Elections 2010 JK 'alivyofunika' TABORA

Mhh, nipo hapa nasubiri picha za wana CHADEMA na nimeona za CCM.

Nikiona zote basi nachanganya Za kuambiwa na za kwangu.

Ila kwa kuwafahamu Wanyamwezi, inawezekana hali ilikuwa hivi:

Walifika mapema na kupata burudani. Alipoingia Kikwete, wakakaa kumsikiliza na picha zikapigwa ambazo tunaona zipo kwa Michuzi. Walipoona stori ni zilezile basi wakaanza kujiondoa taratibu na ndiyo maelezo ambayo Revocatus kaandika.

Nasubiri picha zote tuone kipi ni kipi maana siku hizi wote tumekuwa Mbayuwayu ati.
 
Mkulu anagongesha!!!!









Akiwa na mgombea ubunge Tabora Mjini Bw. Ismael Aden Rage!





 
Nimeshiriki kuujenga enzi hizo nikiwa mwanafunzi tbr school aka berlin kabla jamaa hawajauteka eti ni wa ccm
 
Mbona mashati meupe ni mengi sana jukwaani? Inaonekana rangi nyeupe ni favorite color in Tabora.
 
Asipoambatana na vikundi vya burudani watu wanakuwa wengi hivyo?
 
Mwananchi, la leo limetoa habari kuwa mgombea wa ccm zenga naye, amekataliwa na wananchi mbele ya jk, mwenye habari zaid atufahamishe
 







Picha kwa niaba ya Michuzi

Huyo dada yuko na JK na katikati ya Michuzi na mwenzie nina mfahamu ni mlemavu hana mikono, wala JK hana mchango wowote katika kumsaidia huyo binti kwani toka kichanga kimelelewa kwa masista wa huruma kama wale wa Mburahati pale Tabora RC Cathedral. Hii inaonesha akina Michuzi ndio wanamtafutia JK walemavu kila anapokwenda, ujinga kabisa huo.

Picha za Michuzi haziwezi kuwa na ujumbe kamili.
 
mhh, nipo hapa nasubiri picha za wana chadema na nimeona za ccm.

Nikiona zote basi nachanganya za kuambiwa na za kwangu.

Nasubiri picha zote tuone kipi ni kipi maana siku hizi wote tumekuwa mbayuwayu ati.

ki-ukweli nipo naangalia kwenye taarifa ya habari tbc1 wamechakachua picha,wameelekeza upande ambao watu walikaa kwa wigi na kuacha sehemu kubwa ya uwanja bila kuionyesha ikiwa empty kama ilivyokuwa na kwa taarifa yenu watu wenyewe asilimia kubwa ni wana-vyuo na watoto....hivi kakuambia nani sisiemu wakuonyeshe picha za malori na mabasi yanayoleta watu?

Invisible amepewa hizo picha,ziweke tafadhali watu wajionee hata upande mkubwa wa uwanja ulivyokuwa empty tofauti na ccm wanavyoonesha,but also jinsi makundi ya watu wakiondoka utadhani ndio mkutano umeisha kumbe mheshimiwa anahutubia.
 

Kabsaa,anatoa zile zinazoonesha umati mkubwaa,na hata ungekuwa wewe mwajiriwa wa CCM lazima ufanye hivyo..Sitaki kuwa mnafiki,watu waliingia na kujaa karibia NUSU uwanja,ILibidi kabla JK hajafika wanachuo waombwe kushuka na kukaa katikati ya uwanja sehemu ambayo ni karibu na JK anahutubia ili itakapochukuliwa picha waonekane walikuwa wengi..!hata ukimuuliza michuzi atakuambia kama si mnafiki pia,lakini nani akupigie picha ya ENEO KUUBWA Tena zaidi ya NUSU likiwa halina watu,akuoneshe malori na mabasi na analipwa na CCM?
 
revocatus, mbona picha hatuzioni? au invisible amezibania?
 
Watuoneshe na picha ya Ze Comedy na Marlaw wanavyoimba na kujefanya wanawake.
Mjinga ndio aliwae.Hata Ze Comedy wanasema,Mbona hamshtuki?wao wako kimaslahi zaidi.
 



Picha za malori mbona hakuna UA INVISIBLE KAZICHAKACHUA?
 


Hapo ni baadhi ya mabasi yakileta watu hapa ilikuwa kwa ndani




Hapa malori na mabasi nje ya uwan









Haya makundi unayoyaona siyo kwamba mkutano ulikuwa umeisha ni watu walikuwa wakitoka baada tu ya JK kuanza kuhutubia na baada ya kuangalia ze komedi

N:B picture quality,nilitumia simu
 


Hapo ni baadhi ya mabasi yakileta watu hapa ilikuwa kwa ndani







Hapa malori na mabasi nje ya uwanja

















Haya makundi unayoyaona siyo kwamba mkutano ulikuwa umeisha ni watu walikuwa wakitoka baada tu ya JK kuanza kuhutubia na baada ya kuangalia ze komedi







hii ni sehemu ndogo tu kati ya kubwa iliyo wazi ambayo michuzi hakuthubutu kuiweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…