JK asaka umaarufu mchezoni

JK asaka umaarufu mchezoni

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2006
Posts
2,182
Reaction score
885
JK asaka umaarufu michezoni - Mbunge

na Charles Mullinda

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, amesema Rais Jakaya Kikwete, anajaribu kutafuta umaarufu kupitia jukwaa la michezo.

Mdee alisema hayo katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika juzi kwenye ofisi ndogo ya Bunge, Dar es Salaam kuhusu ziara ya timu ya Real Madrid hapa nchini.

Mdee alisema haoni umuhimu wa ziara hiyo itakayowagharimu mamilioni ya shilingi Watanzania kwa ajili kuwahudumia wachezaji nyota wa timu hiyo.

Alisema Kikwete ambaye sasa anaanza kunogewa sifa za mashabiki wa soka, anaweza kuiharibu sifa hiyo iwapo mashabiki wa kweli wa soka watafuatilia kwa karibu kitakachofanywa na wachezaji wa klabu hiyo hapa nchini.

“Sipingi ziara ya mastaa wa Madrid hapa bongo, lakini ninachojiuliza ni hizo gharama tutakazotumia kuwahudumia, ukizingatia kuwa ni wachezaji tajiri ambao wanalipwa mamilioni kwa siku.

“Madrid wanakuja kucheza na timu gani hapa kwetu, ipo kweli timu ya kucheza nao? Au wanakuja kutalii kwenye mbuga za wanyama na Watanzania waangalie sura zao kisha warudi zao Hispania?” alihoji Mdee.

Alisema anaamini Rais Kikwete ameamua kuwaalika Madrid akifikiria kuwa atakuwa amefanya kitu kikubwa kuliko kiongozi yeyote wa Tanzania, jambo ambalo litabaki akilini mwa Watanzania kwa muda mrefu na kumjengea umaarufu zaidi.

Alishauri kuwa kama nia ni kuiandaa timu ya taifa vizuri, ni bora pesa zitakazotumiwa kuileta Madrid zikatumika kuipeleka timu ya taifa ziara ya nchi za Ulaya, ambako itajipima nguvu na timu mbalimbali za huko.

“Ningemsifu na kukubaliana naye Rais Kikwete kama angewashawishi Madrid kuja nchini kwa gharama zao, kwa kuzingatia jinsi walivyo tajiri.

“Lakini tutaingia Gharama kubwa ambazo zingeweza kufanya mambo makubwa kwa timu yetu ya taifa wakati hata hao wachezaji wa Madrid sidhani kama watakuwa na muda na wachezaji, huu si wakati muafaka wa kualika timu kama hiyo kuja hapa nchini,” alisema Mdee.

Akiwa njiani Kwenda Havanna, Cuba, Septemba 13, Rais Kikwete alitua kwa muda Hispania na kuzuru Uwanja wa Bernabeu ambako alipewa jezi ya timu hiyo na alitumia nafasi hiyo kuialika timu hiyo kuzuru Tanzania wakati wa ufunguzi wa Uwanja mpya wa Taifa uliojengwa jijini.
 
Halima Mdee ni Mbunge wa viti maalum?
 
Back
Top Bottom