JK akiri kufanya makosa sekondari za kata

JK akiri kufanya makosa sekondari za kata

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Hatimaye wanaanza kukubali makosa yao

JK akiri makosa ujensi wa sekondari za kata

Na Jackson Odoyo na Happy Lazaro, Arusha

RAIS Kikwete amesema Serikali ilifanya makosa makubwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari kwa kushindwa kujenga maabara katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza sekta ya elimu ya Sayansi na Teknolojia nchini.

“Tulifanya makosa wakati tunajenga madarasa ile ya mikondo minne kwa sababu hatukukumbuka kujenga maabara mapema katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza elimu ya Sayansi na Teknolojia tangu awali. Lakini
hivi sasa Serikali imeliona hilo na ndiyo maana tukaamua kujenga Chuo Kikuu cha Utafiti wa Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichojengwa kwa fedha za Serikali,” alisema Rais Kikwete.

Chuo hicho mwaka jana kilidahili ya wanafunzi 83, huku wanafunzi 30 wakichukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili.

Mwaka huu kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili, wakiwamo 46 wa masomo ya uzamivu na 89 wa uzamili huku asilimia 22 wakiwa wanawake.

Rais alisema kwamba wasomi watakaosoma katika chuo hicho ni wale wenye shahada ya kwanza baada ya kusoma katika vyuo vingine na watakapofika katika chuo hicho watakuwa na kazi ya kuzama zaidi katika elimu ya utafiti wa Sayansi na Teknolojia.

Rais Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi wa chuo hicho jijini Arusha, huku akifafanua kwamba Tanzania hivi sasa imeanza kuingia katika idadi ya nchi tajiri na kuondokana na umasikini kama Chuo hicho kitakuwa na maendeleo.

Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliwataka wakuu wa chuo hicho, wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Profesa David Mwakyusa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Burton Mwamila kusimamia maendelea ya chuo hicho kwa dhati.
 
Mwana Mpotevu,

..badala ya kujenga maabara kwenye shule za kata, serikali imeamua kujenga chuo kikuu cha sayansi na teknolojia!!

..sasa wanafunzi wanaokolifai kujiunga na hicho chuo kikuu watatoka wapi wakati mfumo wetu wa ufundishaji sayansi uko shaghala-baghala??
 
Last edited by a moderator:
Elimu butu ya kata wanayoipata vijana wetu kwa upande mwingine ina faida kwani imesaidia sana vijana kuichukia ccm baada ya kugundua kwamba wanadanganywa!!
 
Mwana Mpotevu,

..badala ya kujenga maabara kwenye shule za kata, serikali imeamua kujenga chuo kikuu cha sayansi na teknolojia!!

..sasa wanafunzi wanaokolifai kujiunga na hicho chuo kikuu watatoka wapi wakati mfumo wetu wa ufundishaji sayansi uko shaghala-baghala??

hapo ndo ushangae hapo jamaa anaona amefikiri vya kutosha kweli kweli, hii siyo akili. Ubovu wa nyumba uko kwenye msingi wewe unaanza kufanya repair kwenye paa eti jawabu la kurekebisha tataizo la kwenye msingi. Hiki kweli ni kfuu cha nazi siyo kawaida hii. Rais wetu anashida upstairs au wanaomwandalia hotuba wanashida na pia Rais haipitii hotuba prior presentation. Kama Mulugo vile.
 
Last edited by a moderator:
'Uhovyo' wa shule za kata wa kulaumiwa hapo ni sterling & 'visionary leader' wenu Mamvi..eti naskia this self-serving self-important fisadi mnataka kumpa urais! mwe! wadanganyika kweli ni kama punda.

Hii Nelson Mandela ni mzigo mwignine kwa mlipa kodi na sisi wachangiaji wa mifuko ya jamii. Sioni ni kwa jinsi gani sayansi inahusiana na mimastaz na mipihedii..kuna low cost scientific innovations nyingi zngeeza kubadilisha sekta za madini, kilimo, usafirishaji etc kwa kutumia hata watu wa VETA iwapo zingepatiwa funds regularly! hao maprof walishafeli kwa kung'ang'ana na vitabu badala ya kuisaidia jamii ktk muktadha halisia.
 
