Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JITIHADA ZA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA JIMBO LA IGUNGA
"... Tumekamilisha ujenzi wa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) yenye uwezo wa kuhudumia Wagonjwa mahututi kumi kwa wakati mmoja, Tumekamilisha ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto yenye uwezo wa kuhudumia kina Mama na Watoto hamsini kwa wakati mmoja, Tunaendelea na ukarabati mkubwa wa hospitali ya Wilaya, Tumeweka mashine ya mionzi ya kisasa (Digital X Ray's Machine), Tumeongeza upatikanaji wa madawa na vifaa tiba, Tumekamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Itumba na nyumba za wauguzi, Tumefanya upanuzi wa Kituo cha Afya Igurubi na kujenga Stoo ya Kuhifadhi madawa ya kisasa, Tumepanua Kituo cha Afya Cha Nanga na kukamilisha ujenzi Jengo la upasuaji, Wodi ya Mama na Mtoto na Nyumba ya Mganga Mfawidhi, Tumepatiwa Magari ya kubeba Wagonjwa na shughuli za uratibu, Tumekamilisha ujenzi wa Zahanati za Vijiji Tisa (9), Tunaendelea kukamilisha zilizokuwa zimeishia njiani kwenye ujenzi Vijiji Saba (7), Tumeongeza Wauguzi na kutoa huduma mbalimbali za tiba na chanjo..."
NICHOLAUS GEORGE NGASSA
MBUNGE WA JIMBO LA IGUNGA