Jitahidi usizoee jambo hili utaabika. Nimejilaumu sana

Jitahidi usizoee jambo hili utaabika. Nimejilaumu sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mazoea hujenga tabia.Kwa sisi wengine toka tunakua tulizoea sana choo cha kukaa. Tulipoenda shule angalau tukajifunza mambo mapya.

Nimemaliza chuo miaka ming ago, from there nimekuwa nikitumia nyumba zenye vyoo vya kukaa kama utotoni.

Leo nimekutana na changamoto ya kutumia choo cha kuchuchumaa. Miaka yote sijawahi kwenda haja kubwa nikiwa kazini.

Leo nimeenda. Kiukweli nimeteseka sana. Kuchuchumaa ni shida. Miguu inauma. Imebidi nitoe nguo za chini zote maana nlikuwa na wasiwasi zaweza chafuka.

Shida zaidi ikaja wakati wa kutawadha/tawaza. Mkono ulikuwa hauwezi kufika vizuri. Nimetumia dakila zaidi ya 8 kwa kitendo ambacho wenzangu wanatumia sekunde kadhaa.

Mpaka nimetoka siamini kama nimeswafika vizuri. Ilinibidi tu niondoke ofisini kurudi home. Mapaja yanauma kwa kuwa sijawahi chuchumaa kwa muda mrefu.

Sasa nimejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi ya kuchuchumaa.just in case nakutana tena na dhahma kama hiyo. Binafsi napenda chumbani kwangu niwe natumia choo cha kukaa na sipendi kujisaidia kwa watu.

Lakini nimegundua now i have to be ready kwa kila jambo. Mazoea hujenga tabia.
 
Nimekusoma mambo mawili matatu:
1. Wewe ni mtoto pekee home yaani toto la maza
2. Wewe ni mtoto wa fisadi ambaye hajakamatwa na sijui kwanini Taakukuu hawajakumulika
3. Huwa hujitawazi ila ni leo tu umejitawaza huwa unasaidiwa kutawaza
 
Back
Top Bottom