Jisifu Kwa kitu ambacho unacho, vinginevyo tunakuona hamnazo!

Jisifu Kwa kitu ambacho unacho, vinginevyo tunakuona hamnazo!

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
JISIFU KWA KITU AMBACHO UNACHO, VINGINEVYO TUNAKUONA HAMNAZO!

Anaandika, Robert Heriel.

Angalizo; Kama ni mtu wa makasiriko usisome andiko hili.

Oooh! Wahaya Sisi tumesoma Sana! Wewe umesoma? Mtu huna elimu, madarasa hayatoshi alafu kutwa kupiga kelele. Unajivunia elimu ya watu wengine alafu wewe huna, huo Kama sio upunguani ni nini.

Taikon watu wa hivi huwaga wakikutana na Mimi lazima wanichukie, Kazi yao kuwafanya watu wa makabila wengine wajione Duni kwao.

Ooh! Sisi Wachaga tunajua kutafuta Pesa, sijui tumeendelea, upuuzi mtupu! Mtu anayesema maneno hayo ukimtazama Hana mbele wala nyuma, pesa hana anajisifu Kwa vitu vya wengine Kama mtoto mdogo.
Huna nyumba, huna Gari, huna kipato cha uhakika lakini unatumia ndugu zako kujitutumua😀 Kama sio uchizi huo ni nini?

Ooh! Sijui Wambulu Malaya, sijui Wanyaturu Maji ya Mbeya, utafikiri Dada zako waliolewa wakiwa na Bikra, tena unayeongea hayo na kukandia wanawake WA makabila mengine sio ajabu Ukoo wako wanawake karibia wote ni wahuni wahuni tu. Hata mke uliyemuoa sio ajabu hukumkuta Bikra na sio ajabu watoto wengine sio wakwako. KAZI Kupika maneno.

Oooh! Kule kwetu sijui Kaskazini tuna maendeleo, sijui umeme na nyumba zote za umeme, alafu anayeongea hapo Wazazi wake wanaishi kwenye nyumba mbavu za mbwa, nyumba haina umeme Ila anasema nyumba za watu wengine. Upuuzi upuuzi tu!

Ukijisifu uwe na vigezo hata watu watakuunga Mkono lakini kujisifu kitu ambacho hauna ni kujichoresha na kujidharaulisha. Wengi wanatumia mbinu hiyo ku-boost self-esteem Yao kutokana na kutokujiamini.

Oooh! Wanaume wa Dar sijui legelege, sijui hawana nguvu za kiume, huku mkoani tunanguvu na marijali. Anayesema hivyo akienda Kwa mkewe kila siku ni kuomba Msamaha Kwa kushindwa Kazi.

Tuacheni tabia za kujikweza Kwa vitu tusivyokuwa navyo, tuacheni tabia ya kujiona Bora hata kama Mungu alituunba Kwa namna nzuri kushinda wengine.

Oooh! Kwetu tunawanawake wazuri, sijui vianamke vya Kule vibaya, sijui vifupi na blah! Blah! Huko ni kutokujiamini. Mara nyingi watu wenye kujikweza na wenye Dharau hawajiamini na wanaogopa kushindwa.

Unadharau watu wa kabila fulani ilhali kwenye hilohilo kabila kuna watu wanaokuzidi mara elfu Kwa karibu kila kitu. Sio uzuri, sio pesa, sio elimu, sio akili, sio watoto wazuri, sio mke/mume mzuri, hujiona Kama unamatatizo ya Akili?

Ukipewa baraka, zitumie Kwa unyenyekevu na kuwasaidia wengine. Ukiumbwa mzuri utumie uzuri wako kuijenga jamii yako na sio kunyanyasa viumbe wengine WA Mungu. Ukizaliwa kwenye Koo au kabila lenye nguvu usitumie Jambo Hilo Kama kigezo cha kuwatesa wengine.

Ukipewa Akili na maarifa usiyatumie vibaya kuonea viumbe wengine.

Kusoma kwako kusikufanye ujione unastahili maisha mazuri kuliko ambaye hajasoma, utakwama! Nakuhakikishia utakwama na maisha yatakushangaza Kwa namna usiyotarajia.

Be humble, life is for all and everyone deserves the best.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umesahau ya wiki hii: Ooh! kanisa lenu linafungisha ndoa wanzinzi tena wana mimba kubwa kabisa. Sisi kanisa letu haliwezi kufanya huu upuuzi, wakati yeye ndo mzinzi katia mimba watoto wa watu na kakataa mimba zake au kama ni mdada katoa mimba kadhaa na ukute mchungaji wake anakula kondoo.
 
Taikon ilitakiwa upewe kazi kwenye ofisi ya mchapaji wa Serekali kama ungeikubali lakini!!.
 
Back
Top Bottom