Huyu jamaa mzima kweli??????
Source: Habari leo
Kikwete aahidi chuo kikuu Shinyanga
BAADA ya kukamilika ujenzi wa vyuo vikuu vya Dodoma na Mwalimu Nyerere mkoani Mara, utafuata ujenzi wa chuo kikuu cha Shinyanga.
Hiyo ni ahadi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, aliyoitoa juzi baada ya kuombwa na wakazi wa wilaya za Bukombe na Kahama, kwenye mikutano ya kampeni.
Akiwa Bukombe, mgombea ubunge, Emmanuel Luhahula, aliomba chuo kikuu mkoani humo kwa sababu hawana chuo kama hicho.
Naye mgombea ubunge wa Kahama James Lembeli, aliomba chuo kikuu hicho ili kusaidia vijana wa mkoa huu.
Mbunge wa zamani wa Msalala, Ezekiel Maige ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, aliomba kujengwa chuo cha ufundi ili kutoa fursa kwa vijana wa Kahama kupata ajira ikiwamo migodini.
Akizungumza na wananchi wa Kahama kwenye uwanja wa michezo mjini humo, Kikwete , alisema ujenzi wa chuo kikuu ni lazima, lakini kwanza amalize vya Dodoma na Butiama.
Ngoja tulitafakari vizuri, lakini ni lazima tujenge. Kwa sasa tunakamilisha Dodoma na kisha Butiama kwa heshima ya Mwalimu Nyerere
baada ya hapo, tutaliangalia hili, alisema.
Akizungumzia tatizo la maji, alisema Kahama kwa sasa haina matatizo hayo baada ya kupata maji ya Ziwa Victoria, isipokuwa vijiji 15 vilivyopo kilometa 15 kutoka mradi huo, vitapewa maji na tayari zimetengwa Sh bilioni 12.9 kufanikisha kazi hiyo.
Kuhusu barabara za mjini hapa, aliagiza zijengwe haraka kwa sababu fedha zimetolewa na kuwataka viongozi wa Serikali wanaogombana juu ya kujengwa kwa barabara hizo, kumaliza tofauti zao haraka.
Jumla Maoni (2)
Maoni ( huko huko habari leo)
1. anauhakika mpaka chuo cha dodoma kimalizwe kujengwa na kuanzwa kujengwa mpaka kmalizwa kwa chuo kingine cha kumbukumbu ya mwl nyerere atakuwa bado yupo madarakani na kama atakuwa ametoka anajuaje hao wanaofuata kama watakuwa na wazo kama lake au ilikuwa kuwapa moyo wana shy ili apate kura zao? wananchi tusidanganyike.
2. Kikwete hizo sound tu za kutaka kura,kama mwenzangu hapo juu anavyosema kuna vyuo mbili viishe then uanze shinyanga?angalau ungetudanganyia ukasema ile shaicom unaibadili kuwa chuo kikuu kama ulivyofanya chang'ombe......usituzuge bwana......
Mimi binafsi sidanganyiki