Mwambieni basi mheshimiwa akazane kujifunza kiingereza hasa grammar na pronounciation. Nimemsikiliza leo CNN ana problem sana na haya maeneo. Itabidi amuombe Mkapa ampige msasa kidogo.
Yaani swala la kenya ni dogo haliwezi kuchukua muda wa AU? Ati wao anashughulikia maswala ya maendeleo ya Afrika? Sasa ni maendeleo yapi ya Afrika watakayoshughulikia kama wataawaacha Waafrika walioko Kenya wauane wenyewe kwa wenyewe, wachomeane nyumba, na kuharibiana taratibu za maisha yao ?
Pumba kweli kweli hizi.
(Samahani kama hii tayari iko kwenye threads zingine)
salamu za lipumba kwa jk
Taarifa ya Mhe Profesa Lipumba juu ya Uteuzi wa Mhe Jakaya Kikwete kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa AU
Kufuatia kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba, ametoa taarifa ifuatayo:
Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Jakaya Kikwete kwa heshima kubwa aliyopewa na viongozi wenzake wa nchi za Afrika waliyomchagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa mwaka huu wa 2008.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimezipokea habari hizo kwa furaha kubwa na kinaiona heshima hiyo ni ya Tanzania na Watanzania wote kama Taifa bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa. Hapana shaka kwamba kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kuuongoza Umoja huo kutasaidia kuzidi kuipandisha chati Tanzania na kuitangaza kimataifa.......
Hii pia ni nafasi adhimu ya kukamilisha mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili kumpa nafasi Rais Kikwete ya kushughulikia vyema migogoro mingine ya kisiasa barani Afrika, ambalo litakuwa sehemu muhimu ya majukumu yake akiwa Mwenyekiti wa AU.
Namhakikishia Rais kuwa mimi binafsi na Chama cha CUF tutampa kila ushirikiano na msaada anaouhitaji katika kutimiza matumaini ya Waafrika wenzetu waliotuamini kuuongoza Umoja wa Afrika. Kwa mara nyengine tena, tunasema hongera Rais Kikwete.
DAR ES SALAAM
1 Februari, 2008
Wananchi wa Tanzania, walimpokea Lipumba na ni wananchi hao hao walimpokea Muungwana, sio kila ishu ni ya kuwa politicalization,
Kikwete kuwa mwenyekiti wa AU, ni heshima kubwa kwa Tanzania kama taifa, kama vile Lipumba kuwa UN, ni heshima kwa taifa letu pia,
Kama sisi JF hatuelewi hizi simple political facts, basi huko mtaaani hatuwezi kumsaidia mwananchi yoyote kama ambavyo lilivyo lengo letu hapa JF.
Itabidi amuombe Mkapa ampige msasa kidogo.
nampongeza jk kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa au. inabidi ajitahidi ili katika kipindi cha mwaka mmoja awe angalau
amefanikiwa katika jambo moja la kibara (regional issue).
hivi kwa nini mwalimu jkn alikwepa uenyekiti wa oau katika
kipindi chote cha miaka 24 ya uraisi wake? nadhani jibu la hili
linaweza kutueleza undani wa uenyekiti wa au.
WaTanzania haya matusi haya sio mazuri kwenye jamii yetu... unless you are sure off... please don't utter these kind of words...
Kwetu Mwanakwerekwe watu wana hali kama ya pale Kipawa... kwa hiyo naona unatutukana...Yakhee... tutatoana mijino humu...
Mwambieni basi mheshimiwa akazane kujifunza kiingereza hasa grammar na pronounciation. Nimemsikiliza leo CNN ana problem sana na haya maeneo. Itabidi amuombe Mkapa ampige msasa kidogo.
Mtazamo wangu unanituma kutoshereheka na uenyekiti wa rais wetu huko AU.
Ili niwe clear, naomba nifahamishwe faida tuipatayo kwa kuwa mwenyekiti wa AU hasa kiuchumi na kiteknolojia.
Pili ni nani ambaye ana nguvu ya maamuzi ktk vikao vyao hao waheshimiwa. Maana tangu vuguvugu la ukombozi wa bara, sisi tumetumika huku tukiiacha nchi yetu fukara wa kutupwa. Lazima tuamke na kuhamasika ili kuweza kusonga mbele kama tunisia (utata), SA, misri na wengineo. Enzi za chenga twawala zimepitwa na wakati na sasa ushindi ni dk tisini na haijalishi how best you can play but how goals you can score and so on.
Watanzania tuache ulimbukeni wa kushabikia shabikia bali tukae na kufikiri what are the prior issues to tackle.
Hongera Mrisho Jakaya ila Am not proud until u create an opportunity for our country.