Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Hivi Muungwana alianguka tena jukwaani huko Sengerema na Mbeya? Hii ilifichwa bila shaka, ingawa siamini iwapo inawezekana kufichwa! Hebu someni sehemu hii ya makala ya Tegambwage katika Mwanahalisi ya leo:
Lakini nani angependa, wakati huu, kusikia kwa kina na kwa kipindi kirefu kwa mfano, simulizi juu ya Jakaya Kikwete na mke au wake zake; au malumbano kati ya mke mdogo na mkubwa; nyumba ndogo na ahadi za pembeni, kama zipo?
Katikati ya tuhuma za ukwapuaji mabilioni ya shilingi kutoka Hazina na Benki Kuu kwa kutumia makampuni ya kitapeli kama Kagoda Agriculture Limited, nani anategemea wananchi wawe na hamu kubwa ya kusikia uvumi kuwa rais wao ameishiwa nguvu tena na kudoindoka huko Sengerema na Mbeya?
Hii haina maana kuwa hayo hayastahili kufahamika; bali vipaumbele vya wakati uliopo vinalazimu hayo yatajwe na kuachwa ili akili na nguvu za wananchi vielekezwe katika kupagania uhuru, haki na ustawi wa jamii zao na mustakabali wa taifa.
Lakini mkuki kwa nguruwa, kwa binadamu mchungu. Mapema mwaka huu mhariri na mwandishi wa Mwanahalisi waliitwa mara tatu kwa Msajili wa Magazeti (MAELEZO) kuhojiwa kwa nini wanaandika makala juu sa Salma Kikwete, mke wa rais.
Haifahamiki iwapo rais anajua malalamiko hayo, kwani makala zenyewe hazikuwa zinachimba usichana, umama au biashara za mke wa rais. Zilikuwa zikijadili nafasi ya mke wa rais (yeyote yule kwa mifano ya Marekani, Zimbabwe, Kenya na Tanzania) katika mustakabali wa taifa.Bali MAELEZO waliamuru makala zisitishwe kwa madai kuwa mama amelalamika. Jee, leo Dk Slaa hajalalamika?.......