Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Jiwe kubwa la almasi ambalo ni la tatu kwa ukubwa duniani limepatikana nchini Botswana, katika machimbo ya dhahabu ya Jwaneng yanayotajwa kuwa yenye utajiri mkubwa zaidi wa almasi duniani.
Jiwe hilo lenye ukubwa unaolingana na ngumi lina uzito wa karati 1,098. Thamani ya jiwe hilo inatarajiwa kutajwa ndani ya siku chache zijazo, lakini watafiti wa madini ya almasi wanakadiria kuwa litafikia thamani ya dola bilioni 2 (sawa na Tsh. trilioni 4 na bilioni 638).
Jiwe kubwa zaidi la almasi kuwahi kuchimbwa duniani lilikuwa Cullinan lililochimbwa mwaka 1905, likiwa na uzito wa karati 3,106.75. Jiwe hilo lilikatwa katika vipande ambavyo baadhi yake vinaunda vito vya thamani vya Malkia wa Uingereza (Crown Jewels)
Jiwe la pili kwa ukubwa, Sewelo, lilichimbwa mwaka jana likiwa na uzito wa kareti 1,758 na kununuliwa na Kampuni ya Fasheni ya Ufaransa ya Louis Vuitton.
Kampuni iliyochimba jiwe hili sasa, Debswana, inasema hilo ndio jiwe lake kubwa zaidi kuchimbwa ndani ya miongo mitano (miaka 50) iliyokuwa katika biashara ya uchimbaji.
Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi akiwa ameshika jiwe hilo. Picha: AFP