bembela alinieleza kwenye simu, bwana huyo hawezi kumuua mtu kama hatokuwa na kitu binafsi cha mhanga wake, kwahiyo mbali na zile nguo za mwanangu nilizoziona pale nje, asingeweza kuangamiza kiumbe ambacho kipo tumboni mwa mke wangu kama asingekuwa na mali binafsi ya mke wangu.

Nikajihisi kuelemewa na maneno hayo. Kuna muda aliongea lakini sikumwelewa tena maana nilifurikwa na mawazo lukuki kichwani.

Kwanza huyo mjumbe wa BIGI ni nani? Je, ni yule mkewe? Kama ndio, atakuwa ni mjumbe wa aina gani huyo ambaye niliwahi kumpeleka hospitali alipozidiwa?

Nikamweleza Bembela kuhusu mwanamke huyo na safari yetu ya kwenda zahanati siku ile, namna nilivyokuwa nahisi karibu naye na pia yale yalotokea kule zahanati, akanichosha kabisa kwa majibu yake ...

Bembela aliniambia,

"Basi huyo ndo' mjumbe wake, na siku hiyo sikumpakiza mtu bali nilimpakiza kiumbe kilichokuwa kinaenda kutafuta damu na pumzi za wagonjwa, mimi pale nilitumika kama daraja tu. Na usiku huo lazima kuna watu ambao waliondolewa roho zao kule kwenye nyumba ya matibabu."

Hapo nikamkumbuka yule bibi kule zahanati binafsi ya kawe na yale maneno yake.

Lakini zaidi, tumbo liliniuma nilipokumbuka kuwa hata mimi siku hiyo nilienda kugonga na kufoka mlangoni mwa BIGI nikimtaka bwana huyo atoke nisemezane naye, tena kama haitoshi mwanamke yule ambaye nimeambiwa ni mjumbe akiwa ndani amejilaza.

Je, nitakuwa salama?

Bembela aliniaga akiniahidi akifika Dar tutayajenga zaidi na kwa kushirikiana tutamkabili bwana huyo kwa ukamilifu, dawa amekwishaipata, mimi nikamuaga na kukata simu lakini siku ile nzima nikawa naendelea kuyasikia yale maneno yote aloniambia kana kwamba ni kanda ya muziki inayojirudia!

Nilifanya ratiba yangu kama kawaida, kwenda hospitali na kupita baadhi ya mahali kwa mambo yangu binafsi, usiku nikarejea nyumbani nilipoungana na mwanangu kwaajili ya chakula na mapumziko.

Muda wote huo mpaka naenda kulala, usiku wa saa nane, sikuona alama wala viashiria vyovyote vya uwepo wa bwana BIGI, achilia mbali na kwamba yeye mwenyewe sikumwona, lakini hata taa ya makazi yake haikuwashwa kabisa.

Ajabu ni kwamba, majira ya usiku wa saa tisa, kwa mujibu wa saa ya simu yangu, nilikurupuka kusikia mtu anagonga mlangoni. Kabla sijajigusa, nikasikia mtu huyo akisema, "nataka tuongee, nina shida na wewe."

Vilevile kama nilivyosema mimi muda ule malangoni mwa BIGI!
Hiiii.. mbona nimeanza kuogopa sasa [emoji33]
 
Izzyhass
 
Back
Top Bottom