Vvan12
New Member
- Mar 17, 2021
- 2
- 3
TEKNOLOJIA- SILAHA KALI YA ULIMWENGU MAMBOLEO.
Ni ukweli usio fichika kwamba karne ya ishirini na moja imeshuhudia mabadiliko makubwa sana katika ukuaji wa teknlojia duniani. Sekta kama viwanda,kilimo na ata sekta za huduma kwa jamii kama hospitali na elimu zimenufaika na mageuzi haya ya technologia.
Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia technologia mpya kama akili mnemba (artificial intelligence-AI) ambayo kwayo kumefanikisha na kurahisisha mambo mengi sana ambayo yamekua yakiitaji ushirikishaji wa mojakwamoja wa akili ya mwanadamu, Ila kwa kugundulika kwa teknologia hii kumepelekea uhitaji wa binadamu kuhusishwa katika maamuzi mengi katika Nyanja tofauti kupungua
Nchi za ulimwengu wa kwanza kama Marekani ,Uchina ,Japani Na nchi nyingi za umoja wa ulaya zimekua kinara katika kufanikisha uvumbuzi na uanzishwaji wa technolojia mbalimbali na zimekua ziki huisha teknolojia izo katika sekta zake za ulinzi na usalama, viwanda , biashara n.k
Kwa kufanya ivyo kumezipa uzoefu na nguvu za kiuchumi na kisiasa ambapo dunia imeshuhudia nchi izo zikifanya maamuzi juu ya nchi nyingine husasani juu ya nchi zinazo endelea (Nchi za ulimwengu wa tatu) kama Tanzania na nyingine nyingi dunia.
Uvumbuzi na uzalishaji wa teknolojia mpya katika nchi za ulimwengu wa kwanza kumezisaidia nchi hizi na kuzipa nguvu katika mambo mengi ya kitaifa na kimataifa.
Hata ivyo ni nchi chache tu zinazo weza kutekeleza uvumbuzi na uzalishaji wa teknolojia izo mpya ambazo nchi nyingi duniani zimekua ziki nufaika nazo ikiwemo chi ya Tanzania.
Kwa sababu iyo mamlaka za kiserikali za nchi zinazoendelea kama Tanzania zione umuhimu wa kutunga sera zitakazo chochea ushiriki katika uvumbuzi na uzalishaji wa teknolojia mpya katika nchi husika.
NCHI KUA NA MPANGO MKAKATI WA KUJIIMARISHA KATIKA TEHAMA KUKABIRIANA NA VITA YA KIUCHUMI KATI YA MATAIFA.
Karne ya ishirini na moja (miaka ya 2010 mpaka wakati huu) pia imeshuhudia mataifa ya magharibi na uchina yakitumbukia katika vita ya kiuchumi kwa kutumia mifumo ya Tehama kufanya udukuzi wa taarifa za sili za selikali,watu binafsi na makampuni za nchi hizo uku Kila nchi ikifanya ivyo kwa lengo la kua mbele ya mpinzani wake kiuchumi na kimamlaka juu ya mataifa madogo.
Picha chanzo : What Are the Long-term Costs of the China-U.S. Trade War?
Hali hii tunayo ishuhudia sasa ikiendelea baina ya mataifa hayo haitupi uhakika kwamba vita hii itabaki baina ya nchi izo pasipo mbinu hizo kutumika na nchi nyingine dhidi ya nchi yetu Tanzania. Tanzania kama taifa linalokua kwa kiuchumi linapaswa kujidhatiti katika kuhakikisha linajipanga ipasavyo inapokuja maswala kama haya kwa kujikita katika kuwekeza kwenye uzalishaji wa teknolojia za ndani ili kukabiliana na mambo ya namna hii kutoka kwa majirani zake.
Ni salama zaidi kama Tanzania itawekeza nguvu kubwa kukuza teknolojia zake za ndani wakati huu mapema ili kujianda kukabiliana na changamoto za ushindani nyakati zijazo kwani kutegemea mifumo na teknolojia kutoka mataifa mengine kunaleta athari kubwa kijamii,kiuchumi na kiusalama kwa Taifa.
ULINZI NA USALAMA WA MIFUMO NA VIFAA VINAVYO TUMIKA SELIKALINI NA KWENYE TAASISI NYINGINE NCHINI.
Kuna sababu za kutosha kwa Tanzania kuanza utekelezaji wa kubuni mifumo endeshi ya Tehama (softwares) inayotumika katika vifaa vya Tehama katika baadhi ya idara nyeti kwa maslai mapana ya usalama wa taifa. Nchi yetu imekua ikitegemea mifumo endeshi (softwares)zinazo milikiwa na kampuni za nje ya nchi, tangu tupate uhuru mwaka 1961 mifumo iyo ya Tehama inatumika selikalini na katika maeneo mbalimbali nchini. Hali hii inahatarisha usalama wa taifa na ustawi wake kwaujumla kwani taarifa nyingi juu ya ustawi wa taifa zinaishia mikononi mwa makampuni yaliyoko nje ya nchi.
