JK apata PhD ya International Relations

JK apata PhD ya International Relations

nadhani anaweza pewa U-professor next time huko U.A.E (possibly before october); msimdharau rais wetu jamani, kafanya kazi kubwa sana .... kugawa Loliondo II kwa waarabu .... etc. etc. ... na sasa deal za ardhi anazotaka kuwapa wa-turkey siyo kazi ndogo hasa ukizingatia nyumbani "kelele za mlango zimezidi" .... hazimnyimi usingi though! lol!

MDBD
Champunga bila ya nyerere huyo chikwete angeipata wapi hiyo PHD? Kuna mahali pa kushambulia ovyo ovyo utakavyo hata kama unajipatia lubisi. Lakini kuna pa kuweka tafakuri kabla ya kutoa jibu.mkuu champunga usijeukawa chau bwabwa!!!!
 
So simple, maendeleo yetu hayataletwa na majamaa hao toka hukoooo....ni sisi wenyewe.

Sign of the times is that we do not marginalize ourselves from the rest of the world. We chart our path and forge ahead like others, or indeed, backwards as at the present. Reminds me of an unthinkable concept, TIME moving backwards.

The Champungas of Tanzania remind me of some other Champunga suggesting that Tanzania is synonymous with a huge beach, abundantly endowed with Champungas, lazy in their thinking, cognition and actually, just lazy! Maneno mingi tu ya Kiswahili na Uswahili!

Hakika maendeleo hayawezi kuletwa na sisi kama bado tutaendelea kufikiri kiazimio la Arusha. We need technology, skills, and networking with the rest of the world, Rais wetu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anayafahamu hayo na ndiyo mana hawezi kuendelea kuzubaa hapo Magogoni. Anatafuta kutuunganisha waTz tuliodumu sandukuni kwa miaka 45 na watu wegine duniani. Mwanzoni niliongelea upande wa elimu tu lakini pia biashara anafanya vizuri zaidi hata huko uturuki yuko na jopo la wafanyabiashara ameenda nao.

Narudia tena na tena Hongera kwa hiyo PhD unastahili, laiti Marais waliokutangulia wangekuwa na muono kama wako tungekuwa mbali. Usiwasikilize Hao wasiojua kutafuta wanaosubiri kuletewa. Wanasubiri watu waendelee halafu waanzishe azimio lingine la Arusha na kutaifisha mali za watu kisha kuzitelekeza. Hawa ndiyo wavivu wa .......................(Mkapa 200.
 
Champunga bila ya nyerere huyo chikwete angeipata wapi hiyo PHD? Kuna mahali pa kushambulia ovyo ovyo utakavyo hata kama unajipatia lubisi. Lakini kuna pa kuweka tafakuri kabla ya kutoa jibu.mkuu champunga usijeukawa chau bwabwa!!!!

Ooh my God, bado unaamini hivi kweli kazi ni kubwa maana na wengine kule kijijini wanaamini bila chama cha Nyerere (CCM) hakutakuwepo Tanzania. Yaani vijiimami imani tu. Huku tukiendelea kufail.

HONGERA kikwete, KWA hiyo PhD. tena nawaomba university waangalie uwezekana wa kumpatia mama naye haye hata Ka-bachelor ka public relation maana kila penye mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke imara.

Ukimaliza ziara yako huko uwalete hao wafanyabiasha huku niliko mimi maana nako kuna fursa za kuuza korosho zetu za kule Mtwara.
 
Hivi hizo Phd ni za kuwasaidia kufanya kazi?Kama sivyo hiyo ni heshima isiyo na maslahi na wananchi,ni heshima ya kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa,sawa tu na heshima walizokuwa wakipewa machifu wetu za shanga za shaba huku wakitoa gold...Kilichobadilika ni aina ya heshima tu kutegemea na wakati,lakini kitu ni kile kile....
Heshima zenye mwelekeo wa sifa binafsi za kutunukiwa bila kuzi earn zinazotolewa kwa viongozi wa kitaifa hazitakiwi kutafsiriwa kama heshima kwa Taifa kwani hatuko chini ya utawala wa Kifalme,unless ccm ni kizazi cha kifalme.
 
