akilimtindi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 421
- 83
Wakuu samahanini sijatokea kwa siku kadhaa lakini naomba nitokee kwa haka ka-swali kangu, nimekauliza kwa kuwa kuna watu wengi humu naona sasa wanamtetea JK kwamba ni safi sana sasa.
Mimi naona Mkapa alijitahidi sana alipopokea nchi maana ilimbidi kwanza kuweka utaratibu kwenye mstari maana kodi ilikuwa ni zero na serikali ilishaishiwa kabisa, ingawa tunakubali pia kwamba upinzani kisiasa haukuwa mkubwa kwahiyo CCM haikutumia mamilioni kupiga kampeni. Ilitumika tu fimbo ya mchonga. Kwahiyo Mkapa alipopokea ilimbidi kutafuta mbegu akapanda, kisha akapalilia halafu mahindi yalipokuwa tayari akakata kidogo akachoma, akamkwanyulia shemejiye Yona kidogo wakaendelea hivyo hivyo.
Lakini hii ya Mkwere mimi naona sio ulafi ila uzumbuku, alisema vizuri sana alipopewa nchi mwaka 2005 kwamba Mzee Ben ameacha mambo safi. Iweje mara hili mara lile? Akampa swahiba wakashirikiana kuvuna mahindi yote wakachezea chezea wakala yote bila hata kuacha mbegu. Sasa tuwaeleweje wala mbegu? Alipoachiwa nchi alisema msingi ulikuwa tayari yeye sasa ni kujenga tu, juzi after miaka 3 anasema alikuwa anaweka misingi mizuri sasa muda si mrefu ataanza kujenga.
Naamini mwaka 2010 atasema ameshaweka misingi, sasa tumpe miaka mingine 5 apandishe mjengo. Na mimi naamini watanzania watampa. Je tuko tayari kufanya tathmini 2015?