Katika ulimwengu wa sasa taarifa ni nguvu, na taarifa zinazo tunzwa na baadhi ya Taasisi katika kanzidata zake ni taarifa zilizo beba maslahi kwa taifa ivyo zinapaswa kulindwa. Nchi moja (yenye ulinzi katika mifumo ya Tehama) inapokua na taarifa za kutosha juu ya nchi nyingine ambayo haina uwezo wa kulinda taarifa za mifumo yeke ya Tehama , basi kunaipa nchi iyo (yenye ulinzi katika mifumo ya Tehama ) nguvu za kufanya maamuzi mabaya juu ya nchi husika masalani kuchochea migogoro ya kisiasa, kueneza propaganda na hata kudhibiti mifumo ya kibiashara ya nchi iyo.
Baadhi ya sekta zinazo itaji mageuzi ya haraka ya mifumo endeshi ya Tehama ni Pamoja na mifumo ya vyombo vya ulinzi na usalama, mifumo yote ya mapato, mifumo ya kutuma ujumbe wa maandishi (barua pepe), mifumo ya mashirika ya bima (yote) na mifuko ya hifadhi za jamii. Kama tukitekeleza mambo haya sasa, baada ya miaka kumi ijayo tutakua mbele ya nchi washindani wetu (Hususani majirani zetu Kenya).
UCHOCHEAJI NA UHAMASISHAJI WA WAVUMBUZI WA MIFUMO YA TEHAMA NA TEKNOLOJIA NYINGINE KWA MASLAHI YA TAIFA.
Taifa letu limebarikiwa kua na rasilimali watu ya kutosha ambapo takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonyesha asilimia 34 ya watanzania ni vijana, ambao ni nguvu kazi ya taifa. Kwa bahati hii ya kipeke, ni wakati sasa serikali kuwekeza katika kundi hili haraka katika sekta ya Tehama ilikuzalisha vijana ambao watakuja kua wataalamu tegemezi wa kubuni na kulinda mifumo yote ya Tehama ya nchi hii siku za usoni.
Picha chanzo: National Bureau of Statistics - Sensa 2022
Ziko mbinu nyingi sana za kufanikisha lengo hili, moja wapo ikiwa ni Pamoja na kuchagua na kusomesha kundi la vijana wachache katika vyuo bobezi kwenye nchi ambazo zinaongoza kwa technolojia duniani, hususani nchi za mashariki ya mbali (hususani urusi,china na Malaysia), nchi za magharibi Pamoja na nchi za jumuiya ya umoja wa ulaya. Kwa kua na mpango mkakati thabiti wa kusimamia kundi hili, utawezesha Kurejea nchini kwa kundi hilo la vijana ambao watakua msaada mkubwa siku za usoni katika kwendeleza maandalizi ya makundi mengine ya vijana kwenye secta iyo ya Tehama hapa nchini Pamoja na kuanza kutumika kuisaidia serikali katika kutatua matatizo mbalimbali ya upungufu ,uanzishwaji na ulinzi wa mifumo ya Tehama hapa nchini kwa maslai mapana ya Taifa.
ATUA MOJA UZAA NYINGINE, TUTEKELEZE WAKATI NI SASA.
Serikali kwa sasa imejikita katika kufanikisha malengo ya kuvutia uwekezaji na kuchochea ujio wa wageni nchini Pamoja na mauzo ya bidhaa nje ya nchi ili taifa liweze kupata fedha za kigeni. Katika uwanda huu, nchi ili iweze kufanikisha malengo yake inapaswa kuimarisha Sekta ya Tehama kwani tumeshuhudia wawekezaji wengi na wageni wengi wanaokuja nchini huja kuwekeza katka secta ambazo haziitaji matumizi makubwa sana ya teknologia kwani bado nchi iko nyuma sana katka swala zima la Tehama.
Wageni wengine wanaotembelea nchi yetu ni watalii ambao hufata sekta hii ya huduma ambayo pia haitegemei sana teknolojia. Pamoja na kwamba sekta hii inawezesha ukukusanyaji wa fedha za kigeni, bado sekta ya Tehama inaonyesha matumaini yakua na michango mkubwa sana katika kufanikisha malengo haya ya serikali kwa ufanisi wa juu siku za usoni.
Fikiria kama nchi ingekuana wataalamu wa Tehama wenye uwezo wa kutosha kuweza kuwavutia wawekezaji wa nje kusimika viwanda hapa nchini ili kuzalisha bidhaa za kidijitali kama Simu, Runinga, Pannel za sola,Magari,Silaa za kivita, n.k. kuzalishwa kwa bidhaa izi apa nchini kungeongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi ivyo kupelekea upatikanaji wakutosha wa fedha za kigeni na kukuza Uchumi wa taifa.
Ni wakati sasa serikali na mamlaka za kiserikali kutunga sera rafiki za mawasiliano (Tehama),Sera rafiki za uwekezaji, Sera rafiki za elimu na uwezeshaji wa vipaji kwa vijana ,Sera rafiki za utambuzi na uwezeshi wa vijana chipukizi katika Maswala yoote ya Tehama na uvumbuzi wa Teknolojia ili kuweza kulifikisha Taifa mahala ambapo litaweza kushindana na mataifa mengine duniani siku za usoni.
Kitu kikubwa ambacho Taifa litanufaika nacho katika mpango mkakati huu wa kukuza Tehama ni kua na Teknolojia ya asili na inayomilikiwa na Tanzania au watanzania ambayo kayo kutalipa nguvu na kujiamini Taifa pale inapokuja maswala ya vita vya kiuchumi kati ya yetu na nchi nyingine siku zijazo kwani nyakati izo huusisha vikwazo ambavyo huzuia bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi kuingizwa nchini ivyo kuzorotesha Taifa.

Upvote
4