Hongera sana Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hiyo PhD. hakika unastahili.

Wazungu walisafiri kote duniani wakaleta maendeleo Europe. Tunashuhudia maendeleo makubwa hivi sasa ikiwa ni pamoja na ongezeko la waTZ wanaopata nafasi za masomo nje ya nchi.China, UK, United State, India ziko kibao, Belgium na sasa zingine lukuki huko Turkey haya yote ni matunda ya jitahada zako za kuimarisha uhusiano wa nchi yetu kimataifa. Laiti kama Maraisi waliokutangulia wangekuwa na muono kama wako tungekuwa mbali sana naamini hivyo.

Hatuna cha kujifungia nacho hapo TZ kwani kwa miaka 45 tumebaki masikini wa kutupwa dunia haiwezi kutusubili. Watu wamebaki wakimnukuu Nyerere hata kama wanajua na wanaambiwa na dunia mzima kuwa hakuna wazo lake lolote lililowahi kufanikiwa ila ni kuwadumaza watu wake tu kifikra na kimaendeleo. Wengine wanaendelea kusifia eti ukombozi wa bara la Afrika kwani nani angetaka kuitawala afrika au Tz hadi hivi sasa?. Kwa kweli kama hatutatoka nje kutafuta elimu na mitaji tukaendelea kubaki ndani tu eti tunatunza mali zetu hadi mungu atushushie hiyo elimu na uwezo, hakika wenye akili na uwezo na hiyo elimu watakuja kuifungua hiyo mipaka kwa maguvu na kuchukua kila kitu na hatutakuwa na uwezo wa kuwazuia kwani hiyo mipaka hajaweka mungu ni wao ndiyo waliiweka.

Mheshimiwa ukimaliza ziara yako huko Uturuki unaweza kwenda kupumzika kidogo kule Jamaica ukijipongeza kwa hiyo PhD. usihofu sisi ni wazima kabisa huku nyumbani.

Kwa kweli ni wewe tu unayefaa kuiongoza TZ kwa sasa endelea mheshimiwa maana wengine wataturudisha kwa mwalimu JK Nyerere.

ya ar a fool.
 
-kweli wameona wampe jamaa hilo shavu coz pamoja na kuzurura koote kule wasimpe degree ya kuendana na matendo yake,wameamua kuutambua mzururo wake(kidding)

-Lakini pia jamaa kajitahidi kuliuza jina la Tanzania nje ingawa gharama ni kubwa,awe strategic sasa
 
Pia nadhani hata hivyo vyuo vianvyowapa viongozi PHDs ni mbinu ya kujitangaza ama?
 
Lazima tutofautishe kutunukiwa na kupata PhD...vinginevyo mtamtukana mkulu bure..kapewa hajasomea na si lazima a-qualify...
 
Wakati mnaendelea kumkandia kwa kila neno mwenzenu ahhh wanampa mijituzo tuuu na latest ni hii


safi sana

Btw

Freeman Mbowe tangu afukuzwe kule Hull hivi kuna mpango wowote wa yeye kuendeleza masomo walau St Agostino University ?

Wana CHADEMA itabidi mniwie radhi lakini hili la kuendelea kuficha amendeleo ya masomo ya Freeman Mbowe ni aibu!


freeman_bowe_in_lndon.jpg


btw

Bills mpya kiboko hands down !!!

He he heeee,so hilo susla la kikwete umemalizana nalo au umejikatia tamaa?
 
Kuna ajenda ya siri katika yake maana huwa inakuwa ngumu sana kutoa degree ya heshima, wametoa maana huwa mara nyingi sana wanaweza kutoa labda kwa ajili ya kusafiri kwake maana anajua sana kusafiri na tena kwa hilo la kusafiri tu ni rais wa kwanza barani Africa kwa kusafiri. Hilo wampe hata PhD 4 hivi.
 
