Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,501
Hatimaye wanaanza kukubali makosa yao
JK akiri makosa ujensi wa sekondari za kata
Na Jackson Odoyo na Happy Lazaro, Arusha
RAIS Kikwete amesema Serikali ilifanya makosa makubwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari kwa kushindwa kujenga maabara katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza sekta ya elimu ya Sayansi na Teknolojia nchini.
Tulifanya makosa wakati tunajenga madarasa ile ya mikondo minne kwa sababu hatukukumbuka kujenga maabara mapema katika shule hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza elimu ya Sayansi na Teknolojia tangu awali. Lakini
hivi sasa Serikali imeliona hilo na ndiyo maana tukaamua kujenga Chuo Kikuu cha Utafiti wa Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichojengwa kwa fedha za Serikali, alisema Rais Kikwete.
Chuo hicho mwaka jana kilidahili ya wanafunzi 83, huku wanafunzi 30 wakichukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili.
Mwaka huu kimedahili wanafunzi 135 wa kundi la pili, wakiwamo 46 wa masomo ya uzamivu na 89 wa uzamili huku asilimia 22 wakiwa wanawake.
Rais alisema kwamba wasomi watakaosoma katika chuo hicho ni wale wenye shahada ya kwanza baada ya kusoma katika vyuo vingine na watakapofika katika chuo hicho watakuwa na kazi ya kuzama zaidi katika elimu ya utafiti wa Sayansi na Teknolojia.
Rais Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi wa chuo hicho jijini Arusha, huku akifafanua kwamba Tanzania hivi sasa imeanza kuingia katika idadi ya nchi tajiri na kuondokana na umasikini kama Chuo hicho kitakuwa na maendeleo.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliwataka wakuu wa chuo hicho, wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Profesa David Mwakyusa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Burton Mwamila kusimamia maendelea ya chuo hicho kwa dhati.