Kuna wabunge wa ccm wanatokwa povu kutetea kila serikali inapohojiwa kuhusu hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
pesa za uswiss si zinaweza kusaidia kujenga maabara kwa shule za secondari za kata nchi nzima. Mkoroni alipokuwa anjenga shule za secondari, utadhania vile anjenga ikulu kwa jinsi alivyozijenga vizuri. Wewe tembelea ndanda, Tosamaganga, Umbwe na Pugu. Lakini serikali haijaiga ujenzi sekondari za kiaina hiyo mbali ya pale benjamini Mkapa ilipo.
 
na kile chuo cha kata pale dom vp hajakiri bado?au kile n mali ya ccm mana getini tu kuna mnara wa Ccm
 
wewe ndio boring
kwanini?
Je ni zile safari zangu za ughaibuni kila siku?
je ni vile ninavyo ddanganywa na kupotoshwa na wasaidizi wangu?
je ni vile ninavyo chekacheka hata sehemu ambazo kicheko hakitakiwi?
au ni kwa sababu ni mdhaifu na mwoga kwenye kufanya maamuzi magumu?
 
Mwana Mpotevu,

..badala ya kujenga maabara kwenye shule za kata, serikali imeamua kujenga chuo kikuu cha sayansi na teknolojia!!

..sasa wanafunzi wanaokolifai kujiunga na hicho chuo kikuu watatoka wapi wakati mfumo wetu wa ufundishaji sayansi uko shaghala-baghala??
Ha ha ha! mkuu umenikatizia kwa mbele. Umeliona eh! Kwamba unategemea kuweka mbolea wakati wa kuvuna.

Hili la sekondari za kata ambazo zinatumika kumpandisha chati EL tulilisema mapema sana.
Huwezi kuamka asubuhi bila kushauriana na wataalamu halafu ukafanya jambo zito kama hilo.
Tuliposema ni serikali ya JK ilijibu kuwa ujenzi wa madarasa unakwenda samba mba na makataba na maabara.
Leo anageuka.

JK burdani sana
 
Naona kama sijamwelewa Kikwete vile,hivi hivi hao wazamili na wazamivu ndio watakaopelekwa kufundisha sayansi katika shule za kata?
 
Masikini Huyu JK huwa ajui nini cha kuongea na wapi akiongee. Kwanza hiki chuo hakiitwi Chuo Kikuu cha Utafiti wa Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kama anavyokiita bali ni Taasisi ya Kiafrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia (The Nelson Mandela African Institute of Science and Technology) .

Pili, Chuo hiki kinatoa elimu ya kuanzia shahada ya uzamili. Hakidahili wanafunzi wa shule za sekondari bali wanafunzi wenye shahada ya kwanza kutoka katika vyuo vikuu na taasisi zingine zinazotoa elimu ya juu. Hivyo wenye kupata shida na makosa ya shule za kata sio chuo hiki bali ni vyuo vinavyo dahili wanafunzi wa sekondari kwa ajili ya programu zao.

Tatu, kuwepo kwa chuo hiki hata siku moja hakuwezi kuwa ni mbadala wa kukosekana kwa maabala katika sekondari za kata kwani chuo hiki kinashughulika na watu ambao wanaendelea kuingia ndani zaidi katika nyanja zao za sayansi walizokwisha kuwa nazo.


Rais wa wadanganyika sijui huwa hata anajua analiweka taifa katika hali gani kwa mataifa mengine kwa kauli zake zisizo na mantiki
 
Mwana Mpotevu,

..badala ya kujenga maabara kwenye shule za kata, serikali imeamua kujenga chuo kikuu cha sayansi na teknolojia!!

..sasa wanafunzi wanaokolifai kujiunga na hicho chuo kikuu watatoka wapi wakati mfumo wetu wa ufundishaji sayansi uko shaghala-baghala??

wanaendelea kufanya makosa yale yale. wakuu wetu hawa hawajifunzi kuokana na makosa yao
 
Wanafunzi wanaofeli shule za kata ni laki kadhaa..na hiki chuo kinadahili wanafunzi wachache tena kuanzia level ya uzamili...JE kuna kuna uhusiano gan kati ya kuwepo kwa hki chuo na kusahihisha makosa ya kukosekana kwa maabara ktk shule za kata?/matokeo mabovu ya shule hzi?
 
walikurupuka sana kuanzisha shula hizo, kwani Lengo la shule za kata ilikuwa ni Urais 2015 kwa Lowasa ,
 
Hapana lolote litakalo kuwa bila kuanza kujenga msingi! mu-arobaini wa tatizo la elimu nchini ni kuongeza
bajeti katika secta hiyo itakayowezesha kila shule kuwa na hadhi ya shule na pia kurudisha heshima ya walimu
nchini.
Sasa hivi mwalim hawezi kumwambia mzazi wake wa kijijini kwamba yeye ni mwalimu bali atamwambia anafanya
kazi wizara ya elimu.......
Bila shule bora, bila waalim bora wenye afya ya kiakili na kimwili hata pawepo na Obama institute of.... hamna kitu !!!!
 
Back
Top Bottom