Jiwe Lililoko Kamanga Fery Jijini Mwanza Libadilishwe jina Kutoka Bismack Rock na kuwa Muujiza wa Mwanamalundi

Wasukuma wapo hapa kujadili utamaduni wao.

Kisha wanatumia lugha ya kigeni kujadili utamaduni wao.

Na hilo ni tatizo letu wengi. Hakuna nchi itaendelea huku inapiga teke utamaduni wake.

Utamaduni unatia ndani lugha.

Leo hii mambuzi mengine yanachanganya 'L' na 'R' mengine hayaweki 'H' inapotakiwa na kuiweka isipotakiwa. Mengine yapo bize kuandika 'Bhana' mengine yanachanganya 'dh' na 'th' mengine yanachanganya kwa kujiamini kabisa 'nadra' na 'aghalabu'

Yapo mengi. Huu uzi unamaanisha cha kuhifadhiwa siyo hilo jiwe tu.
Lugha ya kigeni? Siyo hakika Kiswahili ni lugha ya kigeni katika Usukuma?
 
Anhaa kajaribu kuongea kisukuma Mtwara.

Ukiona hawakuelewi jaribu Kiingereza.

Ukiona hawakuelewi jaribu Kiswahili.

Rudia zoezi hilo Mbeya, Kilwa na Makete.
 
Wakuu,

Hili ni bandiko la ushauri kwa mam;laka husika lakini kuwekwa kwenye mjadala kuhusu jiwe kubwa la aina yake ambalo linatumika kama utambulisho wa jiji la Mwanza.

Jiwe hili liko pembezoni mwa mwa ufukwe wa ziwa Viktoria karibu na feri ya Kamanga na sambamba na barabara ya Nasser inayoelekea Ikulu ndogo huko Capri-Point.

Jiwe hili alilitumia mchezaji wa ngoma za kienyeji za kisukuma aitwaye Igulu Bugomola (Ng'wanamalundi/Mwanamalundi-thin legs and tall) ambapo alipanda juu yake baada ya kusimika vijiti vya miti kwenye mwamba na kukwea hadi juu kisha akaa na kucheza. Mpaka leo kuna masalia ya matundu ya yaliyotumika kusimika vijiti hivyo na sehemu alipokaa aliacha alama ya upande mmoja wa kalio. Igulu Bugomola alias Mwanamalundi alizaliwa huko Mwakabunga Nera wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza mwaka 1846. Huyu Mwanamalundi alitokea kuwa na uwezo wa kucheza vizuri ngoma za kisukuma kwa ufasaha mkubwa akiambatana na miujiza ya kimazingara. (Soma kitabu kilichoandikwa na Boniphas Z. Boaz kwa undani zaidi).

Wakati wakoloni walipoingia nchini Tanganyika, moja ya maeneo ambayo Mjerumani aliyatamani sana ni jiji la Mwanza ambapo mtawala aitwaye Otto Von Bismarck sanamu lake liliwekwa juu ya jiwe hilo lililoko karibu na Kamanga feri. Baada ya sanamu kuwekwa juu ya jiwe na jina likaitwa 'BISMARCK'.

Ilipotokea vita kuu ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza (WWII) 1939-1945 ambapo Mjerumani alishindwa vita na Mwingereza na kwa kuwa Mwingereza alimchukia Mjerumani waliamuru sanamau la mtawala wa Kijerumani kuvunjwa na kutupwa majini kitendo ambacho kilitekelezwa haraka sana.Masalia ya sanamu hilo yapo mpaka leo hapo majini.

Napendekeza ili kulinda urithi wa kihistoria wa wenyeji jiwe hilo libadilishwe na kuitwa jina la 'Miujiza ya Mwanamalundi-The miracles of Mwanamalundi' kama utambulisha wa jiji hilo la miamba ya mawe.