Ooh my God, bado unaamini hivi kweli kazi ni kubwa maana na wengine kule kijijini wanaamini bila chama cha Nyerere (CCM) hakutakuwepo Tanzania. Yaani vijiimami imani tu. Huku tukiendelea kufail.

HONGERA kikwete, KWA hiyo PhD. tena nawaomba university waangalie uwezekana wa kumpatia mama naye haye hata Ka-bachelor ka public relation maana kila penye mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke imara.

Ukimaliza ziara yako huko uwalete hao wafanyabiasha huku niliko mimi maana nako kuna fursa za kuuza korosho zetu za kule Mtwara.

Mkuu, kauli hizi zako kwangu mimi zina mlio wa SARCASM. Naona wengi hawajakuelewa unavyompiga nondo Muungwana kimzahamzaha.

Nafikiri somo limeeleweka. Shahada za heshima duniani zipo na zinakubalika. Tulichokosa hapa ni hoja thabiti inayo-justify Mkulu kutunukiwa hiyo PhD ilhali wengi hatujawa impressed na rekodi yake na, hapohapo, tunashaka huenda ni mbinu za Waturuki kutulainisha ili wateke fursa za kiuchumi nchini kwetu bila kudhibitiwa ipasavyo.
 
Labda aende Israel uone kama watampa hata Degree ndio ujue kuna nini maana Tanzania imekuwa mbali sana na Taifa la Israel na kufanya mambo mengi sana kukosa hata katika science na ugunduzi mkubwa sana
 
Labda aende Israel uone kama watampa hata Degree ndio ujue kuna nini maana Tanzania imekuwa mbali sana na Taifa la Israel na kufanya mambo mengi sana kukosa hata katika science na ugunduzi mkubwa sana

Israel ni Jimbo la 53 la Merakani, wamerakani walishampa ka-degree
 
Tumaini uko obsessed na Israel na Marekani.
Bora unipe Mjew kuliko shoga wako Mwarabu.

Hata Waturuki ,wajordanians anapokwenda JK wana mju vizuri Mjew.
Kusema kuwa Israel ni 53 state ya marekani ,ni propaganda za Al qaeda na wengine Jihadists ambao wamekubrainiwash wewe Tumaini na utanzania wako
 
Tumaini uko obsessed na Israel na Marekani.
Bora unipe Mjew kuliko shoga wako Mwarabu.

Hata Waturuki ,wajordanians anapokwenda JK wana mju vizuri Mjew.
Kusema kuwa Israel ni 53 state ya marekani ,ni propaganda za Al qaeda na wengine Jihadists ambao wamekubrainiwash wewe Tumaini na utanzania wako

Wewe uko obsessed na jina langu nenda kanisani wamehalalisha ushoga mimi sihitaji wanaume nina wake wawili wazuri

Get out of my way kama huna la kujibu kwenye thread ya nini kuandika about me wtf.
 
JK angepewa hiyo PhD na wazungu ningesema wamempa kwa kuishangaa nchi anayoiongoza mbali na kuwa na migodi mikubwa ya dhahabu barani Afrika bado ni ya pili kwa umasikini duniani kwa vile kapewa na waarabu basi kama si Loliondo nyingine inatafutwa basi wamenusa harufu ya uranium
 
wakuu Tumain na mmakonde,teh teh teh...

Hebu turejee kwenye mstari mara moja mwishowe mtaingiza makanisa na misikiti.Ngoja nionyeshe mfano wa kurejea ktk hoja...

Kwenye hoja,
Mimi naona Jk kwenye siasa za kimataifa kama Rais amefanikiwa but mimi nalia na Foreign policy yetu.Tukiwa na forign policy imara itakua ni muongozo wa Rais yoyote kitaasisi ktk kuimarisha uhusiano na mataifa ya nje bila kuhitaji mizururo isiyo na maana.Our foreign policy inampa rais mwanya wa kuzurura mno .

