Elections 2010 JK alianguka tena jukwaani Sengerema na Mbeya?

Elections 2010 JK alianguka tena jukwaani Sengerema na Mbeya?

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Hivi Muungwana alianguka tena jukwaani huko Sengerema na Mbeya? Hii ilifichwa bila shaka, ingawa siamini iwapo inawezekana kufichwa! Hebu someni sehemu hii ya makala ya Tegambwage katika Mwanahalisi ya leo:





……Lakini nani angependa, wakati huu, kusikia kwa kina na kwa kipindi kirefu kwa mfano, simulizi juu ya Jakaya Kikwete na mke au wake zake; au malumbano kati ya mke mdogo na mkubwa; nyumba ndogo na ahadi za pembeni, kama zipo?

Katikati ya tuhuma za ukwapuaji mabilioni ya shilingi kutoka Hazina na Benki Kuu kwa kutumia makampuni ya kitapeli kama Kagoda Agriculture Limited, nani anategemea wananchi wawe na hamu kubwa ya kusikia uvumi kuwa rais wao ameishiwa nguvu tena na kudoindoka huko Sengerema na Mbeya?

Hii haina maana kuwa hayo hayastahili kufahamika; bali vipaumbele vya wakati uliopo vinalazimu hayo yatajwe na kuachwa ili akili na nguvu za wananchi vielekezwe katika kupagania uhuru, haki na ustawi wa jamii zao na mustakabali wa taifa.

Lakini mkuki kwa nguruwa, kwa binadamu mchungu. Mapema mwaka huu mhariri na mwandishi wa Mwanahalisi waliitwa mara tatu kwa Msajili wa Magazeti (MAELEZO) kuhojiwa kwa nini wanaandika makala “juu sa Salma Kikwete,” mke wa rais.

Haifahamiki iwapo rais anajua malalamiko hayo, kwani makala zenyewe hazikuwa zinachimba usichana, umama au biashara za mke wa rais. Zilikuwa zikijadili nafasi ya mke wa rais (yeyote yule kwa mifano ya Marekani, Zimbabwe, Kenya na Tanzania) katika mustakabali wa taifa.Bali MAELEZO waliamuru makala zisitishwe kwa madai kuwa “mama amelalamika.” Jee, leo Dk Slaa hajalalamika?.......
 
Inawezekana kabisa hili wala sishangai! Muungwana mgonjwa sana tu!
 
Dr Slaa yeye sio binadamu wala hawezi lalamia ila wao (CCM) ndio binadamu wanaweza kulalamika na kusikilizwa. Wahenga walisema "Mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu" ama ule wimbo wa mjomba Mrisho Mpoto alipofika mjini baada ya kupata nauli ndio hayo ukimkanyaja tu........
 
Muungwana keshakuwa gari bovu spana mkononi.Kabakia kuuza sura tu lakini afya ina mgogoro mkubwa saaana
 
Muungwana keshakuwa gari bovu spana mkononi.Kabakia kuuza sura tu lakini afya ina mgogoro mkubwa saaana

That is that - JK anahitaji uangalizi wa Madaktari kama alivyokuwa Pop Star Michael Jackson (RIP)!
 
Natoa wito kwa watanzania KWAMBA tumsaidie raisi wetu kwa njia ya kumnyima kura hapo tarehe 31 october 2010 ili apate muda wa kutosha wa kupumzika na wa kusikilizia afya yake kwani nchi yetu ina mambo na matatizo mengi sana yanayopaswa kusimamiwa na kushughulikiwa na rais mwenye nguvu na afya njema
 
afya yake inafahamika siku nyingi kuwa ni mbovu tatizo wabongo mnamng'anga'nia,si mnakumbuka nigeria? yaliyomkumba rais wao.
 
Waache hao CCM waendelee kuwasha kibatali bila kuongezza mafuta. Watu tumejaribu kuwasaidia kuwastua kuwa mafuta yamebaki kiduchu lakini hawasikii. Sasa kikizimika kabisa watatuambia nini? Huo ndo mwanzo wa kwenda kuficha mgonjwa asiye hai nje ya nchi kwa gharama kubwa za walipa kodi (kama ilivyotokea Zambia) ili waweze kuweka vizuri drama zao. Hii michezo yao lazima itatuingiza gharama kubwa huko mbele ya safari (ingawa hadi sasa tunalipa hizo gharama). Ipo siku mikanda yote inayofichwa aitawekwa hadharani!
 
hivi hii haikutangazwa eee! ni kweli jamaa alidondoka huko sengerema

hawakusema yule jamaa ni mgonjwa sana
 
Hivi wakuu
Wanasema muungwana anaumwa lakini anaumwa nini? Kama kuna mtu anajua anachoumwa asema tu wazi, manake mficha magonjwa maradhi umuumbua. Kwa upande mwingine kila binadamu anaweza kuugua kwa wakati wowote, ishu hapa ni kama ana magonjwa ya muda mrefu au ilikuwa kuishiwa sukari tu.
 
Au tumpeleke st thomas london?......................kunahabari kuwa alianguka huko pia............hii tu inamdiscolify kuwa presidential candidate........aache nchi8 kwa watu strong km akina dr.slaa.
 
Hivi wakuu
Wanasema muungwana anaumwa lakini anaumwa nini? Kama kuna mtu anajua anachoumwa asema tu wazi, manake mficha magonjwa maradhi umuumbua. Kwa upande mwingine kila binadamu anaweza kuugua kwa wakati wowote, ishu hapa ni kama ana magonjwa ya muda mrefu au ilikuwa kuishiwa sukari tu.

KUISHIWA KINGA YA MWILI aka NGOMA
 
Katika hili naanza kutilia shaka pia uwezo wake kiaakili kama anaweza kufanya maamuzi sahihi! Tunaweza kuwa tunaona smiling face kumbe ni picha tu!
 
tehe....tehe............te...te....teeeeeeeeeeeeee......kwa hiyo unamaanisha tuna rais mdoli?
Katika hili naanza kutilia shaka pia uwezo wake kiaakili kama anaweza kufanya maamuzi sahihi! Tunaweza kuwa tunaona smiling face kumbe ni picha tu!
 
Madaktari walishasema kwamba "anatakiwa kupumzika", yaani hata uraisi aachie ngazi - lakini CCM bado wanamtembeza mpaka anaanguka anguka. Hofu yangu gharama za uchaguzi zitaongezeka pale kwa kujua kabisa jamaa anaumwa na tukafanya uchaguzi wa Rais kabla ya kipindi kingine.

Kumsaidia Chagua CHADEMA - ili muungwana apate "honorary exit"
 
Back
Top Bottom