View attachment 1646192View attachment 1646194
Pamoja na jiwe hilo lipo jingine lenye maajabu maeneo ya Bugarika linaitwa majimoto ambalo linaukumbi wa wazi chini yake linafaa kwa utalii wa ndani na nje
View attachment 1646199

Nawasilisha
Nimekuja mbio nikidhani mleta mada ni Infantry Soldier
 
Mmeishafanya sasa hii nchi niyawasukuma?Gwajiboy alituletea ukabila na wewe unakuja na hili kwanj vitabu havitoshi
 
Wasukuma wapo hapa kujadili utamaduni wao.

Kisha wanatumia lugha ya kigeni kujadili utamaduni wao.

Na hilo ni tatizo letu wengi. Hakuna nchi itaendelea huku inapiga teke utamaduni wake.

Utamaduni unatia ndani lugha.

Leo hii mambuzi mengine yanachanganya 'L' na 'R' mengine hayaweki 'H' inapotakiwa na kuiweka isipotakiwa. Mengine yapo bize kuandika 'Bhana' mengine yanachanganya 'dh' na 'th' mengine yanachanganya kwa kujiamini kabisa 'nadra' na 'aghalabu'

Yapo mengi. Huu uzi unamaanisha cha kuhifadhiwa siyo hilo jiwe tu.
Enyelileshi!!
 
Wakuu,

Hili ni bandiko la ushauri kwa mam;laka husika lakini kuwekwa kwenye mjadala kuhusu jiwe kubwa la aina yake ambalo linatumika kama utambulisho wa jiji la Mwanza.

Jiwe hili liko pembezoni mwa mwa ufukwe wa ziwa Viktoria karibu na feri ya Kamanga na sambamba na barabara ya Nasser inayoelekea Ikulu ndogo huko Capri-Point.

Jiwe hili alilitumia mchezaji wa ngoma za kienyeji za kisukuma aitwaye Igulu Bugomola (Ng'wanamalundi/Mwanamalundi-thin legs and tall) ambapo alipanda juu yake baada ya kusimika vijiti vya miti kwenye mwamba na kukwea hadi juu kisha akaa na kucheza. Mpaka leo kuna masalia ya matundu ya yaliyotumika kusimika vijiti hivyo na sehemu alipokaa aliacha alama ya upande mmoja wa kalio. Igulu Bugomola alias Mwanamalundi alizaliwa huko Mwakabunga Nera wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza mwaka 1846. Huyu Mwanamalundi alitokea kuwa na uwezo wa kucheza vizuri ngoma za kisukuma kwa ufasaha mkubwa akiambatana na miujiza ya kimazingara. (Soma kitabu kilichoandikwa na Boniphas Z. Boaz kwa undani zaidi).

Wakati wakoloni walipoingia nchini Tanganyika, moja ya maeneo ambayo Mjerumani aliyatamani sana ni jiji la Mwanza ambapo mtawala aitwaye Otto Von Bismarck sanamu lake liliwekwa juu ya jiwe hilo lililoko karibu na Kamanga feri. Baada ya sanamu kuwekwa juu ya jiwe na jina likaitwa 'BISMARCK'.

Ilipotokea vita kuu ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza (WWII) 1939-1945 ambapo Mjerumani alishindwa vita na Mwingereza na kwa kuwa Mwingereza alimchukia Mjerumani waliamuru sanamau la mtawala wa Kijerumani kuvunjwa na kutupwa majini kitendo ambacho kilitekelezwa haraka sana.Masalia ya sanamu hilo yapo mpaka leo hapo majini.

Napendekeza ili kulinda urithi wa kihistoria wa wenyeji jiwe hilo libadilishwe na kuitwa jina la 'Miujiza ya Mwanamalundi-The miracles of Mwanamalundi' kama utambulisha wa jiji hilo la miamba ya mawe.

View attachment 1646192View attachment 1646194
Pamoja na jiwe hilo lipo jingine lenye maajabu maeneo ya Bugarika linaitwa majimoto ambalo linaukumbi wa wazi chini yake linafaa kwa utalii wa ndani na nje
View attachment 1646199

Nawasilisha

Mwanamalundi ndio nani? Ana faida gani kwenye hilo kiwe?
 
Back
Top Bottom