Hiyo PhD alopewa mkulu pia ni promo za chuo husika.
 
wakuu Tumain na mmakonde,teh teh teh...

Hebu turejee kwenye mstari mara moja mwishowe mtaingiza makanisa na misikiti.Ngoja nionyeshe mfano wa kurejea ktk hoja...

Kwenye hoja,
Mimi naona Jk kwenye siasa za kimataifa kama Rais amefanikiwa but mimi nalia na Foreign policy yetu.Tukiwa na forign policy imara itakua ni muongozo wa Rais yoyote kitaasisi ktk kuimarisha uhusiano na mataifa ya nje bila kuhitaji mizururo isiyo na maana.Our foreign policy inampa rais mwanya wa kuzurura mno .

Hiyo PhD alopewa mkulu pia ni promo za chuo husika.

Ninapingana na kufanikiwa kwa Rais/Tanzania katika sera ya nje na siasa za kimataifa zaidi ya kusafiri. Ukilinganisha na miaka ya nyuma, hivi karibuni sijasikia Tanzania ikitoa msimamo katika matukioa muhimu ya kimataifa zaidi ya kauli-wakati mwingine zinazokinzana-kati ya waziri wa mambo ya nje na Rais (Mfano suala la Zimbabwe). Vile vile sidhani kama sera ya nje ya sasa inampa Rais mwanya wa kusafiri kwa sababu watekelezaji wake wakuu walitegemewa wawe mabalozi aliowateua. Labda kwa sababu diplomasia ya karne 21 imebadilika.

Hivi wenye PhD za uhusiano wa kimataifa Tanzania watakuwa JK na Baregu sasa? Mkuu mwenye kufahamu ninaomba anijuze.
 
Mwenzenu JK kavuna, kaeni mkao wa kula hasa kwa vijana.
Kikwete avuna nafasi za masomo Uturuki
Imeandikwa na Na Mwandishi Maalumu (Habarileo)






Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepewa nafasi 130 za masomo katika vyuo vikuu vya Uturuki kwa vijana wa Tanzania , ikiwa sehemu ya ziara ya Kiserikali ya siku tatu nchini humo ambayo imemalizika jana.

Aidha, Uturuki imetangazwa kuwa kuanzia mwakani, wanafunzi wa Kitanzania ambao wataomba kuingia katika vyuo vikuu vya Uturuki hawatatakiwa kufanya mtihani maalumu kama ilivyo sasa.

Rais alipewa nafasi 30 za kwanza na Serikali ya Uturuki wakati alipokutana kwa mazungumzo rasmi na Rais wa Uturuki, Abdallah Gul kwenye Kasri ya Rais, mjini Ankara , mji mkuu wa Uturuki.

Nafasi nyingine 100 za masomo katika vyuo vikuu vya Uturuki alipewa na taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Medical and Education Foundation (Ishik) .

Nafasi hizo zilitangazwa mbele ya Rais Kikwete na Mwenyekiti wa Shule za Feza Schools, Ahmet Kara wakati wa mkutano kati ya Rais Kikwete na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu vya Uturuki kwa sasa.

Feza Schools ni sehemu ya Ishik, ambayo pia inaendesha shule za Feza katika Tanzania, ambazo zimetoa wanafunzi wengi wanaosoma katika vyuo vikuu vya Uturuki kwa sasa.

Akitangaza nafasi hiyo kwa namna ya kushtukiza, Kara alimwambia Rais Kikwete: ''Naomba radhi kuwa sikukujulisha mapema. Nilitaka kukushtukiza kwa zawadi maalumu. Napenda, kwa heshima kubwa, kutangaza kuwa taasisi yetu ya Ishik itatoa nafasi mpya 100 za masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania.''

