MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kwanza kabisa ninampongeza Waziri wa Kilimo Bashe kwa kuguswa na kijana wa kitanzania anayefanya kilimo cha kitunguu na kutaka kumsaidia. Ubarikiwe sana Bashe. Vijana kama hawa wanahitaji kusaidiwa sana mitaji.
Ila nimesikitika kijana kushindwa kujua nahitaji nini hasa ili kilimo chake kipige hatua. Hajui anahitaji hata Tsh ngapi kutatua changamoto alizo nazo. Hajui bei ya tools za kumwagilia shambani. Kimsingi kijana anatumia nguvu nyingi sana kwenye kazi yake huku akiwa hafanyi tathmini ya kila siku kubaini nini kinahitajika kwa haraka. Kwa kumtazama pia naweza kusema huyu kijana sio kosa lake labda alipaniki kuona viongozi wakubwa wamefanya ziara shambani kwake au hajawahi pita chuo akafanya hata presentations.
Huyu kijana ni mfano wa vijana wengi sana wanaolia hawana mitaji ila wakiulizwa ghafla wanataka Tsh ngapi kama mtaji hawawezi jibu kwasababu hawajui. Ni tatizo la vijana kutotumia muda vizuri kujifunza kwa undani vitu wanavyotaka kufanya ili kujua gharama zake na kuweka strategic plans za kufanya kufikia ndoto zao. Kijana ukiwa muuza nguo, muuza chakula au mkulima usibweteke. Jifunze kila siku biashara yako inahitaji nini ili ikitokea msamaria kama Bashe kakuuliza unataka Tsh ngapi mtaji unamjibu hapohapp bila kupepesa macho.
Hili tatizo limesababisha vijana wengi kupoteza mitaji waliyosaidiwa au kukopeshwa. Hata wale wanaosumbuliwa na kausha damu wengi wao walichukua mikopo kabla ya kuwa na mpango mzima wa kujua atautumiaje ili asikwame marejesho. Kuna mmoja namjua alitaka sana mtaji wa milioni 12 anunue hiace afanye daladala. Siku kapata mkopo kaona biashara ya mahindi ni nzuri akaenda kununua mahindi na kuyauza sehemu ambayo huwa wanalipa baada ya siku kadhaa kama sio wiki. Bahati mbaya leo imeshapita wiki 3 anazungushwa kulipwa. Kwa jicho la haraka unaweza kuona kijana ni mjanja ila naona ni mpuuzi kwa sababu ya kuacha lengo kuu la kuchukua mkopo.
View: https://www.instagram.com/reel/DAE0k7lNoRZ/?igsh=bWRtY2EwejRlampk