Kara pia amemwambia Rais Kikwete kuwa ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kutoka Tanzania kujiunga na vyuo vikuu vya Uturuki, haitakuwa lazima kuanzia mwakani kwa wanafunzi hao kufanya mtihani maalumu wa kuingia vyuo hivyo.

Wakati huo huo Rais Kikwete ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Falsafa ya Udaktari katika Masuala ya Kimataifa na Chuo Kikuu cha Fatih cha Istanbul , Uturuki.

Mara baada ya kuwa ametunukiwa shahada hiyo, Rais Kikwete ametangaza kuwa naye anaitunuku shahada hiyo kwa wananchi wa Tanzania ambao wamechangia mafanikio ya utawala wake katika miaka minne iliyopita.

Akizungumza kabla ya kutunuku shahada hiyo, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Sharrif Ali, amesema kuwa uongozi wa chuo hicho kwa ushauri wa Baraza la Seneti la Chuo hicho umeamua kumtunukia Rais Kikwete shahada hiyo kwa sababu ya mchango wake mkubwa katika masuala ya kimataifa.

''Katika nafasi zako zote ulizozishikilia katika maisha yako yote, hasa ulipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ulisimamia kutatua migogoro mingi katika eneo la Maziwa Makuu ukiwamo ule wa Burundi, na zaidi uliposhika urais umeendelea kusuluhisha migogoro mingi,'' Profesa Ali amemwambia Rais Kikwete.

Profesa Ali ameongeza kuwa kwa kutoa Shahada hiyo ya Falsafa kwa Rais Kikwete, Chuo Kikuu cha Fatih kimepata mwakilishi, mtetezi na msemaji wa chuo hicho siyo tu katika Bara la Afrika bali duniani pote.

Rais Kikwete anakuwa mtu wa tatu kutunukiwa Shahada ya Udaktari na chuo hicho. Wengine ambao wamewahi kutunukiwa shahada ya namna hiyo, tokea kuanzishwa kwa chuo hicho cha sayansi, mwaka 1996, ni Rais wa Azerbaijan, Ilham Heydar Aglu Aliyev na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep T. Edorgan.

Katika hotuba yake ya kupokea shahada hiyo, Rais Kikwete ameelezea jinsi Bara la Afrika lilivyobadilika na kuwa Bara bora zaidi katika miaka ya karibuni iwe katika kujenga demokrasia na kujenga mataifa ya Bara hilo.

''Afrika siyo Bara la ovyo ama Bara lililo gizani kama baadhi ya watu wanavyopenda kuliita. Badala yake, Afrika ni Bara lenye kushamiri, lililojaa matumaini, na ambako mambo yanabadilika na kuwa mazuri zaidi. Afrika inapaa kuelekea kwenye mafanikio ya kiuchumi kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Hii inajionesha na kujithibitisha katika Bara zima la Afrika kutoka Cape Town hadi Cairo, kutoka Dakar hadi Dar es Salaam'' .

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa bado Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi. ''Kuna changamoto za kisiasa, kijamii, kiusalama na kiuchumi. Lakini changamoto kubwa zaidi ni ya kiuchumi, hasa katika kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi za Afrika na kuwainua Waafrika walio wengi kutoka kwenye umasikini.''

Ameongeza: ''Nchi 38 kati ya nchi 49 masikini zaidi kwenye dunia hii wanaishi katika Afrika, na wengi wao wanahemea wakiishi kwa kiasi kisichofikia dola moja ya Marekani (sawa na Sh 1,300) kwa siku.''

Rais Kikwete pia amezungumza hali ya kisiasa ya Afrika, hali ya kiuchumi katika Afrika, umuhimu wa nchi za Kiafrika kuongeza ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na uhusiano kati ya Afrika na Uturuki.

Leo usiku, Rais Kikwete na ujumbe wake, ameandaliwa chakula cha jioni na Gavana wa Istanbul na Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki kwenye mgahawa wa Feriye.
 
Back
Top Bottom